Wednesday 17 April 2013

[wanabidii] Ngoma Africa band yatoa Rambi Rambi kwa msiba wa Bi.Kidude

Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema PEPONI Bi.Kidude



Bendi ya maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" imepokea kwa udhuni na majonzi makubwa taarifa ya kifo cha mwanamuziki mkongwe barani afrika hayati Bibi.Fatuma binti Baraka (Bi.KIDUDE) mwenyezi amrehemu.

Ngoma Africa band inatoa mkono wa pole na rambi rambi kwa familia ya marehemu
Bi.Kidude,pia kwa sisi sote wanamuziki na wasanii  pamoja na watanzania wote kuondokewa na Mkongwe wetu Bi.Fatuma Binti Baraka (Bi.Kidude),ambaye alikuwa
ni balozi na hadhina ya utamaduni wa mwambao na waswahili, kitaifa na kimataifa.
Marehem Bi.Kidude hakuwa msanii au mwanamuziki tu bali alikuwa mpiganaji jemedari aliyeupigania na kuulinda utamaduni wa jadi ya kiswahili na mwambao.

Bendi ya Ngoma Africa inaungana na watanzania wote wa ndani na nje ya nchi
katika kuomboleza msiba huu wa mkongwe wa sanaa barani barani Afrika hayati
Bibi. Fatuma Binti Baraka (Bi.Kidude) .
Ngoma Africa band itasimamisha shuguli za kutumbuiza kwa mda wa siku 10
kwa ajili ya maombolezo ya msiba wa marehemu Bi.Kidude.
Mwenyezi mungu amlaze mahala pema peponi Bibi.Fatima binti Baraka (Bi.Kidude)

Amin.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment