Monday 20 May 2013

Re: [wanabidii] Charles Mullinda ajitoa kwenye Jukwaa la Wahariri Tanzania

Felix,
Demokrasia inakuruhusu kuwaza na kutegemea mengi kama unavyosema. Ila Mulinda aliandika Mtandao Hatari, kwa mtazamo wa hao wahariri aliocheka nao, kula nao na kusafiri nao wakasema kuna kasoro. Yeye akasema anafahamu mengi na ana ushahidi wa kile alichokiandika, kama akipewa nafasi basi ataweka wazi mengi kuhusu madai yake. Akapewa nafasi tena mkutano wa wahariri uliounda kamati yeye alikuwapo. Kamati ikamsikiliza yeye na wengine, taarifa ikaandikwa na ikasomwa yeye akiwapo. Akatoa utetezi wake, wahariri wakapima huo utetezi wakamkuta na hatia, wakamsimamisha.
 
Kwa maana hiyo taratibu za kidemokrasia zilifuatwa yeye akiwa mshiriki kamili wa vikao vya TEF. Inawezekana hakuridhika, hilo ni jambo jingine. Kama kuna mambo mengine zaidi anaweza kuendelea kuandika maana sisi hatukumfukuza kazi, bado ni Mhariri wa Mtanzania Jumatano ila siyo sehemu ya TEF maana amekosa sifa kwa mujibu wa jukwaa letu. Maana ya kumsimamisha uanachama ni kumpa fursa ya kutafakari conducts zake na kama akiona anaweza atarejea. Lakini baada ya kumsimamisha yeye alitangaza kujitoa kwenye TEF, huo ni uamuzi wake ambao mimi binafsi ninauheshimu.
 
Suala la waandishi wa habari kulalamikia wahariri ni sehemu ya demokrasia pia. Wanalalamikia uhuru wa wahariri kuwa na chama chao au umoja wao wa kukutana na kufanya mambo yao! Hili ni tatizo nchini mwetu kwamba vyama vingi vya waandishi wa habari vilianzishwa na kufa. Taja, AJM na vingine kadha wa kadha. Hivi leo tuna Press Clubs karibu katika mikoa yote nchini, lakini waandishi wa habari hawako tayari kuwa wanachama wa klabu hizo kwa sababu zao zao binafsi. Kigezo ni kwamba wanataka kuwa huru, ukijiuliza uhuru dhidi ya nani? Katika mazingira ya sasa ni ujinga na upuuzi kufikiri kwamba ,mwandishi wa habari anaweza kusimama peke yake.
 
Nchi yetu na mazingira ya sasa ambako mtu kama Kibanda anaweza kufanyiwa alivyofanyiwa, vifo vya waandidhsi wa habari na mengine mengi ni utumwa kufikiri kwamba mnaweza kuishi katika tasnia ya habari bila kuwa na umoja. TEF kama taasisi inayokua lazima ikosolewe kama inakosea, lakini kasoro hizo haziondoi umuhimu wa kuwapo kwake. TEF imeonyesha njia kwamba waandishi wa habari wanaweza kuwa na umoja wao na ukafanya kazi na kujisimamia wenyewe. Msipoweza kujisimamia wajuzi kutoka nje ya tasnia watakuja kuwasimamia. Tuache kutukuza vya wengine, tukuzeni na kuheshimu kile kilicho chenu.

2013/5/20 Felix Mwakyembe <fkyembe@gmail.com>
Nionavyo mimi, suala la Mulinda ni zaidi ya haya tunayoyasikia sasa, ukisoma kwa makini maandiko yake, sio kwamba anakurupuka, na ndugu zangu nao unapowasoma unaiona jazba.

Hawa watu walikuwa pamoja, walikaa pamoja kwenye jukwaa lao, walikula pamoja, walicheka pamoja hadi kwenye ziara zao ambazo waandishi wa habari walipozihoji waling'aka, leo wanavuana nguo hadharani, na kadri wanavyoendelea kuna mengi yataanikwa.

Huo ni mtazamo wangu ambapo huko nyuma nilitahadharisha kuhusu mabishano kwenye kwenye mitandao, lakini sasa nadhani muendelee tu tuweze kuwaelewa zaidi!

Felix

2013/5/17 Kitila Mkumbo <kitilam00@gmail.com>
Unajitoaje baada ya kusimamishwa!!?? Hii imekaaje? Ungesubiri utumikie adhabu wakurudishe ndipo ujitoe. Kwa sasa hivi kile cha mwanzo ndicho kinachosimama katika kumbukumbu, ambacho ni: ulimesimamsishwa uanachama wa TEF. 

Kitila

Dr Kitila Alexander Kanyama MKUMBO
Senior Lecturer in Psychology and Education
School of Education
University of Dar es Salaam
Tanzania

Currently:  
Dean, Faculty of Education, Dar es Salaam University College of Education (DUCE) of the   University of Dar es Salaam

2013/5/17 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
Charles Mullinda
Mhariri Mtanzania Jumatano
 
Kaimu Mwenyekiti
Jukwaa la Wahariri

YAH: KUJITOA KWENYE JUKWAA

Napenda kukufahamisha kuwa nimeamua kujitoa kwenye Jukwaa la Wahariri kwa sababu siridhiki na mwenendo wa Jukwaa hilo.

Nimeamua kujitoa kwa sababu sijaridhishwa na uamuzi uliofikiwa wa kuingilia uhuru wa habari na kufumbia macho baadhi ya mambo ambayo ninaamini hayapaswi kufumbiwa macho.

Uamuzi wangu huu pia unatokana na jinsi jukwaa linavyotumia nguvu kubwa kuficha ukweli unao wahusisha
baadhi ya wahariri ambao gazeti hili lilibaini kuwa walikuwa na mawasiliano yenye utata na aliyekuwa mtuhumiwa wa ugaidi, Joseph Ludovick.

Aidha, siridhishwi na jinsi baadhi ya wahariri wanavyoshambuliwa na wahariri wenzao katika magazeti yao pasipo Jukwaa kuchukua hatua huku kwa upande mwingine likitumia nguvu kubwa na pesa nyingi kuwalinda baadhi ya wahariri ambao nyendo zao zinatia mashaka.

Kikao cha kwanza na TEF na kilichofanyika leo kimedhihirisha pasipo mashaka kuwa TEF iliamua kuwa na ajenda maalumu ya kumshughulikia Mullinda kwa kuwa tu nilionyesha mawasiliano ya Deodatus Balile na Ansbert Ngurumo dhidi ya Ludovick kama ambavyo gazeti la Tanzania Daima lilivyoonyesha mawasiliano ya Dennis Msaki na Ludovick.
Ripoti ya timu iliyoundwa kuchunguza ukweli wa habari iliyoandikwa na gazeti la Mtanzania Jumatano ina upungufu mkubwa wa kimantiki ambao hata kwenye kikao niliuonyesha lakini haukusikilizwa.

Ushahidi wa Ngurumo kumtuma pesa Ludovick upo wazi, lakini hakuna mtu anayeliangalia hilo kwa sababu tu timu ile iliundwa kumshughulikia Mullinda kwa sababu aliandika vigogo wa TEF ambao wako karibu na viongozi wa TEF.
Nimeamua kujitoa baada ya kubaini kuwa jukwaa linafanya kazi kwa ajili ya maslahi ya watu binafsi.

Kwa taarifa hii naamini utaratibu wa kawaida wa kuagana utazingatiwa.

Charles Mullinda.

Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/05/charles-mullinda-ajitoa-kwenye-jukwaa-la-wahariri-tanzania.html#ixzz2TXSIcqEO

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
Neville C. Meena,
Secretary General,
Tanzania Editors Forum - TEF,
Dar es Salaam - Tanzania.
Cell: +255 - 787 - 675555
        +255 - 753 - 555556
 
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment