Sunday 5 May 2013

FW: [wanabidii] AHADI KUMI ZA TANU

Angalia zinavyovunjwa na wajanja wetu wa leo:
 
Ahadi 10 za TANU:

1. Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja...............hapana, angalia dini kwanza.
2. Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote..... nitaitumikia familia yangu na washikaji zangu wote.
3. Nitajitolea nafsi yangu kuondoa umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma..........................kuondoa maadili yote ya taifa hili.
4. Rushwa ni adui wa haki. Sitapokea wala kutoa rushwa..............rushwa ni sehemu ya maisha, nitapokea na kutoa kila ninapopata nafasi.
5. Cheo ni dhamana. Sitakitumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu..............Cheo ni ulaji; watanikoma.
6. Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote.....................nitaiba vyeti na kugushi majina.
7. Nitashirikiana na wenzangu wote kuijenga nchi yetu................nitashirikiana na wageni kuibomoa nchi.
8. Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko......nitasema uongo, nitakuwa mfitini, nitapenda majungu, na nitakuwa mzushi.
9. Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa TANU na raia mwema wa Tanganyika na Afrika.....................nitakuwa mwanachama mwaminifu wa makundi ya mafisadi na raia mwizi.
10.                 Nitakuwa mtiifu na mwaminifu kwa Rais wa Serikali ya Tanganyika..............................nitakuwa mtiifu kwa wanaonihonga.

Maskini nchi yetu! Tuipiganie sasa! 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment