Tanzania inahitaji kiongozi kama mkali kama Thatcher ili watu tujitume tufanyekazi kwa ajili ya maendeleo yetu binafsi na ya nchi. Awe mkali lakini ana utu. Itafika wakati pia kama utu haufai-uwaache wafe mfano wanapokataa kuhama mabondeni na maeneo hatarishi na ardhi au pakwenda wanako. wanapoingia kinyemela kiwizi kuchimba maeneo hatarishi na wakafukiwa daima kurudia kufanya hivyo. Ukiwaacha labda baadhi yao watajifunza kwa kuwawekea bango na matangazo kuwa ukiingia huku na kufukiwa serikali haitohusika au nukiendelea kuishi hapa eneo hatarishi tutabomoa na hakuna kesi kwenda mahakamani. Kuna maeneo kame nchini lakini yapo maeneo mengi kuna kila kiltu ila watu wamebweteka. Hata maeneo kame yana mabonde chepechepe ambapo nyanya zinaweza kulimwa, zabibu na karanga kwa kuzingatia ushauri. Kuna maeneo maji na miti, nyasi, makuti yapo ila mtu ana nyumba unamchungulia nje unamuona kwani ukuta upo wazi. Hana hata kuogopa kuwa nyonga na wadudu wengine wanaweza kumuingilia kutwa yupo barazani mabonde na msitu mnene umemzunguka. Maeneo kama Mkuranga, Rufiji huelewi kuwaje mtu aishi kimasikini hivyo. Isipokuwa maneno mengi, ufisadi, uvivu, lawama badala ya kujituma kwa bidii. Uharibifu wa mazingira, kutokujali uhai wetu tunachafua mpaka maji tunayotegemea kwa matumizi yote. Wachafu-unakataa kuchangia shs 500 kwa wiki elfu moja kwa mwezi unatupa takataka katika reinforced stormwater drainage system matokeo yake maji yanakwama hayaendi, kichesi kinajaa ndani ya nyumba yako, unaogelea chako na cha wenzako. Unajenga mabondeni mijini na na vijijini katibu na mto na ziwa au mapito ya mto wa zamani uliokauka kisha mafuriko yanakuzoa-gharama kwako na familia na kwa nchi. Kila mtu anakimbilia mjini-pikipiki, bajaji, kuuza vitumbua. Kijijini huko ndio kunakotoka ndio kunatoka viazi vitamu, mbaazi, nazi kwa wingi, vitunguu, nyanya, mihogo. Maeneo ya kuweka biashara yapo lakini kila mtu anapanga barabarani kiasi kwamba wapita kwa miguu wanakosa njia. Sehemu ya kupita kwa miguu mtaani ndio umepanga viti vya biashara ya bar kuuza bia na mama ntilie hapo na huku pikipiki na bajaji zinapita hapo balaa la kupisha viti, bajaji na watembea kwa miguu-chaos. Ukiondolewa na kiongozi wa serikali wa mitaa-unamvamia vichochoroni kumbonda. Wakija polisi-mnajiunga mnapambana nao eti mnaganga njaa hamuwezi kuondoka. Kuganga njaa ndio sababu kuu ya kuvunja sheria za makazi na ujenzi na za biashara ambazo kwa vyakula vumbi na mainzi tele yamejaa. Maeneo wazi ya kucheza watoto na yale ya shule-gereji na kazi za welding zimejaza nafasi vumbi la chuma na mbao linasumbua na kudhuru afya za watu lakini unaweka deaf ear. Akija mchina, Mkorea kuchukua ardhi kuwekeza hapo kijijini wewe unayesema jembe la mkono halifai kulimia ndio unayepanga foleni ya kulima kibarua kutwa. Ila ukiipoata hiyo hela-pombeni kilabuni sio kununua angalau kilo ya mbegu nawe ulime shamba la babu upande hayo mahindi kumuiga huyo mchina. Nawe umechaguliwa kuwasaidia hao jimboni kwako-upo kuhamasisha maandamano mjini yanayoishia wananchi kuporwa na kuharibiwa mali. Haupo kuhamasisha maandamano kuelekea shambani ktk kilimo endelevu na kuondoa wanaokata miti kuuza mkaa au kuuuchimba mto, mlima ambao utawaporomokea mvua ikija wakitafuta dhahabu ambayo wakiipata haionyeshi maisha yao kubadilika, kuandamana kuwaondoa wanaochimba maeneo hatarishi lakini unawatembelea kujionyesha unawajali. Wanapofukiwa na kuzikwa ardhini maeneo hayo hatarishi-huna vifaa vya kuwatoa ni gharama kwa taifa na uchafuzi wafanyao unaongeza vizazi vya vilema nchini kwao na watoto wazaao. Wanalima kwa trekta na plau ndani ya wildlife conservation area na kukaribisha wageni kuhamia kujenga, twaona wengine na mifugo tele na kukata miti ya misitu yetu. Lakini, daima tunaona upande mmoja tu mfano katika wildlige conservation areas ya authorised hunting na live animal capture paid for na hela zinaingia halmashauri na vijijini ambapo hao wa vijiji wamezifisadi. Huoni ujangili na maafa ya wildlife na encroachment ya ardhi iliopo ifanywayo na watu wako bali unamuona mwindaji tu ndio mwizi lakini uharibifu wa matumizi sio endelevu mengine huoni. Wakati ule ule ulijipa priority katika mafao/benefits zitokazo na uwindaji ukachagua watoto wako wewe wa kwanza wakaenda kusomeshwa. Unaona majengo ghorofa yanajengwa urefu wa juu mkubwa na nchi haina vifaa vitakiwavyo vya zima moto, yanajengwa maeneo yasiyotakiwa; unaona maeneo ya viwanda yanajengwa colleges, nyumba za makazi-unaangalia. kiwanda kiliripuka moto na mchanganyo huo wa makazi ya watu utawaokoaje na vifaa hakuna? Kwa nini unamwachia mwenye plot ya kiwanda ajenge shule ya vidudu, msingi, college humkatazi? Unaona bali ukipofu-Unahitaji Kiongozi Dictator kama Thatcher akupelekeshe ili uzingatie TOR za kazi yako na misingi mema ya maisha yako mwenyewe ili usidhurike. Bila ya viongozi madikteta 'Africa in General' haitoendelea. Tutabakia tu ktk vita kuwa leo ni MC4, kesho inaanza MC4 kuuana, kubaka vizee na vichanga Unajua dawa hii ni sumu ya panya-unayeyusha kiasi kuvulia samaki kisha unachukua dawa ya kuhifadhi maiti isioze unatia maji na kuhifadhia samaki zisioze na kuuzia wenzako.Unachakachua dawa ya Ukimwi au ya kuua mbu unauzia watu wa taifa lako. unachakachua tomato unaweka unga wa rangi wa harudu fulani ndio tomato ya kulia chips. Hapo unaongeza vilema, matatizo ya figo na ya kifafa kwa jamii-hujali mtanzania hata uelimishwe vipi upo kuchakachua dawa na vyakula. Ukaguzi ukipita-unafunda duka masiku ili visichukuliwe kuchomwa moto-kuteketezwa. Jee, tutafika bila ya kutumia nguvu maana elimu jamii na elimu ya umma haionyeshi kufanikiwa? Punda haendi mpaka kwa nyenzo. Miaka mingi nchi za Afrika tumejitawala lakini inaonekana daima tunarudi nyuma hatuendi mbele katima masuala mengi. Fikiria baba kabaka kitoto chake cha miaka 6 halafu kapewa kifungo cha maisha mama wa mtoto (Mke) anasema mumewe asamehewe au ndugu wanamtorosha mbakaji huyo na kumficha au kumtolea dhamana anatoroka-kamata na funga aliyotoa dhamana. usiache kesi ikaishia hivi hivi ili huu mchezo wa ubakaji uishe. Zamani watu kama hawa wabakao mpaka vitoto, vizee waliuawa na jamii ilijua. Hii demokrasia ndio inawapa vichwa. Mtu kama Thatcher-anatufaa. --- On Sat, 20/4/13, Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com> wrote:
|
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment