Sunday 7 April 2013

[wanabidii] Mwaliko Kwenye Kongamano la Elimu tarehe 14 Aprili



UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
Academic Staff Assembly
 

MWALIKO KWENYE KONGAMANO LA ELIMU LA 14 APRILI  2013                                                                                                  
Kwa niaba ya uongozi wa Jumuiya ya Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na uongozi wa ITV na Radio One, napenda kuwakaribisha kwenye  Kongamano la Elimu litakalofanyika ndani ya ukumbi wa Nkrumah siku ya Jumapili tarehe 14/Aprili 2013. Kongamano hilo litaanza saa 9 alasiri hadi saa 12 jioni na kutangazwa  moja kwa moja na ITV na Radio One. Mada kuu ya Kongamano hilo ni, « Elimu yetu na Mustakabali wa Maendeleo ya Taifa kwa Miaka Ijayo ». Washiriki wawe wameketi kwenye viti kuanzia saa 8.30 mchana. 
 
Tunalenga kujadili kwa uwazi matatizo yanayoikabili sekta ya elimu nchini na kutafuta au kupendekeza mbinu za kuyatatua. Wajumbe wa tume ya Pinda nao watakuwepo siku hiyo kwaajili ya kupata mawazo ya wachangiaji ili waweze kuyajumuisha kwenye ripoti yao.  
 
Tumefanya maboresho ya uendeshaji wa kongamano hili kwa kurekebisha kasoro chache za ugawaji wa muda wa majadiliano kama zilivyojitokeza kwenye kongamano la Tarehe 9/12 /2012. Wazungumzaji wakuu wa kongamano hili watakuwa wawili tu, na muda utakaobaki utatumika kwa majadiliano. Pia tutatoa nafasi ya dakika za mwishoni kusoma maoni yatakayotumwa kwa njia ya barua pepe kwa wale watakaoshindwa kufika ukumbini.
 
Tunaomba kwa yeyote ambaye atapenda maoni yake yajumuishwe siku ya kongamano ayatume kwa njia ya barua pepe kwa anwani : kongamanoudasa@gmail.com. Pia yeyote mwenye picha ya shule au mazingira ya kuishi walimu, au wanafunzi au madarasa na picha hiyo inaonyesha jinsi hali ya elimu ilivyo, tunaomba atutumie kwa email hiyo ili tuweze kuitumia katika majadiliano kama ushahidi wa hali ilivyo katika nchi yetu.

Karibu sana ukumbini Nkrumah.
 
 
Mr. Faraja Kristomus (Katibu - UDASA)
Department of Foreign Languages and Linguistics
University of Dar es Salaam
P.O.Box 35040, Dar es Salaam
Tanzania
Mobile: +255 787 52 53 96 / +255 717 086 135

"All human beings are equal except our beliefs, tribes and thinking, which are always accidents and never the essences of our humanity. We acquire them after getting out of the wombs of our mothers".

0 comments:

Post a Comment