Monday 22 April 2013

[wanabidii] Bi. Juliet Rugeiyamu-Kairuki ateuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TIC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bibi Juliet Rugeiyamu Kairuki kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC).

Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, 22 Aprili, 2013 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue, inasema kuwa uteuzi huo ulianza Aprili 12, mwaka huu, 2013.

Bibi Kairuki ni Mwanasheria mwenye Shahada ya Kwanza na ya Uzamili kwenye sheria. Ni mtaalam wa miradi ya ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi (Public Private Partnership). Kati ya mwaka 2002 na 2008 alikuwa Meneja wa Mradi wa Public Private Partnership Capacity Building in SADC, katika Chama cha Mabenki ya Afrika Kusini (The Banking Association South Africa). Kuanzia mwaka 2008 hadi sasa Bibi Kairuki ni Meneja Mkuu wa Idara ya Benki na Huduma za Fedha katika taasisi hiyo.

         "Mwisho"

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
DAR ES SALAAM.

22 Aprili, 2013

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment