Saturday 20 April 2013

[wanabidii] KWANINI UNATAKIWA KU UPDATE PROGRAMU ZA KOMPYUTA

Moja ya maswali ninayokutana nayo mara kwa mara ni kama ni muhimu
kuapdate program za kompyuta , wengi wanataka wanaponunua program kama
antivirus akishaweka tu basi asihangaike na chochote .

Programu ya kompyuta ni sawa na mwili wa binadamu unahitaji vyakula na
mahitaji mengine ili uendelee kuwa bora zaidi na kufanya kazi zaidi na
hata kuendelea kukua .

Kompyuta zetu tunazozitumia kwenye masuala mbalimbali zinakabiliwa na
changamoto nyingi na moja wapo ambayo ni kubwa zaidi ni hii ya kupata
updates zake kwa wakati husika na kwa gharama nafuu au bila gharama
kabisa .

Kompyuta nyingi huko majumbani , maofisini au vyuoni zina shida ya
kupata updates na matatizo yake mengi kama kuwa taratibu , kuingiliwa
na virus au kutokufanya kazi vizuri kunatokana na kutokupatiwa updates
kwa wakati unaofaa .

UPDATE NI NINI ?

Kwa lugha nyepesi update au kufanya update ni ile hali ya kuiongezea
programu Fulani katika kompyuta yako virutubisho ili iweze kupambana
na hali ya wakati huo na inayofuatia , hivi virutubisho vinaweza kuwa
ni programu ndogo ndogo au vitu vingine kwa ajili ya kuboresha
utendaji wa wa programu husika .

UPDATE INAFANYWAJE ?

Kama kompyuta yako imeunganishwa na mtandao yaani internet ina uwezo
wa kupokea update za moja kwa moja kutoka kwa watengenezaji wa
programu husika kama update hizo zipo .

Kama kompyuta hiyo haijaunganishwa moja kwa moja na mtandao unaweza
kuingia kwenye tovuti ya program husika na kutafuta updates kwa ajili
ya kuporesha programu hiyo .
Ukiingia kwenye hizo tovuti kuna sehemu ya Downloads hapo ndio unaweza
kupata updates ingawa sio zote ziko hivyo .

UPDATES HUTOKA MARA NGAPI ?

Inategemea na programu , kwa mfano program ya Microsoft windows 7
inakuwa na update nyingi zinazojulikana kama patch kwa ajili ya kuzima
baadhi ya matatizo kwenye program zake hizi zipo kwenye tovuti ya
Microsoft moja kwa moja na zinatoka mara kwa mara hizina msimu
maalum .

Kwa upande wa antivirus na yenyewe inategemeana lakini nyingi ni kila
siku lakini kwa bidhaa kama mcafee huwa zinatoka kila baada ya siku 3
au 4 na unaweza kubeba kwenye flash kwa ajili ya kuingiza kwenye
kompyuta ambazo haziko kwenye mtandao muda mwingi .

Program nyingine kubwa kubwa kama za kihandisi mfano AUTOCAD hizi
update zake au patches zake hutoka baada ya muda mrefu kidogo
kutegemea na lile toleo ambalo unalo kwa wakati huo .

MADHARA YA KUTOKUFANYA UPDATES KWA WAKATI

1 – Kama wewe ni mfanyakazi unaweza kuchelewesha kazi za watu kutokana
na utendaji mbovu wa program hiyo kutokana na kukosekana updates na
urahisi unaweza kupungua .

2 – Kama wewe ni mfanyakazi pia kompyuta yako inaweza kuwa mwanya wa
kupitisha virus na kusambaza kwa watu wengine ndani ya ofisi yako
kutokana na kuwa na antivirus ambayo haijaboreshwa kwa updates .

3 – kama ni mfanyabiashara unaweza kudownload program za ajabu na
zikafanikisha wizi wa taarifa zako kwa njia ya mtandao kwa sababu
antivirus ambayo unayo sio bora na haiendani na wakati huo haiwezi
kutambua baadhi ya viashiria .

USHAURI WA BURE

1 - Hakikisha unatumia leseni halisi za program kama ni antivirus au
program yoyote au kama program hiyo ni huria ( free ) hakikisha ni
kweli iko hivyo .

2 – Kama leseni za program zako ni halisi sio bandia basi hautoogopa
kuingia kwenye mtandao na kufanya updates za mara kwa mara ,achia
fursa hiyo ya kupatiwa updates za moja kwa moja .

3 – Usipende kutumia program ambazo huzijui au kama huna uhakika nayo
basi angalia kwenye mtandao review mbalimbali zinazohusu program
husika kabla ya kuamua kuingiza kwenye kompyuta yako .

4 – Ukinunua antivirus kesho hakikisha unafanya update zote za nyuma
mpaka siku hiyo kwa asilimia 100 ili kujihakikishia usalama zaidi .

5 – Kwa wale wa makazini hakikisheni mnatumia updates zinazoendana na
utaratibu wa ofisi yenu , kwa mfano unaweza ukawa unatumia office 2007
ukaona office 2010 imetoka ukataka kuweka tu wakati taratibu za ofisi
haziko hivyo hilo ni kosa labda kama ni kwa laptop yako nyumbani .

Kufanya updates za mara kwa mara hakukuhakikishii usalama wa asilimia
100 , vingine ni utumiaji mzuri wa program zako , usipende kutembelea
tovuti za ajabu ajabu na kama una mtoto mchunge , mlinde muelimishe
itamsaidia .

ZINGATIA .

Baadhi ya maofisi yana taratibu zake zinazohusu Matumizi ya Kompyuta
haswa linapokuja suala la updates , tafadhali fuata taratibu za kazini
kwako kama zipo .

Kama una maswali , maoni na ushauri Karibu kwenye mjadala .
YONA FARES MARO
0786 806028

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment