Friday 12 April 2013

[wanabidii] HAYA NDIYO MADARAJA MAPYA KIDATO CHA NNE?

Kuna taarifa kutoka kwenye mitandao ya kijamii kuwa serikali imeamua kuleta madaraja mapya, ili yaanze kutumika katika mtihani wa kumaliza kidato cha nne 2013. Madaraja yatakuwa kama hivi:
A = 80%-100%-
B = 65%-79%-
C = 50%-64%-
D = 35%-49%-
F = 0%-34%-

Madaraja ya awali yalikuwa hivi:
A = 81%-100%-
B = 61%-80%-
C = 41%-60%-
D = 21%-40%-
F = 0%-20%-

Maanake ni nini? Kila daraja litakuwa limenyanyuliwa kidogo, kwamba ili mwanafunzi apate daraja hilo itabidi apate alama nyingi zaidi kuliko ilivyo kuwa hapo awali. Alama 1 zaidi kwa A, alama 4 zaidi kwa B, alama 9 zaidi kwa C, na alama 14 zaidi kuipata D. 

F sasa itakuwa pana zaidi. Kuanzia alama 0 mpaka 34; kuliko ilivyokuwa inaishia alama 20, kwa utaratibu wa kawaida. 

Kwa bahati mbaya taarifa hiyo haina chanzo mahsusi cha kuaminika. Je taarifa hizi ni za kweli? na kama ni za kweli-mdau unazipokeaje?

Taarifa tumezipata kwenye kiunganishi hiki:
http://bit.ly/Yt903q

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment