Friday 17 May 2013

RE: [wanabidii] Dai la kufutwa kashifa na kutakwa radhi; Msigwa amtaka Kinana awahi mahakamani

Mpaka 2015 itapofika Wanasheria mtakuwa mmepata dili za kutosha kwa mambo haya….Siasa za digitali..

 

 

From: wanabidii@googlegroups.com [mailto:wanabidii@googlegroups.com] On Behalf Of Abdalah Hamis
Sent: Friday, May 17, 2013 11:57 AM
To: Wanabidii
Subject: [wanabidii] Dai la kufutwa kashifa na kutakwa radhi; Msigwa amtaka Kinana awahi mahakamani

 

LAW OFFICES 
OF 
ERIC S. NG'MARYO
                                                            ADVOCATE                          
TEL: +255 27 2753898
                                                            PRIVATE BAG                   
TEL/FAX: +255 27 2750343
                                                                18 BOMA ROAD, MOSHI         
E-MAIL: semaericbabu@yahoo.com
TANZANIA - EAST AFRICA

14 MEI, 2013

Mheshimiwa Mchungaji Peter Simon Msigwa, Mbunge 
Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini
S.L.P. 316
IRINGA.


BILA ATHARI
(WITHOUD PREJUDICE)

Mheshmiwa Mchungaji Msigwa,

Salaam.

Yah: 
DAI LA KUFUTIWA KASHFA NA KUTAKWA RADHI


1.     Nakuandikia kwa maagizo niliyopewa na Mteja wangu, Ndugu Abdulrahman Omar Kinana, kufuatia matamshi yako ya uwongo ambayo yamemkashifu, kumfedheshesha na kumshushia hadhi. Matamshi hayo uliyatoa mchana wa tarehe 21 Aprili, 2013 katika mkutano wa hadhara wa kisiasa uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mbugani, Wilaya ya Nyamagana, jijini Mwanza. Mkutano huo ulihudhuriwa na watu wengi. Pamoja na watu hao walikuwepo pia wandishi wa habari, wakiwemo wanahabari wa magazeti, radio na televisheni. Habari zenye maneno yako ya kashfa zimeenea nchi nzima na duniani kote kwa njia ya habari elektroniki, ikiwepo mitandao ya jamii. Habari hizo zinaendelea kusomwa hadi sasa, na zitabaki kuwa kumbukumbu ya kudumu katika intaneti na kwenye hifadhi nyingine za habari.

2.     katika mkutano huo, ulisikika na kurekodiwa ukisema maneno mengi ya kashfa kwa Mteja wangu, yakiwemo haya yafuatayo:

"Kinana (na naomba waandishi wa habari mnisikie na nyie Usalama wa Taifa mkapeleke habari) hana sifa za kupita barabarani na kuwaambia Watanzania waiamini CCM. Kinana mikono yake si misafi hata kwenye NASACO, Shirila la Meli Tanzania, kuna harufu ya ufisadi ndani yake; ajibu hoja.... Kinana meli zake ndizo zilizohusika kubeba mapembe nchi hii. Hajajibu hoja hizo! Kwa siku katika nchi hii tembo sitini na saba wanauawa...

Hao ndio wanaokifadhili Chama cha Mapinduzi wakina Kinana halafu wanakuja eti kuwashawishi Watanzania muwasikilize na kwamba Chma Cha Mapinduzi eti ni kizuri. Halafu leo tukikaa ndani ya Bunge tunapojaribu kuwatetea wananchi tumeacha majimbo yetu. Haya mambo ninayoongea ni hatari kwa sababu haya yote ni majangili ni organised crime ni mtandao wa kimafia uko duniani kote, unaweza ukatuua lakini wabunge tumesimama tunawatetea..."


Umeshatamka maneno haya au, yanayofanana na haya katika hotuba zako nyingine nje ya Bunge.

3.     Katika hotuba hizo na ile ya Mwanza, uliahidi kuzungumza zaidi uwapo Bungeni. Nia ya ahadi hiyo ilikuwa kunoa hamu ya umma kufuatilia zaidi tuhuma zako dhidi ya Ndugu Kinana na pia kujaribu kujificha kwenye kivuli cha kinga ya Bunge; mambo yote mawili yakiwa ni matumizi maovu na mabovu ya nafasi yako ya kisiasa na ya ubunge.

4.     Baada ya ahadi yako katika matamshi ya Mwanza, uliandika na kutoa hotuba ukiwa ni Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Wizara ya Maliasili na Utalii Kuhusu Makadirio na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha wa 2013/2014. Hotuba hiyo ina Kumbukumbu Na HU/08/2013. Katika andiko hilo na hotuba hiyo, bayana na kwa taathira, na kwa uwongo na nia ovu, ulimtuhumu Mteja wangu Ndugu Abdulrahman Kinana, kuwa ni mhusika katika ujangjili wa tembo na biashara haramu ya meno ya tembo, ikiwemo usafirishaji haramu nje ya nchi wa meno ya tembo.

5.     Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania likawa ni njia yako ya kubainisha zaidi na kuongea chumvi kashfa uliyotoa kule Mwanza na kwingineko dhidi ya Mteja wangu, Ndugu Abdulrahman Kinana. Huna kinga ya Bunge kwa matamko dhidi ya Ndugu Kinana, maana hotuba yako Bungeni ilidhihirisha kashfa uliyoitamka awali nje ya Bunge.

6.     Umma unaamini matamko yako na hawayachukulii kwamba ni upuuzi wa mtu asiye makini au ni ujanja-ujanja na porojo za kisiasa. Wengi wa wale waliopiga kura katika Jimbo la Iringa Mjini walikuchagua uwawakilishe katika Bugne la nchi yao. Maneno yako ya uwongo yataaminiwa na wengi wasiojua ukweli wa matamko yako ya uzushi na hoja zako zisizo na msingi. Madhara na hasara uliyosababisha kwa Mteja wangu ni kubwa na zinazoendelea kumuumiza. Hasara hizi zinakera na kuharibu zaidi pale inapodhihirika kwamba umemkashifu, umemtwesha na kumchafua jina kwa sababu zako za kisiasa na kwa nia ya kujipatia umaarufu wambao huna haki nao.

7.     Ndugu Abdulrahman Kinana ni mwanasiasa mweledi na mtu mwadilifu. Ana sifa njema baina ya mafariki zake na katika duru za wanasiasa na viongozi wenzake. Anapendwa na kuheshimiwa na umma mzima wa Tanzania na nje ya Tanzania. Tangu ujana wake, Ndugu Kinana ameshafanya kazi anuwai za umma na ameshika nyadhifa na dhamana nyingi muhimu nchini mwetu. Anaaminiwa na kuthaminiwa na makada wenzie wa Chama Cha Mapinduzi, na ndio maana ametwikwa jukumu la kukiongoza Chama chake katika wadhifa wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi. Ndugu Abdulrahman Kinana asingepewa dhamana zote hizo iwapo angekuwa na sifa ya ujangili na uhalifu kama ulivyoeleza katika hotuba yako ya hadhara ya kisiasa kule Katika uwanja wa Shule ya Msingi Mbugani, jijini Mwanza na kwingineko.

8.     Watu waliosikia hotuba zako, ikiwemo ile ya Mwanza, na kuziunganisha na hotuba yake Bungeni walitaharuki sana kusikia Ndugu Kinana anatuhumiwa kwa makosa ya jinai ambayo yamempotezea sifa zote za kuwa nje ya gereza, sembuse kuwa kiongozi wa namna yoyote katika umma. Umemwonea sana, maana umetuhumu uwongo na umefanya hivyo mahali ambao hakuwepo na asingeweza kukujibu au kujitetea au kukanusha kikamilifu uwongo na uzushi ulioutunga dhidhi yake kwa manufaa yako maovu ya kisiasa.

9.     Ndugu Kinana ana nia ya kukufungulia kesi ya madai katika Mahakama Kuu ya Tanzania ili uchafu uliopaka kwenye jina lake usafishwe kisheria, na wewe uwajibishwe kwa madhara na hasara ulizomsababishia.

10.   Mtu wa wadhifa wa uwakilishi wa watu na mtu wa tasnia yako ya dini anapaswa kuona mapema makosa na uonevu alioufanya na kuujutia kwa dhati. Nakuhimiza na kukudai ufanye hivyo bila kuchelewa. Nakudai ipa utufe kauli yako ya uwongo uliyotoa dhidi ya Ndugu Abdulrahman Kinana katika mkutano wako wa hadhara wa kisiasa ulioufanya jijini Mwanza mnamo terhe 21 Aprili, 2013, na mikutano mingine kwingineko, na umtake radhi Mteja wangu ukitumia maneno ambayo hayataacha shaka kwamba kweli umefuta kauli yako iliyomkashifu. Zaidi ya hayo, nakudai umtake radhi Ndugu Abdulrahman Kinana kama wafanyavyo watu waadilifu wanaoheshimiwa, waishio katika jamii za waungwana kama Tanzania. Nadai pia ufute usemi wako wa kashfa na umtake Mteja wangu radhi katika kipindi cha siku 21 (Ishirini na Moja) kutoka tarehe ya barua hii.

11.   Iwapo utakuwa na ujasiri na uungwana huo, basi Mteja wangu anao ujasiri na uungwana wa kuacha kukufungulia kesi ya madai ambayo tayari nimeshaiandaa dhidi yako.

12.   Nakuangaliza na kukutahadharisha kwamba iwapo hutatimiza matakwa ya Mteja wangu kama yalivyoainishwa kwenye barua hii, basi kesi itakayokuja dhidi yako itakuwa na madai makubwa na mengi kuliko yale yaliyotajwa humu, na unaweza kubebeshwa mzigo wa uharibifu, hasara na madhara uliyomsababishia Mteja wangu, pamoja na gharama za kesi nzima, ambazo zote zinaweza kufikia mamilioni ya Shilingi za Kitanzania.



Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/05/dai-la-kufutwa-kashifa-na-kutakwa-radhi-msigwa-amtaka-kinana-awahi-mahakamani.html#ixzz2TXRtMzi4

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment