Wednesday 3 April 2013

[wanabidii] Re: Vurugu Tunduma Baada ya DC kukataza Kuchinja

Taarifa kutoka Tunduma
mkoani Mbeya zinadai kuwa
hali si shwari katika eneo hilo
kutokana na kuzuka kwa vurugu kubwa zinazodaiwa
kusababishwa na masuala
ya kiimani ya nani achinje
kati ya mkristo na Muislam .

Mwandishi wetu kutoka
Tunduma mkoani Mbeya
anaripoti kuwa vurugu hizo
zimeanza majira ya saa nne
asubuhi kwa makundi ya
vijana kuandamana mitaani na kuvutana kuhusu uamuzi
wa viongozi wa dini ya
kikristo Tunduma kuandika
barua kwa mkuu wa wilaya
kutaka kuruhusiwa kuchinja
wakati wa pasaka.

Ripota wetu anaripoti kuwa
kabla ya ijumaa kuu viongozi
hao wa dini ya Kikristo
walikutana na mkuu wa
wilaya ya Momba Abuud
Saibea ambae aliwataka kuwasilisha barua rasmi ya
kutaka kibali cha kuchinja .

Hata hivyo inaelezwa kuwa
vurugu hizo za leo zina
mikanganyiko mingi kwani
wanaoshiriki katika vurugu
hizo ni vijana wapiga debe .....

Vurugu za uchinjaji
zilifanyika siku ya Pasaka na
hazikuwa na mvutano kwa
sababu wakristo walichinja
katika bucha zao na waislamu
nao walichinja katika mabucha yao ....

Cha kushangaza leo ni baada
ya kuibuka kundi la vijana
wanaofanya kazi katika stendi
na vijiwe mbali mbali ambao
ndio walioanzisha vurugu
kiasi cha polisi kuingilia kati kwa kutumia mabomu ya
machozi na kuwatawanya
wananchi waliokuwa
wamekusanyika maeneo mbali
mbali .


Kutokana na vurugu hizo
mpaka wa Tunduma ambao
unaingia nchi za kusini mwa
Tanzania ulifungwa pamoja
na magari yaliyokuwa
yakitoka Sumbawanga pia yalizuiwa kuendelea na safari
hadi hali hiyo ilipotulia mida
ya saa 8 mchana baada ya
kamanda wa polisi wa mkoa
wa Mbeya Diwani Athuman
kufika eneo hilo.

Source: Mpekuzi
http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/427824-ripoti-maalumu-kuhusu-vurugu-za-tunduma-zilizosababisha-mipaka-kufungwa-kwa-muda.html#post6051399

On Apr 3, 1:19 pm, Faiza Hassan <antiho...@gmail.com> wrote:
> Tupashe kwa ukamilifu kuchinja nini?
>
>
>
>
>
>
>
> On Wed, Apr 3, 2013 at 2:16 AM, Juma Mzuri <jumamz...@gmail.com> wrote:
> > Vurugu Kubwa zimetokea Tunduma baada ya Mkuu wa wilaya kukataza
> > wakristo kuchinja
>
> > --
> > Jobs in Africa -www.wejobs.blogspot.com
> > International Jobs -www.jobsunited.blogspot.com
>
> > Kujiondoa Tuma Email kwenda
> > wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
> > ukishatuma
>
> > Disclaimer:
> > Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> > consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> > presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
> > to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> > ---
> > You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> > "Wanabidii" group.
> > To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> > email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> > For more options, visithttps://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment