Tuesday 9 April 2013

Re: [wanabidii] URAIS 2015 - ZITTO KABWE NDIO CHAGUO SAHIHI KWA CHADEMA

Abdalla Khamis,
REF hoja ya 1:Tukubali au tukatae CHADEMA hatukubaliki maeneo yenye waislamu wengi kama mikoa ya Pwani naTabora kwa sababu ya dhana hii ya udini. Iwapo Zitto Z Kabwe atasimama basi lazima hata wale waliokuwa hawataki kutuchagua kwa sababu ya udini basi kura zao tutakua nazo.

Abdala Khamis inaonyesha wewe ni mdini sana. Kwanini unataka kuwalazimisha watanzania wachague Rais kwa kutumia kete ya UDINI??. Hujaona tu hatari ya kuingiza dini kwenye siasa?? Kumbuka CCM wamefanya hivyo kwenye ilani zao kwa kuwaahidi waislam mahakama ya kadhi jambo ambalo ndio limechangia mtafaruko wa udini. Pamoja na hii kazia ya udini ni ajabu unataka pia CHADEMA watumie  hiyo kete.

Abdala Rais tunaemtaka anatakiwa asiwe mdini wala asifikiri kua dini fulani ndio ime-play kumwingiza madarakani. Kwa maneno mengine hatutaki Rais ambae anafungamana na dini yoyote-urais wa ubia. Inapokuja kwenye kutoa mamuzi ni ngumu sana abdala.

Je! Abdala unaamini kua Tanzania tukianza kuchaguana kwa udini mwislamu atakuja kupata Urais kwenye nchi hii?? Au kwa maneno mengine unafikiri kua Waislamu ni wengi kuliko wakristo TZ kama watu wengine wanvyotaka kuwaaminisha watu??

REF: Zitto hana kashfa yoyote ile ndani ya chama na nje ya chama. Zitto amejiweka safi katika kashfa hizi ukiondoa propaganda chache zisizo na macho.
Abdalla una uhakika na hili?? Zitto wenzake wanamtuhumu kua alikisaliti chama kwenye uchaguzi wa 2010 kwa kumpigia kampeni mgombea wa Rais? Hii huoni ni kashifa kubwa?? Magazeti yamesema alikua na mawasiliano na watu wa usalama wa taifa ambao CHADEMA wanasema wanahujumiwa nao. Unasemaje juu ya hilo??.

Kimsingi Zitto kama mtanzania yoyote anahaki ya kugombea na kuchukua madaraka yoyote nchini kama sheria itamruhusu na chama chake kikamukubalia. Ila usianze kumchafua zitto kwa kete ya kua atapata Urais kwa kua ni mwislamu. Sizani hata Zitto atakubali kua aingoze hii nchi kwa kua ni mwislamu.

Abdalla usiupandikize umma udini hasa kwenye suala mhimu kama Urais.
Alexander



From: ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Tuesday, April 9, 2013 4:26 PM
Subject: Re: [wanabidii] URAIS 2015 - ZITTO KABWE NDIO CHAGUO SAHIHI KWA CHADEMA

Ama kwa kukusudia ama bila kukusudia bila shaka kwa kuishi mbali na mawazo ya watu point yako namba moja imemmaliza badala ya kumjenda. Umekosea sana Abdalah

--- On Tue, 4/9/13, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:

From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
Subject: [wanabidii] URAIS 2015 - ZITTO KABWE NDIO CHAGUO SAHIHI KWA CHADEMA
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Tuesday, April 9, 2013, 6:59 AM

Kwanza poleni na kazi za hapa na pale katika pilikapilika za kutafuta na kuendesha maisha.

Mimi ni mwanachama halali wa CHADEMA mwenye kadi namba 0333673 ya uana chama. Ningependa kuwashirikisha jambo lifuatalo.

ZITTO Z KABWE NDIO CHAGUO SAHIHI KUWA MGOMBEA URAISI KWA CHAMA NA WATANZANIA MWAKA 2015.

Ndugu zangu, viongozi wa chama na wanachama! Kama kweli tuna taka kuchukua nchi hii basi Zitto Z Kabwe ndio chaguo sahihi kwa nafasi ya uraisi kwa chama chetu. Nina sababu chache zifuatazo.

1. Tukubali au tukatae CHADEMA hatukubaliki maeneo yenye waislamu wengi kama mikoa ya Pwani naTabora kwa sababu ya dhana hii ya udini. Iwapo Zitto Z Kabwe atasimama basi lazima hata wale waliokuwa hawataki kutuchagua kwa sababu ya udini basi kura zao tutakua nazo.

2. CCM wanatumia dhana ya ukanda. Iwapo Zitto atasimama basi hawatakua na ajenda yoyote katika kampeni zao dhidi ya hoja hiyo. Hakika huo ndo utakua mwisho wao.

3. Zitto ni kielelezo cha democrasia bungeni na mtaani. Ni Kijana aliye ibuo hoja nyingi sana nzito na ni kijana aliyeamsha vijana wengi sana usingizini. Zitto hajachoka kuwatetea vijana pamoja na kejeli zote anazozipata.

4. Zitto ni kijana na anamvuto kwa vijana wengi sana . Vijana sasa wamechoka sana na wangependa kupata mkombozi wa kweli. Zitto is a right guy in this. Zitto atavuta hata vijana wasio penda kupiga kura na wao washiriki kuongeza ushindi.

5. Zitto hana kashfa yoyote ile ndani ya chama na nje ya chama. Zitto amejiweka safi katika kashfa hizi ukiondoa propaganda chache zisizo na macho. 

6. Zitto ameishi umaskini. Anajua nini adha ya kuwa na shida na anajua uchungu wa kuwa maskini. kwani ametoka katika familia maskini sana na mkoa maskini sana. Kwa ufupi ana uchu wa maendeleo.

7.Zitto sio mdini kama viongozi wengine wa kiislamu walivyo. Zitto hajawahi kujiingiza katika mgogoro wowote wa udini na hana mpango huo kwani kwa mtazamo wangu yeye ni public figure.

Mwisho, najua wengi tungependa Dr Slaa agombee tena urais. Lakini amini nawambieni kama kweli nchi hii tunaitaka basi Dr. Slaa sio chaguo la ushindi. Kwani hana vigezo vingi ambavyo zitto anavyo.

Pia najua Zitto kasema hataongelea tena urais lakini hakusema sisi wanachama tusiongele huo urais. Ningependa sana Dr. agombee lakini mwisho wa siku hatuta shinda kwa mgawanyo wa kura.

Mimi sio mfuasi wa Zitto. Mimi ni mfuasi wa CHADEMA na mpenda mabadiliko. Naongea kitu halisi, kama mtaona nimeandika vyema asante lakini kama mtaona nimeandika vibaya, subilini mwaka mmoja na nusu uliosalia halafu muone yatakayotokea.

JJB,UDSM

http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/430993-barua-ya-wazi-kwawana-chadema.html
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 


0 comments:

Post a Comment