Thursday 4 April 2013

Re: [wanabidii] TAMKO LA NGOS KUHUSU MGOGORO WA ARDHI WA LOLIONDO


Kijana chunga lugha yako au tutakung'oa kucha na meno!!

Lakini ukisoma magazeti utaona wanatangaza uvunaji wanyama eneo fulani ambapo wanaonyesha na bei yake. kama wewe mwindaji una lesseni na bundiki yenye leseni au kuandikishwa miliki yake-unakwenda kuua mbogo, swala, ngiri, nguruwe mwitu etc baada ya kulilpia bei ya mnyama. Kila mnyama ana hesabu yake-bei na idadi yake ya kupunguzwa kwa mwaka. wapo pia wawindaji haramu wanauza nyama daily. utaona gari kando ya mbuga ya hifadhi  (N.Park, Game Reserve, Game Conservation Area) mbovu imeharibika na tairi zimetolewa jamaa wanajifanya wanatengeneza. Kumbe wanasubiri ishara, wafunge tairi, jamaa walete na kupakia mzigo kukiwa shwari waondoke. bado hao wawindaji wasio kibali (haram) ambao hutimia mikuki, mishale ya sumu na mashimo ya kuchimba msituni ndani wakaweka mtego fyatuka na mnje wakaweka nyasi kama vile hakuna shimo. kama umepotea njia-please usipite hovyo porini mpakani na vijiji vilivyozunguka hifadhi-itakula kwako. Ukitumbukia ndani ya mashimo hayo, mtego utafyatuka unakunasa na kukukua. Mashimo ni mbinu ya uwindaji haramu. daima sindikizwa na wanavijiji ktk tembea na tafiti zako za Transect walk watakuambia-huko usipite-kubaya. wanyama wawindwao na sisi kiwizi bila leseni ni wengi sana sana kwa idadi. Kama kuna watu ambao hawawezi kulala kupata usingizi bila ya kula nyama pori-Wavidunda, Wasagala ni wamojawapo. Wengine kama Waikoma wa serengeti nyamapori ni sehemu ya Kirago.

Ni wanyama wangapi kwa mwaka  ukilinganisha na wale wa leseni? Si kwamba natetea wavunao kwa leseni (ambao anaweza akaandikiwa na kulipia 10 akavuna 30) bado mimi naona uwindaji-haramu unamadhara mpaka ya mnyama kupata kilema akijinasua mtegoni na kuondoka na mguu mbovu.

Usikubali kila unaloambiwa na wananchi au mtu yoyote pande moja bila vidhibiti na kukaa nao kujadiliana na kupekua kiundani kukwepan kanyaboya.  Hapa nitataja Kisa cha Kijiji kimojawapo cha  jirani au karibu na Mji wa Mugumu-Serengeti.

Kisa:- Serikali ililaumiwa mpaka tukapata Kizunguzungu. Jamaa akaonyesha mkono wenye makovu ya ajabu akasema alipigwa na game scout kwa kuonewa (Wa National Park wakitembelea Game conservation area jirani na kijiji hicho), amechanywa na kisu na hayo ndio makovu ya matokeo ya uonevu. Tuliandika haraka peni zikatembea ilivyo.  Kumbe mwongo. Tukapiga picha na kuchukua maelezo. Lakini katika kusoma dalili za macho na kope za watu nikaona kuna zaidi baadae nikawafuata walionipiga UKOPE na nikaomba kunisindikiza kutembelea mazingira ya uchimbaji wa mawe ya rangi eneo hilo.  Wakasema kuniambia huyo ni juangiri kuu hapa kijijini. Alikuwa anawinda akaangukia mshale wake wa Sumu ikabidi akate nyaman kabla sumu haijamuingia na anti-poison alikuwa kaifunga mbali. Sisi kwetu ingekuwa taarifa ya UONEVU na kudhuru mwili kumbe ilikuwa-kanyaboya. Tukawauliza viongozi wa kijiji wakathibitisha na mengine mengi.
Kijijini tukapiga  mapicha kibao ya nyama pori zilizoanikwa ili kutetea haki ya kupata nyama-kumbe ulikuwa uwindaji haram. 

Alexandar nisikupotezee muda na wa wengine. Bado hizo takwimu za hela toka NCAA, Tanapa, Hotels na huyo Mohamed Ali-Ali-OBC mahesabu unaweza ukayapata. Shukrani ya mwindaji wa Loliondo ilikuwa kubwa Halmashauri ya Wilaya tu jinsi anavyotoa mafao, kujenga airport na mengine mengi niliyataja huko nyuma. Anyway-Hakuna Kizuri 100% duniani. Hata zile za NCAA kama mafao ya kufaidika kwa wananchi ndani ya NCAA kwenda kwa Pastoral Council-Vijiji-mamilioni. Ulizia kutumika kwake upate na Kizunguzuru uone na mahindi mabovu yaliyonunuliwa badala ya mazima. Vitu hivi vya ufisadi hata ngazi ya chini ya mtu kutetea jamaa zake kwa wapenda maendeleo vinatutia wazimu.

Fahamu hizi ni kazi ambazo wasomi hutumwa na GVT kama neutral people from academic institutions wenye uzoefu na kazi za jamii kuisaidia assessment na upangaji miradi au Evaluation fulani. Zinakusanya mpaka copy ya cheque hotel ilizotoa kupeleka halmashauri na kuuliza hela zilivyotiumika na vijiji pia walioipata toka halmashauri au miradi iliyohisaniwa na mafao mengine-scholarships kusomesha watoto kaya hadi kaya etc.

Zipo NGO zinazopenda maendeleo ya wananchi na zipo za 'Tumboni Street'. Wapige kelele waonekane ndio wapate uhisani na huko Loliondo ndio zimejaa NGO kila kona na humo NCAA kwa jamii. Wapo NGO wapendao haki na kuitetea kimamilifu na wanawajibika grassroots. Na wapo kama hao wa kuhamasisha nchi isitawalike mpaka damu imwagike. Na huwezi kuona maendeleo yakawa ya mfano hapo walipo pamoja na raslimali kuwepo na misaada iliyoletwa na wakifanyiwa auditing inakuwa utata kuonyesha zilivyotumika. Na pamoja na kutetea haki na Demokrasia, viongozi wengine ni viongozi wa kudumu hawaachii  ngazi maana ni ulaji. Toka kiundwe yeye ni director mpaka dunia iishe.Jiulize!!

Nitasaka auditing report mojawapo ya 1997 ya fund mojawapo toka UK niliipata kwa siri huko UK na waliazimia kutokuwapa hela NGO hizo kutokana nan ufisadi. Chipalazya nikumbushe niisake nikuvurumishie.

Nikuulize Kijana mwanaharakati-Tunaponunua Faru kutoka South Africa na kuwapeleka katika Zuu la Kuzalisha Faru na Mbwamwitu Mkomazi kwa Tony fitzjohn hao Faru wanakuwa nyani au ni Rhino mnyama Pori? Tumemaliza mbwa mwitu kwa kuwaua kwa sumu. Mbwa mwitu ni mnyama muhimu katika kurekebisha wingi wa wanyama wabaya wala watu. Mbwa mwitu wanakuja kwa ndege-Jee tunakuwa tumeleta panya buku au wanyamapori toka mbuga za wenyetu tumenunua? Nilisoma gazetini kuna Faru aliitwa jina la Mhemshimiwa-Kikwete. Hata wale Faru wa Kenya waliokuwa na bodu guard watano Faru mmoja wameuawa na majangiri.

Sasa, kama tunanunua toka S.A wanapanda meli au ndege-kwa nini nasi tusiuze na ruhusa za kuuza  mnyama nlive zipo katika hifadhi za wanyama pori duniani? Ndio maana nchi nyingine hazina wanyama zinanunua na kuweka Zoo nchini kwao. wengine wananunua wanyama kwa utafiti wa madawa ya wanyama na binadamu ingawanye wanaharakati wa haki za wanyama huleta utata. Usije ukashangaa ukatembea hovyo Uk, au USA ukaliwa na Simba aliyetoroka kwenye Zoo au ukakumbatiwa na gorilla barabarani kama ilivyotokea hivi majuzi ulaya. wanyama hawa wananunuliwa nchimbalimbali kulinganisha na harvesting quotas za live animals. wanaojua sheria za wanyama pori mauzo ya live animals na ya uwindaji watatujuza.

-Pamoja na matatizo mengine-kumbuka ile case ya wasomali kutamba Loliondo kukaa ktk maboma huko na ugomvi uliotokea baadae kufa police kamanda Soitsambu katika mapambano baada ya marriage of convenience kuisha na serikali kupata taarifa. Kuna kilimo kikubwa sana tulikikuta baadhi ya vijiji na wanalima kwa plough za ng'ombe na unaona wanyama pori pembeni na mifugo ktka mabanda solid ya mbao ya mloliondo huko engerosambu, baadhi ya maeneo ya soitsambu. Kuna maeneo utaonyeshwa mpaka makazi ya wageni ila watakuambia (usinitaje kama ndiye niliyokuonyesha). Wageni Tanzania wapo Mikoa yote tunawakaribisha wenyewe. Kuna hatua viongozi/madiwani wa makabila ya wafugaji wamechukua kuondoa ukaukaji wa vyanzo vya maji maeneo ya wanyama pori NCAA na Loliondo pia vijiji vya Tarangire -Simanjiro kwa wafugaji kwa kudhibiti ukiukwaji hata wa Mila na bado wana matatizo. Olbalbal-NCA ni mahala pamoja wapo Diwani alifanya kazi kubwa. Niliwekaga mapicha humu huko nyuma ya Loiborsirret-Tarangire na degradation ya mto na ardhi. Si Loliondo tu kuwa tatizo. Hata ukienda Terrat kwa wafugaji ambapo ndio makao makuu ya NGO ya wafugaji, pana na radio station, kituo kikubwa-Mto terrat chanzo chake cha maji na mto umekuwa degraded. Mifugo na wanyama pori inapata tabu.

Conservation biology imeshatupa maone kuwa wanyama pori wengi wapo jirani na makazi na maelezo yake mengi. Hili la wanyama kuwa karibu na watu si hadithi ya leo, kuna sababu zake nyingi pamoja na kuwa na Mosaic ya vegetation za lishe kwa kuwa binadamu anafanya modification na environment kwa kulima, kuchoma moto etc. Na ndio maana mbvuga hufanya controlled bushfire ili kuwapa lishe wanyama.  Wanasayansi wa wildlife na conservation biology wakakutan Bali-Indonesia 1982 na maeneo mengine baadae na kukubaliana masuala ya 'Conservation with Development'  (as part of benefit sharing); kuwe na benefit sharing kwa walindao wanyama na wanaoathirika na wanyama na misitu au mradi wowote ule wa conservation. Na ndio kuna concept ta Particiaptory Forest management, CBNRM, Wildlife Management Areas (WMAs). Ukitaka kujua hasa wananchi wanafaidikaje na NCAA, Serengeti national park, Loliondo na OBC please toa tender, tafuta neutral organizations, zikapekue mafao yaliyotolewa na evidence zake halafu ndio uanze kulaumu.

Kweli Benefit sharing muhimu, kushirikisha wananchi ndio wimbo na sala ya maendeleo. basi yarekebishwe pale yalipokosewa tusije tukaingia vitani na tunazuia utalii usituingizie mapato. Umefika wakati sasa NGO kuunda Tanzania NGo volunteer Services yenye wataalamu mbali mbali ktk sekta mbali mbali ili kutoa ajira kwa wasomi vijana waende vijijini kusaidia upangai na utekelezaji maendelea ili tupunguze lelemama. usishangae-mharibifu na muhujumu naye hulalama. Hata atupaye takataka ndani ya mtaro zikakwama na kutoacha tabia ya uchafu, maji yakishindwa kupita yakafurika ndani ya nyumba akapoteza mali na uhai wa familia yake-hulalama kuwa serikali haimjali-sembuse kwenye ardhi kama mali asili ulinzi na matumizi yake hakutokosa lawama, kulaumiana na ulalamishi.
 
Tanzania nakulilia nani atakukomboa! Utaikomboa mwenyewe kwa kulinda raslimali zake, kutumia kwa kuangalia uwezo wa raslimali hizo sio kuzidi uwezo, kuwa mkweli, mchapa kazi, unayekubali kubadilika kulingana na wakati, uchumi na technolojia lakini bila ya kukiuka maadili ya mila na nchi; mpenda na mtenda haki, mwenye macho yanayoona pande zote kama kinyonga ili ujue jema na baya, kuuona na kuukubali ukweli, kuacha shutuma pande moja daima, kuwa mtu wa Mungu, kuona pande zote hizo kujua nani anafanya nini na nani wa kumuhusisha ambaye mtapanga malengo tekelezeki na ambayo yatafikia viashiria mlivyoweka. Jee-Upo tayari?

Mungu ibariki Tanzania.





--- On Thu, 4/4/13, alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com> wrote:

From: alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com>
Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA NGOS KUHUSU MGOGORO WA ARDHI WA LOLIONDO
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, 4 April, 2013, 12:29

Hivi viongozi wa nchi za kiafrica wananini jamani?

Kisa kama hicho kinaendelea Tana River naTana Delta Districts, Kenya. Huko serikali ya Kenya imewapa waarabu wa Qatar ardhi ya wana vijiji ili walime kwa ajili ya kuexport chakula nchini kwao kwa makubaliano kua kenya itajengewa bandari. Zoezi hilo lilifanyika bila kuwashirikisha wanavijiji. Mbaya zaidi Wanavijiji hawajaambiwa wao watafaidika vipi kutokana na ardhi yao kupotelea mikononi mwa 'mwaraabu muekezaji'. Je! katika hali ya kawaida unatehgemea nini hapo mbeleni?? je hicho kilimo kitapata support kutoka kwa community. Ardhi ikichukuliwa kwa dhuruma hata uwekezaji juu yake hauwezi kua salama. Rukwa magazeti yalireport kua Shamba la mahindi la Efatha Ministry lenye ekari 25 zilifyekwa usiku na watu wasiojulikana. Kuna wanavijiji wengi wanalalalmika kua ardhi yao ilichukuliwa bila utaratibu; yamkini ilikua revenge.

Tukumbuke kua pia hao hao waarabu hapa kwetu wamechukua wanyama wetu hai tena na ndege ya kijeshi. Mpa sasa hivi hatuoni chamaana kinaendelea. Nilitegemea GVT ya Tanzania itaiamuru serikali ya Qatar kuwarejesha wanyama wetu, na wasipokubali funga ubalozi wao. Lakini wapi! Hivi wanapo apa kua wata ilinda nchi na katiba yetu huwa wanamaanisha kweli?.

Hizi NGOs zinasema kua mwaraabu mfalme Brigadia Mohamad Al-Ali amepewa haki ya kufanya uwindaji katika ardhi ya vijiji bila wao kushirikiswa. Hivi tuseme tumesahau kua waarabu na wazungu ndio kwa karne na karne walituuza utumwa na kutuua?? Hata baada ya uhuru the so called 'mwekezaji' anaonekana bora kuliko mzawa. Masikini Tanzania nakulilia nani atakukomboa!
Alexander



From: lucas haule <kisacha2003@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, April 4, 2013 1:13 PM
Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA NGOS KUHUSU MGOGORO WA ARDHI WA LOLIONDO

Viongozi wa serikali yetu ukiwaangalia ni kama midubwana imevaa ngozi ya binadamu. Kila nikisoma habari za viongozi wa nchi hii, kuwa vibaraka wa wageni, moyo wangu unauma sana. Yaani yamekuwa kama makasha yatembeayo. Siku zinakuja..........

--- On Thu, 4/4/13, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:

From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
Subject: [wanabidii] TAMKO LA NGOS KUHUSU MGOGORO WA ARDHI WA LOLIONDO
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, April 4, 2013, 2:45 AM

TAMKO LA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI TANZANIA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MGOGORO WA ARDHI WA LOLIONDO
Pori tengefu la Loliondo ni eneo lililopo mashariki mwa hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Eneo hili linajumuisha vijiji ambavyo vinatambulika kisheria tangu wakati wa ukoloni na kulindwa kisheria na sheria ya ardhi ya vijiji Na. 5 ya mwaka 1999 na sheria ya Serikali za Mitaa, Tawala za Wilaya namba 7 ya Mwaka 1982. Vijiji hivyo ni Ololosokwan, Soitsambu, Oloipiri, Olorien, Maaloni, Arash, Malambo na Piyaya.  Eneo hili pia limekuwa likijulikana kama pori tengefu la Loliondo kulingana na sheria ya wanyama pori ya mwaka 1974 na sheria ya wanayma pori namba 5 ya mwaka 2009 ambazo zote hazija badilisha hadhi ya vijiji vilivyopo wala haki za ardhi za wenyeji wa vijiji husika wala hazihamishi haki hizo kwenda kwa mamlaka nyingine yoyote ikiwemo wizara ya malisaili na Utalii. Itambulike kwamba hadhi ya pori tengefu haingilii hadhi ya umiliki wa ardhi bali inatoa mamlaka kwa mkurugenzi wa wanyama pori kusimamia wanyama pori waliopo katika eneo hilo pamoja na kutoa mamlaka ya kugawa vitalu vya uwindaji kwa makampuni ya uwindaji bila kuingilia haki za ardhi kwa wakazi wa maeneo husika. Aina hii ya mgawanyo, usimamizi na matumizi ya ardhi na rasilimali zake imekuwa ndicho kiini kikubwa cha mgongano wa maslahi na migogoro ya mara kwa mara katika eneo hili na maeneo mengine yenye sifa ya aina yake.
Mwaka 1992 serikali ilimruhusu mwana mfalme Brigadia Mohamad Al-Ali kupitia kampuni ya Otterlo Business Corporation (OBC)  kuwinda ndani ya vijiji vya tarafa vya Loliondo na Sale. Ruhusa hiyo haikufuta haki na uhalali wa wananchi wa kuendelea kuwepo na kutumia ardhi yao kulingana na sheria ya Ardhi ya vijiji ya mwaka 1999 na sheria ya serikali za mitaa, tawala za wilaya.
Tangu wakati huo kumekuwepo na upotoshaji mkubwa kuhusu uhalali wa umiliki wa eneo la Loliondo ambao umefanywa na serikali kwa lengo la kuilinda kampuni ya uwindaji ya OBC. Upotoshaji huo umekuwa ukifanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii na uongozi wa Mkoa wa Arusha na wilaya ya Ngorongoro na kupelekea wananchi kutolewa kwa nguvu katika maeneo hayo kwa madai mbalimbali ikiwa ni pamoja na madai kuwa wananchi wa Loliondo ni wakenya, waharibifu wa mazingira na kuongezeka kwa watu na mifugo. Upotoshaji huu umekuwa na lengo la kuwaahadaa umma wa Watanzania  na ulimwengu kwamba eneo lote la Loliondo ni eneo la hifadhi pekee na siyo ardhi ya vijiji na kwamba wananchi ni wavamizi wa eneo hilo jambo ambalo siyo sahihi wala halina uhalali wowote wa kisheria.
Kutokana na nia ya serikali kuwaondoa wananchi katika maeneo yao ya vijiji vyao kumekuwepo na harakati mbalimbali za wizara kutumia mbinu mbalimbali za kumega na kupokonya kilomita za mraba 1500 ya ardhi ya vijiji na kuikabidhi kampuni ya OBC kwa kisingizio cha kwamba wanawagawia wananchi sehemu ya pori tengefu la Loliondo. Jambo hili siyo sahihi kwani ardhi hiyo ni ardhi ya vijiji husika.
Tarehe 21 Marchi 2013 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Balozi Khamisi Khagasheki, alitoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari. Taarifa hiyo ina kichwa cha habari  "Wizara ya Maliasili kurekebisha mipaka na ukubwa wa eneo la Pori tengefu la Loliondo kutoka Kilometa za mraba 4,000 hadi 1500". Katika taarifa hiyo Waziri ametangazia umma kwamba serikali imeamua kupunguza ukubwa wa eneo hilo ili kutatua migogoro iliyopo katika eneo hilo, kunusuru ikolojia ya hifadhi ya Serengeti, Ngorongoro na Pori tengefu la Loliondo.
Vilevile katika tamko lake Waziri alielezea sababu zingine kwamba ni kulinda masalia ya wanyama pori, mapito na vyazo vya maji kwa ajili ya ustawi wa hifadhi kwa manufaa ya wananchi wenyewe na taifa kwa ujumla. Pia waziri alizungumzia kwamba wananchi wataweza kuanzisha hifadhi za wanyama pori (WMA)  katika ardhi itakayobaki kuwa ardhi ya vijiji.
Kutokana na tamko hili la Mh. Waziri , SISI mashirika ya kiraia yanayojihusisha na utetezi wa Haki za Ardhi na Haki za Binandamu na ambao tumekuwa tukifuatilia suala hili kwa karibu sana tunapenda kujulisha umma wa watanzania kama ifuatavyo;
  1. Kwamba siyo kweli serikali inawaachia wananchi ardhi yenye ukubwa wa kilomita za mraba 2500 kwani ardhi hiyo ni ardhi ya vijiji iliyopo ndani ya mipaka ya vijiji na kinachofanyika ni kuwapokonya wananchi ardhi iliopo ndani ya mipaka ya vijiji vyao yenye ukubwa wa kilomita za maraba 1500 na kumpatia mwekezaji wa OBC.
  2. Hakuna eneo lolote alilopewa OBC kama waziri alivyo potosha katika ukurasa wa pili wa taarifa  yake  kwa umma kwamba "serikali ipo tayari kuangalia upya eneo kubwa alilopewa OBC na ikibidi litapunguzwa…"            Ukweli ni kwamba OBC iko katika eneo la pori tengefu la Loliondo ndani ya vijiji husika  kwa kibali cha kuwinda tu na sio umiliki wa ardhi na hawakuwahi kupewa ardhi anayodai  Mh Waziri kwamba wamepewa. Vilevile waziri anatuaminisha kwamba mgeni amemilikishwa ardhi ya Loliondo jambo ambalo ni kinyume cha sheria  ya ardhi na sheria ya uwekezaji inyokataza wageni kumiliki ardhi isipokuwa kwa kuwekeza tu.
  3. Kwamba uamuzi wa serikali wa kugawa eneo la vijiji na kulifanya kuwa pori tengefu unachochea mgogoro uliopo. Kusema kuwa serikali inawagawia wananchi eneo watakaloikalia ni upotoshaji kwani  wananchi  ndio wenye haki ya kugawa eneo lolote ndani ya mipaka ya vijiji vyao  kwa matumizi watakayoamua wao.  Serikali kudai kuwagawia wananchi eneo ambalo tayari ni la kwao inatosha kuchochea mgogoro katika eneo hilo na ni dalili ya serikali kutaka kutumia mabavu kama ilivyotokea mwaka 2009.
 
  1. Kwamba siyo kweli kuwa serikali ina lengo la kuinusuru ikologia ya hifadhi ya Serengeti ila ina lengo la kumpatia mwekezaji (OBC) eneo la kuwindia bila kuzingatia sheria na matakwa ya wananchi wa vijiji husika. Hili pia halina ukweli wowote kwani serikali wasingeruhusu uwindaji ufanyike kama wangekuwa na uchungu wa kuwalinda wanyama pamoja na ikolojia hiyo. Hili linadhihirishwa na wanyama wenyewe kukimbilia karibu na maboma ya wafugaji ili kuwakimbia wawindaji  wa OBC kwani wanyama pori wanajisikia wako salama zaidi wanapokuwa karibu na mifugo kuliko kuwa karibu na wawindaji.
  2. Siyo kweli kwamba serikali inataka kulinda vyanzo vya maji  kama anavyodai Mh Waziri. Hili linadhihirishwa na ujenzi wa kambi ya kudumu ya OBC  kwenye chanzo cha mto wa Olasae linalotegemewa na wanyamapori pamoja na wanakijiji wa kijiji cha Soit Sambu , Arash,Ololosokwa na Kirtalo. Ujenzi huu umefanywa na kampuni ya OBC ndani ya mita 10 kutoka chanzo cha maji  kinyume cha sheria.
  3. Taarifa ya Mh. Waziri haikuzingatia suala la utawala bora wala sheria ya wanyama pori ya mwaka 2009 kifungu cha 16(5) ikinachomtaka kwamba hakuna ardhi ya kijiji itakayoingizwa ndani ya pori tengefu. Kipengele hiki kinasomeka kama ifuatavyo;  16(5) "For the Purposes of subsection (4), the Minister shall ensure that no land faIling under the village land is included in the game controlled areas."  Kipengele cha 16(6) "Subject to subsection (4), the Minister shall, in consultation with the relevant authorities, make regulations prescribing the manners in which sustainable management of game controlled areas shall be achieved."
Kutokana na maelezo yetu hapo juu sisi  mashirika ya hiari tunaitaka serikali kutekeleza yafuatayo;
  1. Serikali iache mara moja mpango wake wa kugawa ardhi ya wananchi kwa manufaa ya mwekezaji kwa kisingizio cha manufaa ya umma badala yake itambuwe ardhi yote ya Loliondo kama ardhi ya vijiji na kuwaachia vijiji kujipangia matumizi yao ya ardhi kwa njia shirikishi na mujibu wa sheria za ardhi.
  2. Kuacha mara moja kupotosha umma kwamba ardhi hiyo siyo ya vijiji na izingatie sheria kwa kuvipa vijiji haki yao ya kujiamulia mambo yao wenyewe kwa kutumia sheria zilizopo za ardhi na za serikali za mitaa.
  3. Serikali iweke bayana  kwa umma nia  yake ya kuchukua ardhi hii kwamba ni kwa ajili ya mwekezaji wa OBC badala ya kisingizio cha uhifadhi wa mazingira na sio vinginevyo.
  4. Serikali iache mara moja vitisho kwa wananchi wa Loliondo na wawakilishi wao, wanaharakati, mashirika na waandishi wa habari wanaofuatilia mgogoro huu. Serikali kuendelea kutishia makundi haya inakiuka haki ya kikatiba ya kupata habari na kuzuia jamii kuelimishwa juu ya haki zao za kikatiba na kisheria kwa manufaa yao wenyewe na taifa kwa ujumla. Kufanya hivyo ni kuwanyima haki yao ya kupata taarifa na kutoa maoni kama inavyolindwa na katiba ya Tanzania na mikataba ya Kimataifa ambayo serikali imeridhia.
  5. Serikali iache mara moja kudharau na kuingilia utendaji wa  mhimili wa mahakama kwa kuacha kuingilia suala la Loliondo kwa kuzingatia kuwa tayari kuna kesi ya kikatiba (MISC CIVIL CAUSE NO 15/2010) iliyofunguliwa katika mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha ambapo Waziri wa Maliasili  na Utalii na mwekezaji wa OBC ni miongoni mwa  wa walalamikiwa.
 
  1. Serikali iache mara moja visingizio kwamba mgogoro wa Loliondo unasababishwa na wanaharakati na mashirika ya nje kwani yenyewe inatambua uwepo wa mgogoro huo unasababishwa na maamuzi ya serikali ya kugawa ardhi ya wananchi bila kuwashirikisha kwa kuangalia upande mmoja wa manufaa kwa wawekezaji tu bila kuangalia athari kwa wananchi.
  2. Serikali iache matumizi mabaya ya  vyombo vya usalama hasa jeshi la polisi ambalo hutumiwa kuwaondoa wananchi katika makazi yao kwa nguvu huku wakisababisha athari kubwa kwa wasiojiweza, wanawake na watoto.
 
TAMKO HILI LIMETOLEWA LEO TAREHE 4 APRILI 2013 NA MASHIRIKA AMBAYO NI;
  1. PINGOs Forum
  2. Tanzania Land Alliance- TALA
  3. Haki Ardhi
  4. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu- LHRC
  5. Tanzania Human Rights Defenders
  6. Tanzania Gender Network Program (TGNP)
  7. Tanzania Natural Resource Forum –TNRF
  8. Cords
  9. Ujamaa Community Resource Team- CRT
  10. Pastoralists Women Council –PWC
  11. Ngorongoro NGOs Network –NGONET
  12. Tanzania Pastoralists Community Forum-TPCF
  13. OSEREMI
 
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment