Friday 19 April 2013

[wanabidii] Re: MAFUTA YA ZANZIBAR AU YA MUUNGANO?

Tatizo ni Choice of preferences(VIPAUMBELE)!Yaani wanaamua kuweka vipambele vitu ambavyo siyo vya msingi wala vya kujenga na kukosa kukazania vya maana.Mafuta kesho yataisha,mafuta kesho yanaleta maendeleo kwao peke yao na hapo kuzaliana(ongezeko la watu HILOOOO),Je,watakimbilia wapi?Wanakosa kuweka UNDUGU/UZALENDO pamoja yaani kushiriki chochote kilichomo kwenye ARDHI YA MUUNGANO haya kinachoonekana kuwa raslimali adimu.HUU UBINAFSI utawakosesha mengi.Tena vijana wanashabikia wazee wambao siku si nyingi wataachia ngazi.Vijana wanasahau wao ndiyo nchi ya kesho na wattoto wao na hao viongozi wa leo wanawatumia tu kwa mtaji wa umaarufu ili kuwaingiza WAKOLONI wa kiaarabu tena na kufaidi tu na familia zao!!!
Tuweni makini na UBINAFSI WA VIONGOZI wanaouza nchi kwa maneno matamu eti wanatetea uzanzibar kumbe wanauza nchi bila sie kujua.

On Thursday, April 18, 2013 10:27:12 AM UTC-5, Fakhi Karume wrote:
TUumeambiwa kuwa 'mafuta yametolewa katika orodha ya mambo ya
muungano'. Tumeambiwa hivyo katika mfululizo wa vikao vingi. Cha
mwisho kilikaa Zanzibar, beach resort, mara tu baada ya sherehe za
mapinduzi January 12-2013, chini ya uenyekiti wa Makamo wa Rais,
Dr.Bilali na huku Balozi Seif Ali Iddi.

Vilifuata vikao vya chama – CCM, pia viliridhia hilo. BLW, na Bunge
limeambiwa hivyo mara elfu kidogo. Hii imekuwa nyimbo ya wanasiasa wa
pande zote mbili – Tanganyika na Zanzibar.

Karibuni hivi, pinda aliliarifu Bunge kuwa 'mafuta yametolewa katika
orodha ya mambo ya Muungano'.

Msimamo wa Warioba na tume yake ya katiba ni kuwa 'suala hilo
litajadiliwa kama sehemu ya kutengeneza katika mpya'. halina haraka?

Jana, Mohammed Aboud, Waziri wa Nchi 9Zanzibar) Makamo wa PILI wa Rais
aliliarifu BLW kuwa 'bado majadiliano yanaendelea kuhusu suala hilo'
ama yawe ya Zanzibar au Muungano au…..vipi sijui. Yaani, suala hili
bado halijatolewa maamuzi, ndio maana yake.

Ndugu, wana-mzalendo — TUKAMATE WAPI???

Hapa ndio panaponiuma mimi kuwa tunachukuliwa Wazanzibari just for
granted, na just for ride. Na nyie wenzangu wengi mnakubali.

Hii ndio hali inayotukabili Zanzibar. Tumekosa muelekeo, tumekosa
mawazo mbadala, tumekosa uongozi na viongozi.

Tumegeuzwa kama mpira wa kona. Hatuna wabunge wala wawakailishi.
Ingalikuwa jana wawakilishi ni watu wenye akili timamu, na kumbukumbu,
wangaliweza kumbana Mohammed Aboud atupe ukweli wa mambo: which is
which???

Jamani nchi inateketea, inatutoka hiyo.

Nimeambiwa kuwa mara nyingi, ninatoa lawama, bila kushauri: nishauri
nini, nimshauri nani?

Msimamo wangu au imani yangu: Tanganyika hawakubali wala hawathubutu
kuyatoa mafuta katika ulingo wa muungano, na kama watayatoa, basi ni
'kimaandishi tu'; wao ndio signatories wa mikataba yote '….na
ushirikiana wa kimataifa….'

Tanganyika hawakubali aslan Abadan kuitoa Zanzibar au kuiwacha
Zanzibar altogether. Mfanye mnavyoweza, wala msijilinganishe na ex-
USSR au Yugoslavia au wapi na wapi sijui. Wale wana…………watanganyika na
sisi hatuna.

Sisi tusubiri, one day, tuimbishwe Aleluyah kanisani, na tutakwenda
kuimba na huku tumevaa misalaba. na Hatutokataa.

Tutabaki kucheza keram, na kupanga list wa wachezaji wa Asernal,
Manchester United, Liverpool, na Real Madrid.

Tutabaki kuhadith mipira kila asubuhi tu, na nchi inazidi kututoka.
Kigezo cha kuwa mstaarabu – ni kujua mpira na kuangalia mpira wa Man
United, na kumhadith Sir Alex Ferguson/na upumbavu kama huo. Mtoto wa
miaka saba, juzi ninamsikia anapanga list ya majina ya wachezaji
wataocheza usiku wake, na ilikuwa hivyo hivyo.

Na Abdi Salem

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment