Monday 15 April 2013

[wanabidii] RAIS KIKWETE LEO AANZA ZIARA YA SIKU MBILI UHOLANZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Aprili 15, 2013, anaanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku mbili katika Ufalme wa Uholanzi kwa mwaliko wa Her Majesty Malkia Beatrix wa nchi hiyo.

Rais Kikwete akiambatana na Mama Salma Kikwete na ujumbe wake ameondoka nchini mchana wa jana, Jumapili, Aprili 14, kwenda Uholanzi tayari kwa ziara hiyo ambako pia ataandamana na Mawaziri wanne wa Serikali.

Mawaziri hao ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe, Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Dr. Abdallah Kigoda, Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa Maji, Ardhi, Nishati na Maendeleo ya Makazi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Ramadhan Shaaban.

Katika siku ya kwanza ya ziara yake leo, Rais Kikwete atafanya mazungumzo rasmi ya Kiserikali kati ya Tanzania na Uholanzi kwenye Makazi Rasmi ya Waziri Mkuu. Mazungumzo hayo rasmi yatakuwa kati ya Rais Kikwete na ujumbe wake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi Mheshimiwa Frans Timmermans.

Baada ya mazungumzo hayo rasmi, Rais Kikwete atakutana kwa mazungumzo na HRH Princes Maxima, Mke wa Mfalme Mtarajiwa wa Uholanzi, Prince of Orange Willem Alexander ambaye anatarajiwa kurithi kiti cha Ufalme kutoka kwa Mama yake, Malkia Beatrix, mwishoni mwa mwezi huu, Aprili 30, 2013.

Baadaye, Rais Kikwete na ujumbe wake atakutana na kufanya mazungumzo na Her Majesty Malkia Beatrix wa nchi hiyo ambaye anastaafu rasmi Aprili 30 mwaka huu kumwachia nafasi hiyo mwanawe, Prince Willem Alexander.

Miongoni mwa shughuli zake nyingine za leo, Rais Kikwete atakutana na uongozi wa Kampuni ya Rijk Zwaan Netherlands Limited, atakula chakula cha mchana cha kazi na wawakilishi wa Jumuiya ya Biashara ya Uholanzi na baadaye atakutana kwa mazungumzo na viongozi wa Chama cha Wenye Viwanda na waajiri wa nchi hiyo.

Kesho, Jumanne, Rais Kikwete atatembelea Bandari ya Rotterdam, moja ya bandari maarufu zaidi duniani, atakutana kwa mazungumzo ya faragha kati yake na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Mheshimiwa Mark Rutte ambaye pia watakula naye chakula cha mchana.

Mchana, Rais Kikwete atatembelea Kampuni maarufu ya mafuta duniani ya Shell na kukutana na jumuiya ya Watanzania wanaoishi Uholanzi.

Rais Kikwete na ujumbe wake anatarajiwa kurejea nchini Jumatano, Aprili 17, 2013.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

15 Aprili, 2013

Picture
Rais Kikwete akizungumza na uongozi wa Kampuni ya Utafiti na Uzalishaji mbegu bora za mazao ya mboga ya RIJK ZWAAN jana katika kitongoji cha De Lier nje kidogo ya jiji la The Hague.

Picture
Rais Kikwete akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo rasmi na ujumbe wa Serikali ya Uholanzi ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa nchi hiyo, Bwana Frans Timmermans jijini The Hague, Uholanzi.


Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2QbSF6u6V

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment