Tumeiona suala hii ktk TV kama lile la mwendesha gari mmoja kumkunja askari wa usalama barabarani. Mkuu wa Mkoa hakuongea kibaya ktk suala hili kama TV ilivyoonyesha. Ila inajulikana sana kuwa vyuo vya juu wanafunzi waliowengi ni Chadema. Huu ni ukweli tunaouona ktk vyombo vya habari na matukio kitaifa. Usishangae kuona Mkuu wa Mkoa au wilaya au kiongozi wa CCM kuzomewa na wa Chadema hata akipita tu barabarani kupugiwa makofi na wanafunzi. Wakati mwingine ni vema kufahamu pia-kwa nini mwanafunzi kachomwa kisu? Alikuwa wapi na anafanya nini hata akachomwa kisu? Jee, amefumaniwa na mke au mtoto wa mtu? Amejihusisha na ujambazi? Wapo mpaka wanafunzi wa shule za msingi au sekondari wanaokamatwa wakijihusisha na ujambazi. Wapo vyuo vya juu wanaoshirikiana na vibaka nje kuwapa funguo au kuwaelekeza chumba cha kuiba na kitu chenyewe-laptop, simu za bei etc. Kuna mabweni mengine katika vyuo wanakamata kibaka akiimba jengo au bweni fulani na kumpiga mawe kuja kugundua ni student. Wao wanapoua inakuwaje? wanajipeleka kuvungwa? si inakuwa-wanafunzi wenye hasira nguvu ya umma imeua? Mbona matukio haya yapo na hawaandamani kama wanavyofanya akipigwa na kuuawa na non-students au wananchi? unasikia tu mwizi kauawa mabibo etc!! Kwani protocol inasemaje? Chuo kipo chini ya jirani wengi wa vyama na mashirika mbali mbali. Nani anahusika na chuo kukiwa na vurugu-ni mwana siasa yoyote yule aliyejirani? Kama ni hivyo basi, nyumbani kwako jirani yoyote aingine kuja kutatua matatizo wanao wanapogombana daily unapokuwa mbali au haupo-itakula kwako. Utawala na usimamizi utakushinda. Vyuo kuishi kiusalama na upendo na majirani wao wazungukao vyuo ni vema kwani ktk mahusiano mabaya ya chuki na kujidai-wanafunzi wanaweza kuviziwa na vijana waovu vuta bangi wa eneo hilo wakawapora, kuwapiga, kuwadhalilisha kwa kuwabaka both gender na uovu mwingine. Nao jirani hutegemea wanafunzi hao kwa kipato maana wanafunzi hununua bidhaa zao na huduma watoazo (kusuka, kuuza vyakula, vinywaji bar; kuchapa na kutoa photocopy etc). Tunategemeana na vyuo kwa sasa vina mashirika ya ulinzi walindao maeneo ya vyuo na pia mashirika ya kufanya usafi. --- On Wed, 24/4/13, Emma Kaaya <emmakaaya@gmail.com> wrote:
|
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment