Sunday 21 April 2013

[wanabidii] Re: Mwanamuziki Diamond ni mdhalilishaji wa Mwanamke "Bi.Wema Sepetu"

Ukiangalia na kufuatilia kwa ukaribu ni kuwa WANAHARAKATI WANATETEA pale palipo na MASLAHI!!!!Kiwasila uko sawa.Ukiona eti watu wanjitolea kuzoa takataka,kusafisha mitaro,kutetea walemavu na mengine katika mgongo wa UHARAKATI ujue kuwa kuna HARUFU YA PESA hasa NGOs hizi Au RUSHWA.Hivyo,kwa upande kwa WEMA Sepetu kusema kadharirishwa,mie nadhani wafikie na wao waone kuwa inatosha.Ndiyo wanajidharirisha zaidi na zaidi.
Kiwasila naunga mkono hoja yako,na yote uliyosema ni kweli kabisa 100%.
KEEP IT UP waone kuwa Udharirishaji unaanzwa na wao,wengine wanapigilia mstari tu pale mtu anapojidharirisha.

On Sunday, April 21, 2013 9:35:01 AM UTC-5, Buberwa Jackob wrote:

             WANAWAKE WAUNGANA KUSUSIA BIDHAA NA MAONYESHO YA MWANAMUZIKI DIAMOND
                         Kwa Kumdhalilisha Bi.Wema Sepetu kwa kumrekodi katika simu na kusambaza mazungumzo nyeti !

Kitendo cha Mwanamuziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul Juma maarufu kama Diamond,cha kurekodi mazungumzo yake na star wa Bongo Move Bi.Wema Sepetu,
na kuyatuma mazungumzo yao ya mapenzi katika mitandao ni kitendo cha "Udhalilishaji wa Mwanamke" . kwa kuwa wanamuziki na wasanii wote wanatakiwa wawe ni mfamo na kioo cha jamii katika kielekeza jamii kuishi 
kwa kufuata na kuheshimu mahadili ,lakini mwanamuziki Diamond ameonekana kuwa ni  kiongozi wa "Udhalilishaji wa Mwanamke" kufuatia kitendo chake cha
kurekodi na kusambaza mazungumzo yao ya simu  ya kimapaenzi kati yake na
Bi.Wema Sepetu na mpenzi wake wa sasa Bi.Penny,kitendo hiki ni cha "kuwadhalilisha wanawake wa kitanzania" Tunaowaomba akinamama
na kinadada na wanawake wote kwa ujumla kususia kununua video,vcd,cd
pia kugomea kuhudhuria onyesho lolote lile litakalofanya na mwamuziki
Nasibu Abdul Juma aka Diamond hadi pale atakapo waomba radhi wanawake wote
wa kitanzania popote pale walipo.
Wanawake wote wanatakiwa kugomea maonyesho ya mwanamuziki huyo na
na kutonunua bidhaa za mwanamuziki huyo Diamond ili kukomesha kabisa tabia hizi chafu za "Udhalilishaji wa Mwanamke"



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment