Friday 12 April 2013

[wanabidii] MATOKEO YA TUME KUHUSU KUSHUKA KWA UFAULU HAYA HAPA!

Hii ndiyo ripoti kuhusu kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa mtihani wa kidato cha nne mwaka 2010 iliyotolewa na tume aliyounda Mh Pinder. Pamoja na kwamba matokeo yamezidi kuwa mabaya tangu mwaka huo, ripoti hii haikuwahi kutolewa hadharani wala kufanyiwa kazi! Inasikitisha na inauma sana kuona kwamba tume nyingine imeundwa mwaka huu kuhusu tatizo hilo hilo. What a waste of public money?
 
Sasa hii tume aliyounda mwaka huu inatafuta nini ikiwa sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu tayari zainafahamika lakini serikali imeshindwa kuzifanyia kazi? Je, ina maana kila mwaka tutakuwa tunaunda tume kutafuta sababu za matokeo mabaya? Mbona hao wajumbe wa tume wataneemeka sana? Matokeo yamekuwa yakishuka tangu mwaka 2010 hadi mwaka huu ambapo yamekuwa mabaya zaidi kumbe serikali inayo majawabu lakini imeyakalia? Viongozi wanataka kuipeleka wapi nchi hii? What a lunatic government? Jamani hii ni kitu gani hasa? Kwa nini pesa zetu zinachezewa kiasi hiki huku tumekaa kimya?
 
Kinachosikitisha ni kuwa baada ya ripoti hii kuwasilishwa, ilizuiliwa kabisa isiende public ati inaichafua serikali. Matokeo yake mwaka huu wamelazimika kufanya kilekile kilichofanyika awali lakini wakihitaji kupata ripoti wanazotaka ziseme kile walichotarajia kuambiwa. Fedha za walipa kodi zinatumika visivyo!

Hebu fungua hili faili muone ripoti yenyewe msijesema nimewauzia mbuzi kwenye gunia:
 

0 comments:

Post a Comment