Sunday 14 April 2013

Re: [wanabidii] Yaliyonikuta Jana Jumamosi....

Nami nikupe pole ndugu yangu. Hebu hesabu hili nalo kama sehemu moja ya mapito katika maisha ya mwanadamu. Hivi ndivyo historia ya mtu inavyotengenezwa na matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na mengine kama haya.

Sent from Yahoo! Mail on Android

From: Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>;
To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>; mabadilikotanzania <mabadilikotanzania@googlegroups.com>;
Subject: [wanabidii] Yaliyonikuta Jana Jumamosi....
Sent: Sun, Apr 14, 2013 2:44:39 PM

Ndugu zangu,

Kwanza kabisa niwashukuru kwa dhati kabisa nyote mlionitumia salaam za kunifariji kwa njia za simu, email, facebook, majukwaa ya Mabadiliko, Wanabidii na JF.
Nimefarijika sana kutambua kuwa kuna wengi wenye kunifuatilia na kunijali.

Ndugu zangu,
Kama alivyowataarifu kaka yangu Nyaroonyo Kichehere, ni kuwa, jana Jumamosi nilikuwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kuanzia saa tano asubuhi ya jana mpaka saa tatu usiku. Ilihusu mahojiano ya Polisi na mimi kuhusiana na sakata la ndugu yetu Absalom Kibanda.

Ukweli sikukamatwa mahali popote, bali niliitwa na Kamishna ( Upelelezi) Advocate Nyombi. Alhamisi nikiwa Iringa, tukakubaliana na kiungwana na Kamishna Nyombi kuwa nifike Makao Makuu hayo ya polisi Jumamosi saa tano. Ikawa hivyo.

Hapo nilipokelewa na Kamishna Nyombi. Baada ya mazungumzo mafupi ndipo akawaita maofisa wengine watano wa Upepelezi kufanya mahojiano nami.
Niliomba niwe na Mwanasheria, nikakubaliwa.

Nilimpigia simu kaka yangu Nyaroonyo, naye, kwa vile ni Wakili pia wa Kibanda akanisaidia kuhakikisha napata wakili mwingine. Pamoja na kuwa ilikuwa ni Jumamosi, ndugu yangu Nyaroonyo Kichehere alifanya alivyoweza. Ndani ya dakika 40 hivi alifika chumba nr 704 ghorofa ya saba akiwa na Wakili Jacquiline Rweyongeza na Legal Officer Dickson Mbonde.

Nilimshukuru Kaka Nyaroonyo Kichehere. Na nilimuaga kwa kumwambia; " Nenda ukaifahamishe jamii juu ya hiki kilichonitokea".

Nachukua fursa hii pia kuwashukuru kwa dhati kabisa dada yangu Wakili Jacquiline Rweyongeza na kaka Dickson Mbonde kwa kuacha yote ya Jumamosi na kuwa tayari kuwa msaada kwangu. Jacquiline alimuacha nyumbani mtoto wake wa miezi minne kwa ajili ya suala langu. Sina namna nyingine ya kumshukuru. Na hakika, msaada wao niliuhitaji sana.

Nawashukuru pia kwa dhati kabisa, ndugu zangu Saed Kubenea, Mbaraka Islam na wengine wote waliokuwa na utayari wa kunisaidia pale msaada wao ulipohitajika.

Kwa ufupi, nimetoa maelezo yangu bila shuruti wala kutishwa. Na nimeweka wazi kuwa yanaweza kutumika Mahakamani kama yatahitajika au hata kama mimi nitahitajika, kwa namna yeyote ile.

Kesho saa mbili asubuhi nitaripoti Makao Makuu ya Polisi kupewa maelezo ya kitakachofuatia.

Kwa mara nyingine tena, nawashukuru sana kwa kuwa nami katika muda wote huu.

Maggid,

Dar es Salaam.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment