Thursday 18 April 2013

[wanabidii] MEMORANDUM OF UNDERSTANDING(MOU)

Ni kawaida kuwa kila taasisi iwe ya Serikali au isiyo ya kiserikali hata taasisi yoyote ile inakuwa na mikakati ya namna ya kufikisha huduma kwa watu!Taasisi husika ina kuwa na mipango ya muda mrefu na mfupi ili basi mipango na mikakati yao iweze kufanikiwa.Pia,ni wazi kuna taasisi ambazo malengo yao yanakuwa sawa ila jinsi ya kuifanikisha inatofautiana na hii ndiyo inaleta migongano katika kufanikiwa kwa taasisi moja na nyingine kushindwa kufanikisha mipango na mikakati waliyojiwekea.Sasa maswali hapa yakuja ,je ni sababu zipi zinasababisha taasisi zenye malengo na madhumuni sawa kutofautiana katika mafanikio ya kufikisha huduma?
Baada ya kuangalia na kwa kutumia uzoefu na common sense nikagundua haya na kweli ndivyo ilivyo;
1.Utamaduni wa taasisi(Organisation Culture)
Kwa vyovyote vile,utamaduni wa taasisi husika huwa na madhara katika kutoa huduma.Kama utamaduni wa taasisi husika hudhani mambo yote hutolewa kwa mazoea basi inaoonekana taasisi moja kuwa juu ya nyingine katika mafanikio basi taasisi inayoshindwa kutimiza malengo yao basi husukumia lawama taasisi inayofanikiwa.Hata kwa watu binafsi,mfano mtu anadhani unapata kazi na mshahara unadhani kuwa ndiyo mafanikio,ila mtu hana budi kufahamu kuwa kuna mipango na malengo.Hivyo mtu anayeona pesa ndicho chanzo cha mafanikio,basi mwenzake mwenye mshahara sawa anafanikiwa basi lawama zinaanza ohh ni mwizi,ohhh sijui nini...1
2.Elimu:
Kwa kawaida hakuna kazi za kitalaamu zinazoweza kufanywa kwa mazoea.Hata kutangaza imani ya dini ni taaluma tena inayohitaji ufahamu wa mambo mengi sana ili kuwawezesha watu kuwa karibu na huyu tunayemuamini kuwa ndiye KILA KITU.Kutangaza imani pia kunaweza kuonekana jambo rahisi tu maana tunaweza kudhani ni kufundishwa namna ya kwenda mbinguni tu ila tukasahau kuwa tunafundishwa namna ya kuishi hapa duniani.Hivyo,elimu iwe yoyote ile inahistaji INTERDISCIPLINARY MATERIALS.Ni elimu hii itasaidia mtu kuweza sasa kufanikisha malengo ya Taasisi husika na hapo ndipo maendeleo yanakuja.
3.Mwanzilishi wa Taasisi;
Kuna taasisi mbalimbali duniani,na zote lazima zinamwanzilishi nahuyo anakuwa na malengo kwa jamii husika,hivyo kila anayeiingia humo basi lazima accomply na malengo ya taasisi husika(Mission na Vision na Objectives) za taasisi husika.Kama hafuati,basi huyo hafai hata kidogo kuwa mmoja wapo wa kuleta huduma kwa kupitia taasisi hivyo.Mfano hata kama watu wanatofautiana imani ya dini,kama mwanzilishi wa Taaasisi hiyo alikuwa wa imani fulani,basi kama wewe si wa Imani husika unapaswa kufanya kazi kwa kufuata taasisi hiyo, na si wewe unavyopenda.Mfano;wewe ni mwalimu wa Geography unaomba kazi shule ya taasisi ya dini usiyo iamini basi njoo ufundishe Geography na ufuate utaratibu wao na wakati wa kufanya mambo yako fanya kwa kutoingilia kazi na malengo ya shule.

Hivyo basi baada ya kutoa ufafanuzi huo ngoja niweke dukuduku lengu hapa hasa kuhusiana na MEMORANDUM OF UNDERSTANDING(MOU)
Hili jambo sijui hata Serikali inalifahamu na kama inalifahamu basi ni kwa mazoea tu.Mambo haya yote hasa malalamiko kutoka kwa Waislamu baada ya Udh.Illungakuzunguka ncchi nzima analihubiri na kuchochea vurugu nadhani TUNGEKUWA TUMESIKIA SERIKALI IMELIZUNGIMZIA,ila hadi sasa nadhani hakuna aliyekuja hadaharnai nakulizungumzia.Je,tuseme hawalifahamu?
Nimesema maendeleo na mafanikio ya taasisi yoyote ile inategemea STRATEGIC PLANNING na kama hiyo hakuna usitegemee maendeleo ya taasisi husika.Na bila watalaamu wa mambo hayo,hata kama kuna malengo basi hayawezi kufikiwa.Kwanza kama hakuna uongozi wa kusimamia,kama haukna moyo wa kuyafanikisha,kama hakuna watu waliona moyo wa kujitoa kwa ajili ya taasisi husika basi UTEGEMEE muujiza au basi utegemee LAWAMA kwa wale wanaofanikiwa.

KUHUSU MOU;
MOU inafahamika ni maelewano ya serikali nataasisi za dini katika kuwafikishia watu huduma za elimu na afya.Katika hili Serikali inasaidia namna ya kuwezesha watu kupata huduma za afya, elimu na pia ajira kwa watu watakao fanya kazi kwenye taasisi hizo.Na si kwamba serikali inazipa pesa taasisi hizo,basi inawalipa watu mishahara ili kuboresha huduma kule zisipokuwa.Mfano ,je ni Wahudumu wa afya wangapi bila kujali itikadi za dini wanaoajiliwa na taasisi hizi na serikali inawalipa mishahara?Je,ni wanafunzi wngapi wanaosoma vyuo vikuu na wanapokea mikopo kutoka bodi ya mikopo na kufaulu na kupata kazi nzuri?Mbona haya mafanikio watu hawayazungumzii wanazidi kupandikiza chiki kuwa serikali inasaidia taasisi za dini moja?
SUALA SI UPENDELEO suala ni KULAUMU kwa kutofahamu namna ya kufanya.Mafanikio ya mwenzako si wizi,MUULIZE KAFIKAJE PALE.Mfano,katika taasisi mbali mbali za dini ya Kikristo kuna watalaamu wa kada mbali mbali,na kutokana na ORGANISATION CULTURE YAO basi kila anayeingia humo yupo COMMITTED TO DEATH kwa kutoa huduma kwa taasisi hiyo kwa uaminifu na kwa moyo wote.Taasisi hizo zina kila watalaamu,Walimu,Madaktari,Wahudumu wa afya,Meneja,watalaamu wa kila nyanja na haya yote hayako tofauti na malengo ya Taasisi.Mfano unakuta mtu ni Kiongozi wa dini Ila ni Mtaalaamu wa Uchumi na fedha,unakuta ni profesa wa Saikolojia,Mtalaamu wa mipango ya maendeleo,unakuta ni mtalaamu wa Banking,mtalaamu wa electronic na vitu mbalimbali.Usitegemee hata kama mna malengo na dira moja utakuwa sawa nayeye wewe ambaye unafahmu tu yale ya kumjua Mungu bila kuoanisha na maendeleo ya hapa duniani.Hivyo,lawana si kwa sababu ya SERIKALI KUTOA PESA KULIPA MISHAHARA NA MIKOPO kwa WaTanzania,bali ni WIVU wa KUONA MAFANIKIO YA WENGINE na kuyafanya yaonekane ni WIZI WA RASLIMALI ZA NCHI.Pia shida ni kukosa watalaamu wenye nia na moyo wa kujitoa kufanikisha malengo ya taasisi hisika.Lakini kikubwa zaidi ni KUKOSA WATALAAMU wa taasisi husika ambao wanafahamu mambo ya DUNIA na KUWEZA KUYAOANISHA na yale TUYADHANIAYO ya MBINGUNI.
Nimeeleza kuwa sababu ni moja kuwa malengo hayawezi kutimia hasa haya ya hapa duniani bila kupata wataalaamuwa kuyachambua na kujua namna ya kuyafanikisha.Je,tujiulize ni matajiri wangapi TZA wanamafanikio kwa kufanya FRANCHISING?Je, na wao ni wezi?Ni mipango tu.Tusilalamikie mafanikio ya mtu au taasisi tukadhani iko hivi hivi.Ukitaka mafanikio lazima uyasotee na ujue namna ya kuyalinda pia.
Hivyo nadhani kila kitu kina kuja kwa malengo na malengo hayatoshi bila nia na nia haitoshi bila utalaamu wa kuyafanya.
Nadhani kwa SUALA la MOU,ije ifkie mahala watu waelimishwa kwa nini MOU ipo na inafanya kazi namna gani.Na mwenye dhamana ya kulielezea hili ni SERIKALI na si mwingine awaye yoyote yule.

MOU  is the way to Carry out the MISSION,VISION AND OBJECTIVES of a WELL ORGANISED and CULTURED ORGANISATIONS.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment