Wednesday 17 April 2013

[wanabidii] Re: [Mabadiliko] Mazungumzo yangu na Kibanda kuhusu stori ya MTANZANIA

Jamani,
Wahariri na waandishi, poleni sana. Tunahitaji busara sana katika
mambo haya. Nchi yetu inayumba, na iwapo tasnia ya habari nayo
itayumba namna hii, basi hali itakuwa mbaya sana. Nilishawahi kusema
siku moja jukwaani kwamba watu wawe waangalifu na mhariri wa sasa wa
gazeti la Mtanzania, na nadhani atakuja kuleta kilio kikubwa zaidi.
Sina hakika kama anafahamu uzito wa maandishi anayoyaweka gazetini na
hii si mara ya kwanza. Pengine anahitaji kusaidiwa tu kama mtu mchanga
kwenye fani. Poleni sana mlioumizwa.
Matinyi.


On 4/17/13, Ansbert Ngurumo <ansbertn@yahoo.com> wrote:
> Mazungumzo yangu na Kibanda
>
> Baada ya stori ya gazeti la MTANZANIA leo, iliyotuhumu wahariri wanne na
> mwanasiasa mmoja kuhusu ushiriki kwenye mtandao hatari, nimefanya utafiti
> kujua kilichotokea, maana nimehusishwa na uchafu na ujinga usiofanana na
> haiba na hulka yangu.
>
> Nimezungumza na watu wengi kujua mwelekeo wa habari hii na hatua za
> kuchukua. Hatumaye, nimezungumza na Kibanda kwa simu mnamo saa 10 jioni.
>
> Bahati nzuri, naye alikuwa ameshazungumza na watu kadhaa, wakiwamo wahariri
> na viongozi wenzake wa New Habari. Kimsingi, amekerwa na kinachotokea
> kwenye vyombo vya habari kuhusu sakata la kutesana kwake.
>
> Kwa kifupi, anasema stori anayoiona yeye ni jinsi ambavyo Ludovick ameweza
> kujipenyeza na kuwazoea wahariri na wanablogu kwa sababu anazojua yeye.
>
> Anasema stori si kuwahusisha wahariri na ujambazi. Anasema hii ni njama ya
> kufunika mambo na kuwalinda wahalifu wa kweli. Akasema anadhani wametumia
> njama ya kugombanisha wahariri, ili kugawa vyombo vya habari katika makundi,
> waweze kutimiza malengo yao.
>
> Anasema Charles Mulinda amekuwa na hisia kwa muda mrefu kwamba Ansbert
> Ngurumo anamchukia. Mulinda, hata alipokwenda Afrika Kusini, alimwambia
> Kibanda kuwa Ansbert amekuwa anampigia Bashe simu, akimtaka amfukuze kazi.
> Anadai pia kwamba Ansbert ndiye alimshauri Msama amfukuze kazi katika gazeti
> la Dira. Anadai pia kwamba mwaka 2009 Ansbert aliporejea kutoka masomoni,
> alikuwa anadhamiria kumfukuza kazi, kwa madai kwamba yeye (Mulinda) ni mla
> rushwa.
>
> Mulinda anadai pia kwamba timu ya wahariri inayochunguza tukio la Kibanda
> ilipomhoji, miongoni mwa maswali aliyoulizwa ni kwamba inasemekana amekuwa
> akipokea rushwa kwa jina la Kibanda. Mulinda anadai kwamba mtu aliyewapa
> swali hilo ni Ansbert.
>
> Inasemekana pia kwamba Ratifa alimwambia Kibanda kuwa Ansbert amemwambia
> Bashe kuwa yeye (Ratifa) ni shushushu.
>
> Hivyo, watu hawa wawili walipopata taarifa za mawasiliano ya Ludovick na
> Ngurumo, wakaamua kumshughulikia. Kwa maneno ya Kibanda, Mulinda na Ratifa
> "wametumia moyo" badala ya kichwa.
>
> Lakini anasisitiza kwamba hata kama hayo yangekuwa kweli, haikuwa sahihi
> kuandika stori mbaya hivi dhidi ya wahariri. Anasema kwamba wao wamefanya
> hivyo kama kulipa kisasi, hasa kwa kuwa Tanzania Daima lilichapisha tamko la
> Marando likitaja majina na simu za watu, akiwamo Denis.
>
> KIBANDA amesikitika kwamba newsroom ya MTANZANIA imemwacha Mulinda kufanya
> atakavyo. "How can you have an editor who is an unguided missile?" alisema.
> Anasikitika kwamba yeye ambaye angeweza kudhibiti tabia hii ndiye ameumizwa,
> kwa hivyo hawezi kuchukua hatua.
>
> Amesema ana uhakika Ofisi itachukua hatua mwafaka.
>
> Tayari amezungumza na Bashe na kutaka Mulinda ahojiwe, ataje chanzo chake
> cha habari hiyo, ili hatua hiyo isaidie katika hatua zinazofuata, hasa kujua
> wanaofanya jitihada za kutumia media kuficha wahalifu.
>
> Amesema pia ni vema wahariri wakutane haraka iwezekanavyo na kuweka msimamo
> kabla ya mabaya zaidi kuwakuta.
>
> Tayari Jukwaa la Wahariri limeitisha Kikao cha dharura kesho, Dar es
> Salaam.
>
> UFAFANUZI WA BAADHI YA KAULI
>
> Nimemjibu Kibanda ifuatavyo:
>
> 1. Sijawahi kumfukuza kazi Mulinda. Nilimlea kazini akiwa correspondent
> (2006), baadaye Kibanda alipokuja akamwajiri na kumpa uhariri Tanzania
> Daima. Niliporejea kutoka masomoni, alijiondoa mwenyewe kwa woga, akidai
> kwamba nilikuwa nataka kumfukuza kazi kwa rushwa.
>
> 2. Sikuwahi kumwambia Msama amfukuze kazi. Msama mwenyewe ndiye alikuja
> Ofisini kwangu kuomba radhi kwa niaba ya Mulinda, kuhusu stori iliyokuwa
> imeandikwa kwenye gazeti la Dira kuhusu Free Media kuchelewesha mishahara,
> ikidai Mbowe ndiye amechota pesa na kuelekea Club Bilicanas. Msama alisema
> anashangaa stori hiyo kwani hata yeye alikuwa hajalipa mishahara, na Mulinda
> hajapokea wa kwake. Akasema Mulinda amekuwa anamgombanisha na watu
> anaofahamiana nao. Akaazimia kwenda kumfukuza kazi.
>
> 3. Ni kweli nilimweleza Bashe kwamba Mulinda ni mlarushwa, na haandiki stori
> kubwa bila kupewa pesa. Nilitilia shaka mwenendo wa stori zake kupotosha
> suala la Kibanda. Nikamshauri Bashe stori zao wasiwe wanamwachia Mulinda na
> Ratifa peke yao, bali wazijadili kwenye vikao, wakubaliane. Nilisema
> mkimwachia aamue peke yake atawaumiza nyie na watu wengine. Ndilo
> limetokea!
>
> 4. Kuhusu Ratifa, sikusema ni shushushu, bali ni msiri mno. Nikasema
> nimeshuhudia mara kadhaa akigombezwa na Kibanda kwa kumficha mhariri chanzo
> cha stori. Nikamshauri kwamba katika suala tete kama hili, ni vema waandishi
> wote wawe wanataja vyanzo vya habari kwa wahariri na wenzao katika Chumba
> cha Habari, ili kudhibiti dhuluma.
>
> 5. Nilisema chanzo cha habari yao hakikuwa na nia njema, na wao walitumia
> mawasiliano ya Ludovick kama kificho cha majangili ili kuwanusuru
> wanaotuhumiwa kushirikiana na Ludovick kwa mabaya.
>
> Wasiwasi wa wengi, akiwamo Kibanda, ni kwamba chanzo cha habari cha Mulinda
> kinaweza kuwa kinatumiwa na UWT au Polisi kuua stori HALISI. Ndiyo maana
> Kibanda amependekeza kwamba Mulinda ataje chanzo chake cha Habari.
>
>
>
>
> Ansbert Ngurumo
> Dar es Salaam
> Tanzania
>
> --
> Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
> Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda;
> mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
> Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
>
> TEMBELEA Facebook yetu:
> http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
>
> For more options, visit this group at:
> http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
>
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Mabadiliko Forums" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>
>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment