Thursday 25 April 2013

[wanabidii] Je? Umewahi Kutembelea Madampo yetu? je tupo salama? Pigia Kura Video hii ili tafiti itupatie majibu!


Salaam wanabidiij

Ninafanya tafiti kubaini viumbe /vimelea vya maradhi vinavopatikana au kuibuka  katika maeneo ya kutupa taka vinavyoweza kuleta madhara kwa afya ya binadamu, mazingira na wanyama. Natumia teknolojia ya kisasa ( Metagenomics) inayoweza kubaini vimelea vinavyoweza kukuzwa maabara na vile visivyoweza kukuzwa, ili kubaini mahusiano baiana yake na madhara yanayoweza kuletwa na vimelea hivyo kwa jamii.

Hii ni kutokana na ukweli kuwa; kwa sababu ya ongezeko la watu, makazi na shughuli za kiuchumi; utupaji wa taka hasa katika nchi za ulimwengu wa tatu (kama Tanzania) haukidhi viwango vinavyotakiwa, na hivyo kuacha maswali mengi yanayohitaji majibu dhidi ya mazingira ya dampo.

Nimeomba ufadhili katika taasisi ya Canada inayo fadhili tafiti zenye tija kwa jamii. kwa sasa wazo langu katika video hapa chini lipo katika mchakato wa kupigiwa kura ili kujua ni kwa kiasi gani jamii inaona haja ya tafiti hii.

Naomba KURA yako (LIKE) Chini ya video hii kwa kugonga LIKE, na pia uhakiki kama kura yako imesajiliwa( registered) ili tafiti iweze kufadiliwa na kufanyika kwa ufanisi




Natumaini wote tunajali mazingira yetu ili afya zetu ziwe bora,

Ahsante

Mwaikono, KS
Mobile phone: +255 762 85 66 16
website : www.nm-aist. ac.tz

---------------------

------------------------------------------------------------

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment