Saturday 20 April 2013

[wanabidii] AISEE HUYU NI ABSALOM KIBANDA? IF SO, VERY ENCOURAGING


Nilivyosoma maandishi haya, nikalazimika kuangalia mara tatu tatu email iliyotumika/iliyotuma. Ni baada ya kusoma mara ya kwanza na kukuta ni email ya Absalom Kibanda

Inafanana kwa kiasi kikubwa na email yake nyingine ambayo nimekuwa nikiwasiliana nayo kwa kipindi kirefu sasa. Hasa kwa masuala yahusuyo kazi.

Katika ile thread inayohusu article (nzuri) ya Chief Mobhare Matinyi juu ya Magreth Thatcher, Ndugu Absalom, akiwa bado J'burg, ameaandika hivi;


"On Sat, Apr 20, 2013 at 9:36 AM, Absalom Kibanda <absakibanda@gmail.com> wrote:
I liked CNN commentator who described Thatcher as decisive and devisive. Im in J'burg where many people despised her for labelling ANC and PAC's anti apartheid fighters as terrorist organisations. Thatcherism was more or less barbarism. 

To her our freedom fighters, the Nyereres, Mandelas and the likes, where all terrorists!" 

Baada ya kusoma, tena na tena, nikakumbuka haraka haraka, vitu viwili. Kwanza baadhi ya maneno ambayo aliandika mtu mmoja, nafikiri ni Hoyce Temu pale alipomtembelea Absalom kule hospitalini. 

Sikumbuki maneno xactly, lakini in summary alikuwa akisema, referring to Kibanda, "He is still the same old Kibanda" she had just met two or so months before the former being assaulted and tortured.

La pili, nikakumbuka siku ile Chief Ndimara Tegambwage na Saed Kubenea wamevamiwa wakiwa kazini ofisi za Mwanahalisi. Wakati napewa taarifa, nilikuwa bafuni (nilikuwa chuoni bado), sijui kwa nini, lakini nilijikuta nikiuliza, "wameumizwa kichwani au ubongo umeathirika", nikaambiwa hadi sasa (then) inaonekana kuwa shambulio limemuathiri Saed Kubenea macho na Mzee Ndi ameumizwa kichwani.

Nikasema "basi ataaandika...Mungu amsaidie, lakini kama kweli wamemuumiza macho ma majeraha ya kawaida kichwani, bila kuathiri ubongo wake na kwamba bado unafanya kazi, Saed/ Ndi, ataendelea kuandika, kwa sababu anaweza kufikiri na kuwaza sawasawa, kutunza taarifa/kumbukumbu na kujua namna ya kuziwasilisha. Uandishi huanzia kichwani kabla ya kupitia mikononi na hatimaye kwenye kalamu.

Kweli hadi leo wote wawili, Ndi na Saed wanaandika. The same old...

Sitaki wala siwezi ku-undermine maumivu na madhara makali na makubwa ambayo Absalom ameyapata kwa muda wote tangu baada ya lile tukio baya kabisa, ambalo anasema alichungulia kifo. He passed through the valley of death. Lakini kwa kweli, kwa wengine tuliomuona pale hospitalini hadi Uwanja wa Ndege wa JNIA, kuweza kumsoma hapa akiwa ameandika a short piece but worthy reading, it is more than encouraging. 

Tuzidi kumuombea heri na afya njema katika wakati huu mgumu wa kujaribu kuzoea hali ambayo hakuzaliwa nayo na huenda kabisa hakuwahi kufikiria kuwa nayo, hadi atakaporejea nyumbani.

Ugua pole Absalom, but wishing u a quick recover brother. Thanx for sharing with us, once again, your opinion, after a long time.


Tumaini Makene
CHADEMA Senior Information(Press) Officer
0752 691569/ 0688 595831

Sent from my iPad

0 comments:

Post a Comment