Friday 26 April 2013

[wanabidii] KUHUSU MKUTANO WA 26 WA DHARURA WA BARAZA LA MAWAZIRI LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MKUTANO WA 26 WA DHARURA WA BARAZA LA MAWAZIRI LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI


Mkutano wa 26 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki umekwisha leo jijini Arusha. Mkutano huo ambao ulianza kwa ngazi ya Wataalam tarehe 22-23 Aprili, 2013 na kufuatiwa na wa Makatibu Wakuu tarehe 24 Aprili, 2013 umepokea taarifa ya hatua zilizofikiwa katika majadiliano ya Itifaki ya Umoja wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo inatarajiwa kutiwa saini na Wakuu wa Nchi Wanachama katika Mkutano wao wa 15, mwezi Novemba, 2013.

Aidha, Mkutano ulijadili pia pendekezo la kuongeza wigo wa Mamlaka ya Mahakama ya Afrika Mashariki. 

Vilevile, Baraza la Mawaziri limepokea na kujadili mapendekezo ya bajeti ya Jumuiya kwa mwaka 2013/14 na limeridhia mapendekezo ya bajeti ya Jumuiya kwa mwaka 2013/14 kuwa Dola za Marekani 117,238,966.

Mkutano huu umejadili pia hatua iliyofikiwa katika uandaaji  wa   Itifaki ya  Hadhi na Kinga kwa watumishi wa Jumuiya na Taasisi zake.

Imetolewa na 

KATIBU MKUU
WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment