Tuesday 14 May 2013

Re: [wanabidii] IKULU : DR SLAA AACHE UZUSHI

Serikali ndiyo muasisi wa udini hapa nchini. Sasa baada ya kuona udini umeota mizizi akilini mwa wananchi, wameamua ku-deflect mawazo ya wananchi kwa kuwaaminisha kwamba kila tukio baya linalotukia hapa nchini ni UGAIDI. Serikali inataka kuwaondoa wananchi kutoka kwenye UDINI na kuwaelekeza kwenye UGAIDI. Baada ya wananchi kuwa sugu kwa ugaidi sijui wataambia nini tena. Na, kwa bahati mbaya, baadhi ya wananchi wenye akili za mbayuwayi wanakubali bila kupima wala kutumia akili zao binafsi, badala yake wanategemea akili za kisiasa za serikali.
 
Akili za kuwambiwa muwe mnachanganya na za kwenu ndugu zangu. Mbona matukio ya kuuliwa kwa Mwangosi na majaribio ya kuuliwa kwa Dr Ulimboka na Kibanda hayajaitwa matukio ya kigaidi na serikai ilishaacha kuyafanyia upelelezi kitambo? Mnaweza kuniambia upelelezi wa kesi ya Dr Ulimboka (kwa zaidi ya mwaka sasa) umeibua watuhumiwa wangapi so far? Na mbona yule mtuhumiwa wa maigizo (Joshua Mulundi) hajashitakiwa kwa kosa la UGAIDI, ijapokuwa alikuwa amenuia kuua, badala yake ameshitakiwa kwa kosa la kushambulia? Acheni kupumbazwa kirahisi hivyo na serikali!
 
Msidhani kwamba kila mtanzania ni zezeta---watanzania wa wale sio wale wa mwaka 1947! How the hell can the government term a crime as terroristic so abruptly before detectives' investigation reveals the same? Wao ni malaika wa aina gani (au Mungu) mpaka wajeu tukio ni la kigaidi hata kabla polisi hawajaanza upelelezi? Acheni kukubali kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa na hawa wanasiasa wachumia tumbo. Jueni kwamba tunaumizwa sana kuwaona ndugu zetu wakiuliwa kikuku huku serikali ikifanya maigizo yasiyokuwa na tija. Tafakari, chukua hatua!


From: Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>
To: Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, May 14, 2013 2:39 PM
Subject: [wanabidii] IKULU : DR SLAA AACHE UZUSHI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mheshimiwa Wilbroad Slaa, leo, Jumatatu, Mei 13, 2013, amekaririwa na gazeti moja akidai kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na timu yake ya kampeni, "ilikuwa ikisaka kura kwenye nyumba za ibada na kumwaga sumu mbaya ya udini ambayo sasa inaitesa Serikali na taifa" kwenye Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2010.

Aidha, katika habari hiyo iliyoandikwa chini ya kichwa cha habari, "Dk. Slaa amlipua JK"kwenye gazeti linalounga mkono CHADEMA la Tanzania Daima, Mheshimiwa Slaa anadai kuwa migogoro ya sasa ya kidini "inajengwa au kutengenezwa na Serikali iliyojikita kusambaza sumu ya udini katika misikiti wakati wa kampeni za Urais mwaka 2010".

Kwa hakika, hakuna namna nyingine ama namna bora zaidi ya kuielezea kauli hii ya Mheshimiwa Slaa isipokuwa kwamba kauli hiyo ni riwaya nyingine isiyokuwa na mshiko. Ni uongo mtupu. Yake Mheshimiwa Slaa ni maneno yasiyokuwa na ukweli wowote. Ni uzushi na santuri ambayo imezoeleka sasa kwa wananchi.

Kauli ya Mheshimiwa Slaa ni mwendelezo wa mtiririko usiokuwa na mwisho wa ghiriba ambazo kamwe hazitafanikiwa za Mheshimiwa Slaa kuwahadaa wananchi kuhusu ukweli wa mambo ulivyo katika nchi yetu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na timu yake ya kampeni kamwe hawakufanya kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2010, ama wa mwaka mwingine wowote, katika nyumba yoyote ya ibada iwe msikitini ama kanisani ama hekaluni ama nyumba nyingine yoyote ya ibada mahali popote katika nchi yetu.

Mheshimiwa Rais Kikwete hajawahi hata kufikiria kuchanganya dini na siasa. Hana sababu ya kufanya hivyo. Anaelewa fika madhara ya udini kwa mustakabali wa nchi yetu, kwa umoja wa taifa letu na kwa mshikamno wa wananchi wake. Yoyote anayejaribu kumbebesha Rais Kikwete msalaba wa udini ana lake jambo na ni vyema atuambie fika Rais alitumia Msikiti upi, ama Kanisa lipi, mahali gani na kwa nyakati gani kufanya kampeni.
Vinginevyo, kauli ya Mheshimiwa Slaa itabakia ni kauli tu inayostahili kupuuzwa na wananchi, itabakia ni kauli ya mtu mzima anayetapatapa na kufanya jitihada kubwa kujivunjia mwenye heshima kwa kutunga na kusambaza uongo.

Tunanapenda kumshauri Mheshimiwa Slaa kuwa kama hana jambo la maana la kuwaambia wananchi ama ameishiwa na hoja ni vyema anyamaze, awaachie wananchi waendelee na shughuli zao za maendeleo, kuliko kuendeleza riwaya zake zisizokuwa na mshiko. Yake ni santuri iliyowachosha wananchi.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
13 Mei, 2013


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 


0 comments:

Post a Comment