Monday 15 April 2013

[wanabidii] NAOMBA NITAFAKARISHWE...JE,RUDO ALIKAMATWA KWA SABABU IPI?

Ndugu wanaBidii leo baada ya kusoma TAMKO LA CHADEMA nimepata maswali yafuatayo baada ya kutajwa Rudo kama T.S.S;
Je,alikamatwa ka sababu ipi?
1.Je,ni ile ya kutaarifu juu ya kutekwa kwake,na jinsi alivyoenda polisi na hospitali kumuona Ndugu Kibanda?
2.Je,alikamatwa kwa sababu ya kusikika jina Rudovick,na Rwakatale akashinikizwa kumtaja huyo Rudo aliyemtaja ni nani?

Mimi baada ya kusoma hilo tamko,basi nikaona kuna yafuatayo
1.Je,kama Rudo asingetajwa mle kwenye Video,ingekuwaje hadi sasa?
2.KAMA Rudo anahusika(Bado kujua,japo inakisiwa)basi angekuwa bado yuko mtaani na angekuwa mstari wa mbele kama wengine kulaani kuhusu kukamatwa kwa Rwakatale na angeongoza kuwa mtu wa maumivu zaidi ya hata mke wake na wanaCDM damu.
3.Kama Rudo ni T.S.S basi,kwa kusikika jina lake,basi ndiyo maana hata Polisi walichelewa kuhoji tamko la Mwigulu Nchemba,na kuja kuwakamata Rwakatale na Rudo baada ya habari kuonekana kwenye Youtube,vinginevyo....TUSINGEJUA HILI maana afisa wao tunayedhani(Rudo) alichemsha baada ya Nyota ya Rwakatale kumtaja kwa bahati mbaya.

Kama kweli Rudo alishiriki kwa 100%,basi tuzidi kuamini kuwa Mungu anawaabisha wale wanaowasumbua watenda na wanaotafuta haki kwa watu.
Mungu ibariki Tanzania.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment