Sunday 14 April 2013

Re: [wanabidii] Yaliyonikuta Jana Jumamosi....

Hk,

It was fantastic au waHaya wasemavyo "Fuantastic mbwenu"
Keep it up!
"The most uncivilized way of making friendship with an uncivilized folk ni jino kwa jino" hawataki matumizi staha ya kuelewana kwa ustaarabu, hivyo tumieni ushenzi kuwafanya waelewe na kuwa rafiki!
Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Vodacom Tanzania.

From: hkigwangalla@gmail.com
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sun, 14 Apr 2013 16:28:08 +0000
To: <wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Yaliyonikuta Jana Jumamosi....

Hahahahaaa! Ulifurahi nilivyowaambia ukweli eh? Kuna baadhi yao wamenipongeza wamesema ile si siasa ya chama serious cha siasa...nikashangaa, nikasema kumbe tunatakiwa kuwapa darasa tu hawa watu!
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

From: "Tony PT" <tony_uk45@yahoo.co.uk>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sun, 14 Apr 2013 16:24:52 +0000
To: <wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Yaliyonikuta Jana Jumamosi....

Hk

Juzi uliamua na ukafanya kweli! Mkiwa 4 hadi 5 humo mjengoni itasaidia kurudisha adabu za baadhi ya watu! Yote hayo wafanyayo ni maumivu mabaraza ya katiba...wameumizwa sana.
Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Vodacom Tanzania.

From: hkigwangalla@gmail.com
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sun, 14 Apr 2013 16:19:01 +0000
To: <wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Yaliyonikuta Jana Jumamosi....

Tony, nami pia naamini kuwa yataisha mapema, pengine asishtakiwe kwa lolote simply because alijipambanua mapema kutohusiana na kijana Ludovick, mara tu alipotuhumiwa kwa 'ugaidi'

Kuji-diassociate na mambo ya akina Ludo kutakuwa kulimsaidia kiasi fulani naamini
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

From: "Tony PT" <tony_uk45@yahoo.co.uk>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sun, 14 Apr 2013 15:47:40 +0000
To: <wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Yaliyonikuta Jana Jumamosi....

HK

Nimpe pole sana mimi pia. Lakini alikuwa muungwana sana kwa kuonyesha kutojihusisha kwake mara yalipotokea tu. Yatakwisha na wakosa watabainika tu kwenye vyombo husika.

Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Vodacom Tanzania.

From: hkigwangalla@gmail.com
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sun, 14 Apr 2013 15:36:12 +0000
To: <wanabidii@googlegroups.com>; mabadilikotanzania<mabadilikotanzania@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Yaliyonikuta Jana Jumamosi....

Mtani,

Pole sana. Yote haya maisha tu pia!

Regards,
HK.
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

From: Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sun, 14 Apr 2013 15:44:39 +0100
To: wanabidii<wanabidii@googlegroups.com>; mabadilikotanzania<mabadilikotanzania@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] Yaliyonikuta Jana Jumamosi....



Ndugu zangu,

Kwanza kabisa niwashukuru kwa dhati kabisa nyote mlionitumia salaam za kunifariji kwa njia za simu, email, facebook, majukwaa ya Mabadiliko, Wanabidii na JF.
Nimefarijika sana kutambua kuwa kuna wengi wenye kunifuatilia na kunijali.

Ndugu zangu,
Kama alivyowataarifu kaka yangu Nyaroonyo Kichehere, ni kuwa, jana Jumamosi nilikuwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kuanzia saa tano asubuhi ya jana mpaka saa tatu usiku. Ilihusu mahojiano ya Polisi na mimi kuhusiana na sakata la ndugu yetu Absalom Kibanda.

Ukweli sikukamatwa mahali popote, bali niliitwa na Kamishna ( Upelelezi) Advocate Nyombi. Alhamisi nikiwa Iringa, tukakubaliana na kiungwana na Kamishna Nyombi kuwa nifike Makao Makuu hayo ya polisi Jumamosi saa tano. Ikawa hivyo.

Hapo nilipokelewa na Kamishna Nyombi. Baada ya mazungumzo mafupi ndipo akawaita maofisa wengine watano wa Upepelezi kufanya mahojiano nami.
Niliomba niwe na Mwanasheria, nikakubaliwa.

Nilimpigia simu kaka yangu Nyaroonyo, naye, kwa vile ni Wakili pia wa Kibanda akanisaidia kuhakikisha napata wakili mwingine. Pamoja na kuwa ilikuwa ni Jumamosi, ndugu yangu Nyaroonyo Kichehere alifanya alivyoweza. Ndani ya dakika 40 hivi alifika chumba nr 704 ghorofa ya saba akiwa na Wakili Jacquiline Rweyongeza na Legal Officer Dickson Mbonde.

Nilimshukuru Kaka Nyaroonyo Kichehere. Na nilimuaga kwa kumwambia; " Nenda ukaifahamishe jamii juu ya hiki kilichonitokea".

Nachukua fursa hii pia kuwashukuru kwa dhati kabisa dada yangu Wakili Jacquiline Rweyongeza na kaka Dickson Mbonde kwa kuacha yote ya Jumamosi na kuwa tayari kuwa msaada kwangu. Jacquiline alimuacha nyumbani mtoto wake wa miezi minne kwa ajili ya suala langu. Sina namna nyingine ya kumshukuru. Na hakika, msaada wao niliuhitaji sana.

Nawashukuru pia kwa dhati kabisa, ndugu zangu Saed Kubenea, Mbaraka Islam na wengine wote waliokuwa na utayari wa kunisaidia pale msaada wao ulipohitajika.

Kwa ufupi, nimetoa maelezo yangu bila shuruti wala kutishwa. Na nimeweka wazi kuwa yanaweza kutumika Mahakamani kama yatahitajika au hata kama mimi nitahitajika, kwa namna yeyote ile.

Kesho saa mbili asubuhi nitaripoti Makao Makuu ya Polisi kupewa maelezo ya kitakachofuatia.

Kwa mara nyingine tena, nawashukuru sana kwa kuwa nami katika muda wote huu.

Maggid,

Dar es Salaam.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment