Friday 17 May 2013

Re: [wanabidii] Charles Mullinda ajitoa kwenye Jukwaa la Wahariri Tanzania

Mi nahisi huyu Mullinda ana hoja za msingi, asikilizwe siyo kufukuzwa na wala siyo kujitoa uanachama!
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

From: Reginald Miruko <rsmiruko@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Fri, 17 May 2013 13:47:37 +0300
To: wanabidii<wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Charles Mullinda ajitoa kwenye Jukwaa la Wahariri Tanzania

Hiyo ilikuwa reaction ya tukio hili:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

1.               Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) katika kikao chake leo, Jumatano, Mei 15, 2013 limemsimamisha uanachama kwa muda usiojulikana, Mhariri wa Mtanzania Jumatano, Charles Mulinda. Kwa maana hiyo Mulinda ataendelea kuwa nje ya TEF hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo.

2.               TEF imechukua uamuzi huo baada ya kupokea na kujadili kwa kina taarifa ya Kamati ndogo ya wahariri watatu ambayo iliongozwa na Mhariri wa Nipashe, Jesse Kwayu kwa ajili ya kuchunguza habari iliyochapishwa na Gazeti la Mtanzania, Jumatano Aprili 17 mwaka huu ikiwa na kichwa kisemacho "Mtandao Hatari".

3.               Habari hiyo iliwataja wahariri wawili, Ansbert Ngurumo wa Tanzania Daima na Deodatus Balile wa Jamhuri kuwa ni washirika wa  Joseph Ludovick, mshitakiwa katika kesi ambayo ilikuwa ikihusishwa na ugaidi (kabla ya kubadilishwa na mahakama) lakini ikiwahusisha kwa namna moja au nyingine na tukio la kuumizwa kwa Mwenyekiti wa TEF, Absalom Kibanda.

4.               Yalikuwa ni maoni ya wahariri wengi katika Mkutano wa April 18, 2013, kwamba habari hiyo ilikuwa na upungufu mkubwa kitaaluma, hivyo kuamua kuchunguza habari hiyo na kubaini iwapo kulikuwa na ukiukwaji wa maadili na misingi ya kitaaluma ya habari.

5.           0 Kamati hiyo pamoja na mambo mengine ilipaswa kuchunguza yafatayo:

5.1                    Kuchunguza mazingira ya kuchapishwa kwa habari hiyo na kama kulikuwa na msukumo wowote nyuma ya kuandikwa kisha kuchapishwa kwake.

5.2                    Kuchunguza chanzo/vyanzo vya habari hiyo na kubaini kama kulikuwa na ajenda maalum.

5.3                    Kuchunguza ushahidi wa tuhuma zilizotolewa dhidi ya Deo Balile na Ansbert Ngurumo (kama Mullinda) alivyokiambia kikao cha Aprili 18 kwamba alikuwa na ushahidi wa yale aliyoandika.

5.4                    Kuchunguza na kubaini iwapo habari husika ilikidhi vigezo vya kitaaluma.

6.           0  Katika uchunguzi wake Kamati ilibaini yafuatayo:

6.1        Kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa maadili ya kitaaluma katika mchakato mzima uliowezesha kuandikwa na kuchapwa kwa habari husika na kwamba habari hiyo haikuwa na sifa wala vigezo vya kihabari.

6.2        Mulinda akiwa Mhariri wa Gazeti la Tanzania Jumatano, alishindwa kuthibitisha usahihi wa taarifa hiyo na hata alipotakiwa kutoa ushahidi wa tuhuma dhidi ya wahariri aliowataja hakuweza kufanya hivyo.

6.3        Tangu kuandikwa kwake, kuhaririwa na hadi kuchapishwa kwa taarifa hiyo, hakukuwa na vikao rasmi vya wahariri ambavyo kimsingi ndivyo vinavyopaswa kufanya uamuzi kwamba ni habari gani ichapishwe na kwa vigezo gani.

6.4        Kwamba kulikuwa na nguvu (msukumo) ya ziada katika kuchapishwa kwa habari hiyo kwani taarifa kwamba habari hiyo ingechapishwa zilifahamika siku moja kabla ya kuchapishwa kwa habari yenyewe.

6.5        Kwamba Mhariri husika alithibitika kukaidi uamuzi wa TEF kwa kuendeleza mjadala huo katika Makala yake ya Mchokonozi ya Mei 8, 2013 iliyobeba kichwa cha Habari "Simba hapigani na Binadamu" huku akijua kuwa kufanya hivyo ni kuingilia Uhuru wa Kamati iliyokuwa ikiendelea na uchunguzi wa suala hilo.

7. 0 Hitimisho

7.1                    Kwa kuzingatia matokeo hayo TEF inaushauri Uongozi wa New Habari (2006) Ltd na vyumba vingine vya habari  kuboresha mfumo wake wa usimamizi wa uhariri ili kuziba mianya kwa habari tata kama hiyo ya "Mtandao Hatari" kupenya na kuwaumiza baadhi ya watu bila kuwapo kwa uthibitisho wa tuhuma husika.

7.2                  TEF inaendelea kuchukua hatua nyingine za ndani kuimarisha usimamizi wa nidhamu na maadili kwa wahariri ikiwa na itaendelea kuchukua hatua dhidi ya ukiukwaji wowote ule wa kitaaluma utakaofanywa katika vyombo vya habari.

Imetolewa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)

Dar es Salaa, Mei 15, 2013

RSM

2013/5/17 ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk>
Mhariri ndugu yangu,
 
Itoshe tu kusema POLE.
 
K.E.M.S.
From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
To: Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Friday, 17 May 2013, 1:57

Subject: [wanabidii] Charles Mullinda ajitoa kwenye Jukwaa la Wahariri Tanzania

Charles Mullinda
Mhariri Mtanzania Jumatano
 
Kaimu Mwenyekiti
Jukwaa la Wahariri

YAH: KUJITOA KWENYE JUKWAA

Napenda kukufahamisha kuwa nimeamua kujitoa kwenye Jukwaa la Wahariri kwa sababu siridhiki na mwenendo wa Jukwaa hilo.

Nimeamua kujitoa kwa sababu sijaridhishwa na uamuzi uliofikiwa wa kuingilia uhuru wa habari na kufumbia macho baadhi ya mambo ambayo ninaamini hayapaswi kufumbiwa macho.

Uamuzi wangu huu pia unatokana na jinsi jukwaa linavyotumia nguvu kubwa kuficha ukweli unao wahusisha
baadhi ya wahariri ambao gazeti hili lilibaini kuwa walikuwa na mawasiliano yenye utata na aliyekuwa mtuhumiwa wa ugaidi, Joseph Ludovick.

Aidha, siridhishwi na jinsi baadhi ya wahariri wanavyoshambuliwa na wahariri wenzao katika magazeti yao pasipo Jukwaa kuchukua hatua huku kwa upande mwingine likitumia nguvu kubwa na pesa nyingi kuwalinda baadhi ya wahariri ambao nyendo zao zinatia mashaka.

Kikao cha kwanza na TEF na kilichofanyika leo kimedhihirisha pasipo mashaka kuwa TEF iliamua kuwa na ajenda maalumu ya kumshughulikia Mullinda kwa kuwa tu nilionyesha mawasiliano ya Deodatus Balile na Ansbert Ngurumo dhidi ya Ludovick kama ambavyo gazeti la Tanzania Daima lilivyoonyesha mawasiliano ya Dennis Msaki na Ludovick.
Ripoti ya timu iliyoundwa kuchunguza ukweli wa habari iliyoandikwa na gazeti la Mtanzania Jumatano ina upungufu mkubwa wa kimantiki ambao hata kwenye kikao niliuonyesha lakini haukusikilizwa.

Ushahidi wa Ngurumo kumtuma pesa Ludovick upo wazi, lakini hakuna mtu anayeliangalia hilo kwa sababu tu timu ile iliundwa kumshughulikia Mullinda kwa sababu aliandika vigogo wa TEF ambao wako karibu na viongozi wa TEF.
Nimeamua kujitoa baada ya kubaini kuwa jukwaa linafanya kazi kwa ajili ya maslahi ya watu binafsi.

Kwa taarifa hii naamini utaratibu wa kawaida wa kuagana utazingatiwa.

Charles Mullinda.

Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/05/charles-mullinda-ajitoa-kwenye-jukwaa-la-wahariri-tanzania.html#ixzz2TXSIcqEO

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment