Saturday 6 April 2013

[wanabidii] Wakuu picha story ya GTI niliisahau, frm Thehabari.com

Wakuu picha za story ya GTI niliisahau kuambatanisha, frm Thehabari.com


Mbunge Mnyika Ahaidi Kumsomesha Mwanafunzi Bora Chuo cha Jinsia

Na Joachim Mushi

MBUNGE wa Jimbo la Ubungo kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John

Mnyika ameahidi kumsomesha mwanafunzi bora wa Chuo cha Jinsia (GTI) kupitia sehemu ya

mshahara wake wa ubunge.

Mbunge huyo alitoa ahadi hiyo jana jijini Dar es Salaam katika sherehe za Mahafali ya Kwanza

ya Chuo cha Jinsia, GTI alipokuwa mgeni rasmi. Alisema anatambua mchango wa chuo hicho katika

kuiandaa jamii kupigania usawa wa rasilimali za taifa, hivyo kupitia mshahara wake wa ubunge

atatoa mchango wa kumlipia ada mwanafunzi bora wa chuo hicho mwakani.

Mbunge huyo aliupongeza uongozi wa GTI kwa mafanikio waliofikia ya kuanzisha chuo kinachotoa

mafunzo ya jinsia kwa jamii na kushauri uongozi kujipanga na kuwasilisha ombi la kuomba fungu

la fedha kutoka Mfuko wa Mbunge wa Maendeleo wa Jimbo ili kukiwezesha chuo hicho kufanya

shughuli zake kiufanisi.

Awali akizungumza katika mahafali hayo, Mkuu wa Chuo cha GTI, Dk. Diana-Bupe Mwiru alisema

mahafali hayo ni ya kihistoria kutokana na kwamba yanafanyika kipindi ambacho Mtandao wa

Jinsia Tanzania (TGNP) ambao ni wamiliki wa chuo hicho wakisherehekea miaka 20 tangu

kuanzishwa kwa taasisi hiyo.

"TGNP inasherehekea miaka 20 ya harakati za ukombozi wa mwanamke kimapinduzi dai kuu likiwa

rasilimali za nchi kunufaisha watu wote na hasa wale walioko pembezoni. Mwanamke wa

kitanzania amekuwa miongoni mwa makundi yaliyoko pembezoni kutokana na mila na sheria

kandamizi ambazo zilishindwa kutambua mchango wa mwanamke katika jamii na majukumu makubwa

ambayo ameyabeba ili kuhakikisha kuwa jamii inaendelea kuwepo," alisema Dk. Mwiru.

Aliongeza kuwa GTI tangu kuanzishwa kwake imekuwa ikitoa mafunzo kwa umahiri mkubwa katika

soko la ndani na nchi za jirani, huku kikiwa kimefundisha washiriki zaidi ya 6000 kutoka nchi

za Msumbiji, Nigeria, Malawi, zambia, Kenya, rwanda, Uganda, Ethiopia, Norway pamoja na

Tanzania yenyewe.

"Kutokana na umahiri wake katika kutoa mafunzo GTI imeweza kutambuliwa kimataifa kama chuo

kilichotukuka katika kutoa maarifa na stadi katika nyanja ya jinsia na maendeleo kwa Afrika

Mashariki na Kati. Kwa GTI hii ni hatua ya mafanikio ambayo tuna kila sababu ya kujivunia,"

alisema Mkuu wa Chuo hicho.

Aidha Dk. Mwiru alitoa shukrani kwa mashirika mfadhili wa GTI ambayo ni 'Foundation for Civil

Society, UN Women, UNFPA, Deloitte, Action Aid na SIDA kupitia TGNP na RATN ambayo yamekuwa

sehemu ya mafanikio ya chuo hicho. Ikiwa ni pamoja na kuiomba Serikali pamoja na taasisi zake

nayo kuanza kukitumia chuo hicho.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya GTI, Profesa Saida

Othman aliiomba Serikali kushughulikia changamoto ya ubora wa elimu kiujumla kwani matokeo

yanavyokuwa mabaya hata vyuo vinavyotegemea wanafunzi hukosa wanafunzi wenye sifa kujiunga na

vyuo hivyo.

Jumla ya wahitimu wa 11 walifanikiwa kutunukiwa vyeti vya mafunzo ya jinsia katika mahafali hayo ya kwanza.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com.
_____________________________________________________
Joachim Mushi, Mhariri Mkuu wa gazeti tando la Thehabari.com
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066/ 0786 030066/ 0756 469470
Web:- www.thehabari.com  
          http://joemushi.blogspot.com

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment