Friday 17 May 2013

Re: [wanabidii] Charles Mullinda ajitoa kwenye Jukwaa la Wahariri Tanzania

Unajitoaje baada ya kusimamishwa!!?? Hii imekaaje? Ungesubiri utumikie adhabu wakurudishe ndipo ujitoe. Kwa sasa hivi kile cha mwanzo ndicho kinachosimama katika kumbukumbu, ambacho ni: ulimesimamsishwa uanachama wa TEF. 

Kitila

Dr Kitila Alexander Kanyama MKUMBO
Senior Lecturer in Psychology and Education
School of Education
University of Dar es Salaam
Tanzania

Currently:  
Dean, Faculty of Education, Dar es Salaam University College of Education (DUCE) of the   University of Dar es Salaam

2013/5/17 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
Charles Mullinda
Mhariri Mtanzania Jumatano
 
Kaimu Mwenyekiti
Jukwaa la Wahariri

YAH: KUJITOA KWENYE JUKWAA

Napenda kukufahamisha kuwa nimeamua kujitoa kwenye Jukwaa la Wahariri kwa sababu siridhiki na mwenendo wa Jukwaa hilo.

Nimeamua kujitoa kwa sababu sijaridhishwa na uamuzi uliofikiwa wa kuingilia uhuru wa habari na kufumbia macho baadhi ya mambo ambayo ninaamini hayapaswi kufumbiwa macho.

Uamuzi wangu huu pia unatokana na jinsi jukwaa linavyotumia nguvu kubwa kuficha ukweli unao wahusisha
baadhi ya wahariri ambao gazeti hili lilibaini kuwa walikuwa na mawasiliano yenye utata na aliyekuwa mtuhumiwa wa ugaidi, Joseph Ludovick.

Aidha, siridhishwi na jinsi baadhi ya wahariri wanavyoshambuliwa na wahariri wenzao katika magazeti yao pasipo Jukwaa kuchukua hatua huku kwa upande mwingine likitumia nguvu kubwa na pesa nyingi kuwalinda baadhi ya wahariri ambao nyendo zao zinatia mashaka.

Kikao cha kwanza na TEF na kilichofanyika leo kimedhihirisha pasipo mashaka kuwa TEF iliamua kuwa na ajenda maalumu ya kumshughulikia Mullinda kwa kuwa tu nilionyesha mawasiliano ya Deodatus Balile na Ansbert Ngurumo dhidi ya Ludovick kama ambavyo gazeti la Tanzania Daima lilivyoonyesha mawasiliano ya Dennis Msaki na Ludovick.
Ripoti ya timu iliyoundwa kuchunguza ukweli wa habari iliyoandikwa na gazeti la Mtanzania Jumatano ina upungufu mkubwa wa kimantiki ambao hata kwenye kikao niliuonyesha lakini haukusikilizwa.

Ushahidi wa Ngurumo kumtuma pesa Ludovick upo wazi, lakini hakuna mtu anayeliangalia hilo kwa sababu tu timu ile iliundwa kumshughulikia Mullinda kwa sababu aliandika vigogo wa TEF ambao wako karibu na viongozi wa TEF.
Nimeamua kujitoa baada ya kubaini kuwa jukwaa linafanya kazi kwa ajili ya maslahi ya watu binafsi.

Kwa taarifa hii naamini utaratibu wa kawaida wa kuagana utazingatiwa.

Charles Mullinda.

Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/05/charles-mullinda-ajitoa-kwenye-jukwaa-la-wahariri-tanzania.html#ixzz2TXSIcqEO

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment