Saturday 6 April 2013

Re: [wanabidii] TAMKO LA NGOS KUHUSU MGOGORO WA ARDHI WA LOLIONDO

Wanayasoma sana hapa watu wa kila aina haya tuandikayo. Ninasema hivyi kwa sababu, wakati wa evaluation sisi tunaona madudu na ukweli mwingi. Tuankuta kilimo ndani ya wildlife conservation area. tunakuta ukataji miti migumu ya mloliondo ipo lundo mpakani inapelekwa Kenya. tunakuta uhamiaji tunaelezwa kwa siri boma lile, lile. Tunakuta uharibifu wa vyanzo vya maji na kilimo cha mashamba makubwa zaidi ya ekari zilizoruhusiwa. Twakusanya evidence za mafao ukiuliza zimetumikaje-wanapanda mori. Evaluation daima hujenga utata kama sio uadui na auditing ndio usiombe. mafao yatolewayo yana vidhibiti hata hoteli zina copy ya cheque za 10% bed fee wanapeleka wilayani. Wengine wamehamasisha jamii walime bustani ili wasiende Arusha kununua kabichi, karoti, sukuma wiki, mayai bali wapate jirani toka kwao na kuwasaidia mbegu-kaputi hawapo interested. akiuza mara moja na kupata hela-nauli Mererani au DSM. Binafsi niliomba enzi za zama za mid 1980s hela toka SIDA laki 4 kusaidia akina mama kijiji cha Robanda wafuge kuku wa kienyeji wa mayai na nyama. Kijiji kipo mbali na Mji wa wilaya karibu na gate la kuingia serengeti ukitokea Mugumu. Wana walikuwa na mashine ya kusaga mahindi na tuliwasaidia kuboresha borehole yao ya maji. Huo mradi waliutaka wao ili kujikimu maana hata wafanyakazi wa park enzi hizo wakienda kijijini hapo kupata mahitaji. kuuza nyama na mayai mahoteli na jamii ya mbuga ingewapa vijisenti. Dona alitoa hela, ajabu zikaingia account ya wilaya badala ya kikundi. wajanja wakafanya hivyo nikiwa likizo lakini niliporudi-ilikula kwao. DED akahakikisha aliwakata kutoka mishahara yao ikaingia akaunti ya kikundi husika ile hela. Lakini mradi haukufika mbali expectation za wanakikundi zinakuwa za ajabu, kujituma na kuwajibika kuchangia ulishaji kuku inavyotakiwa watoe yai standard sio la mjusi au dogo kama la njiwa inakuwa tatizo. anyway-kutangaza mafao in cash or inkind OBC, Hotels, TANAPA, NCAA na wengineo ni muhimu kuondoa utata. Pia muhimu ni kuandika sheria za wanyama pori ili watu wasifahamu. Maana yake live capture or curling of wild animals inaruhusiwa idadi ya uzao wao ikifika na kupita.

Tufahamishwe kuwa wanyama nao kuna carrying capacity yake. Ukiwaachia nyumbu wawe mabilioni, pia mbwa mwitu au simba unataka kuleta balaa. Pia, kuondoa tembo uache wawindwe wafe waishe-utaua wanyama wengi sana wanaomtegemea yeye afanye modification ya mazingira ili wao wale waweze kuishi. na hivyo utakavyoacha kununua Mbwa mwitu, kuwazalisha na kuwatawanya kila wananapopungua na fisi kuwepo-Simba zitakuwa nyingi hadi kupishana nazo DSM. Kama tunanunua live animals-vipi sisi kuuza ikawe nongwa? Isitoshe- awindaji wanapokuwepo wakati wa msimu wa kuwinda-wanatoa ajira kuanzia Kuli wa kubeba mizigo na wasindikizaji, wachunaji wanyama waliowindwa, walinzi, kisha wao wanachukua trophies nyama inapelekwa kijijini ambapo huuzwa ktk busha la WMA yao. Au kama hakuna WMA (wamekataa) inauzwa kijijini. Viajna wa Ausha wakati wa msimu wa kuwinda na utalii ni busy ajabu na magari yao. wanajitahidi kuwa waaminifu kwa wageni ili wasikose ajira. Na sasa tour drivers wengi wamejifunza kiingereza na lugha nyingine. Tusiangalie mabaya tu-twende tukafanya utafiti-tutembelee. Tutakuja kuona hao wanaolalama hawafaidiki kuna mamilioni wameshindwa kuyatolea maesabu/mrejesho yametumikaje; wamezidisha uharibifu wa vyanzo vya maji kiasi kwamba hata mifugo yao inahaha na akina mama kuhangaikia maji mwendo mrefu. Wamekaribisha wageni wanaofaidi raslimali zetu. Kuchukua eneo kulilinda ili maji yapatikane kwa wanyama Pori na mifugo yao-ni jambo la busara kama kuna uharibifu kama nilioutaja wa Mto Terrat, Loiborsirret araound-Taragire N.P; Uharibifu wa Msitu wa Loliondo na vijito vyake na vijito ndani ya vijiji vya Loliondo ambavyo wanyama hutegemea pia. Ardhi inakua wazi, kavu-jangwa kutokana na ulimbikizaji mifugo na uchimbaji madini. Tulisalame tu wakati tunahusika pia na uchakachuaji mazingira. Tupange kwa pamoja-kieleweke ndugu yangu.

--- On Sat, 6/4/13, alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com> wrote:

From: alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com>
Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA NGOS KUHUSU MGOGORO WA ARDHI WA LOLIONDO
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, 6 April, 2013, 20:03

Madam Kiwasila,
Hili pendekezo lako likifanyika litasaidia kupunguza ulalamishi. Sijui kama hapa jukwani kuna watu wa-TANAPA watusaidie kulifikisha kwa wahusika.
Alexander

From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Saturday, April 6, 2013 9:37 PM
Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA NGOS KUHUSU MGOGORO WA ARDHI WA LOLIONDO

Ninaomba, ikiwezekana, serikali upande wa TANAPA, waanze kutangaza katika vipindi vya TV ya Taifa na nyinginezo na magazeti kwa Kiingereza na Kiswahili na Newsletter yao kuorodhesha mafao yaliyotolewa na mbuga zake kwenda kwa jamii kutokana na fee za kuingia mbugani, uwindaji, WMA, NCAA; fedha kutoka wawindaji kama OBC kwenda halmashauri na vijiji katika eneo la hunting block; fedha ambazo hoteli za kitalii zimetoa kama 10% ya daily bed fee kwenda halmashauri na miradi ya hotel ya kusaidia vijiji directly ambavyo vimeomba msaada au ina mipango ya kuvisaidia ktk kutoa ajira, kununua mazao yao na kuwapa fedha taslimu, mafunzo. Hii itatoa picha maalum jinsi ya mali asili inavyowasaidia na kufaidisha wahusika. Mfano-Mikumi National park kwa mwaka imetoa shs kwa wilaya zinazoizunguka, miradi gani ya vijiji gani imehisani; kusafirisha wanavijiji wenye kupeleka mazao gulioni na kuwarudisha na mizigo yao, kusomesha vijana Veta etc; hela directly kijijini kama wanatoa. Hapo viongozi fisadi wazilazo wananchi wakiwa hawafahamu wanaadhirika na kuhama mji. NCAA kwa mfano ikitoa gazetini mihela itoayo, vijana wasomeshwao na huyo OBC etc wakifanya hivyo na misaada yao yote na mihela by village itasaidia na orodha ya mtoto wa nani alisomeshwa shule au nchi gani kwa gharama gani, kila aina ya ujenzi by fiscal year-hapatokalika.

--- On Thu, 4/4/13, john mahaba <mahabajo@yahoo.com> wrote:

From: john mahaba <mahabajo@yahoo.com>
Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA NGOS KUHUSU MGOGORO WA ARDHI WA LOLIONDO
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, 4 April, 2013, 11:52

Serikali kila siku inaongelea kuhusu ushirikishaji wa jamii katika
m,asuala muhimu ya kimaendeleo. hivi huwa inahubiri tu bila kutenda?
binafsi suala hili linahitaji utashi wa kiuchumi zaidi ya utashi wa kisiasa
kwani kama ni faida ipatikanayo na serikali kutoka kwenye pori hili basi
wananchi wa Loliondo nao wawe wa kwanza kufaidikia na uwepo wa pori
 hili tofauti na hivyo ubabe hautatusaidia chochote kwani wanachi wameshaamuka.

From: lucas haule <kisacha2003@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, April 4, 2013 2:13 PM
Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA NGOS KUHUSU MGOGORO WA ARDHI WA LOLIONDO

Viongozi wa serikali yetu ukiwaangalia ni kama midubwana imevaa ngozi ya binadamu. Kila nikisoma habari za viongozi wa nchi hii, kuwa vibaraka wa wageni, moyo wangu unauma sana. Yaani yamekuwa kama makasha yatembeayo. Siku zinakuja..........

--- On Thu, 4/4/13, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:

From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
Subject: [wanabidii] TAMKO LA NGOS KUHUSU MGOGORO WA ARDHI WA LOLIONDO
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, April 4, 2013, 2:45 AM

TAMKO LA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI TANZANIA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MGOGORO WA ARDHI WA LOLIONDO
Pori tengefu la Loliondo ni eneo lililopo mashariki mwa hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Eneo hili linajumuisha vijiji ambavyo vinatambulika kisheria tangu wakati wa ukoloni na kulindwa kisheria na sheria ya ardhi ya vijiji Na. 5 ya mwaka 1999 na sheria ya Serikali za Mitaa, Tawala za Wilaya namba 7 ya Mwaka 1982. Vijiji hivyo ni Ololosokwan, Soitsambu, Oloipiri, Olorien, Maaloni, Arash, Malambo na Piyaya.  Eneo hili pia limekuwa likijulikana kama pori tengefu la Loliondo kulingana na sheria ya wanyama pori ya mwaka 1974 na sheria ya wanayma pori namba 5 ya mwaka 2009 ambazo zote hazija badilisha hadhi ya vijiji vilivyopo wala haki za ardhi za wenyeji wa vijiji husika wala hazihamishi haki hizo kwenda kwa mamlaka nyingine yoyote ikiwemo wizara ya malisaili na Utalii. Itambulike kwamba hadhi ya pori tengefu haingilii hadhi ya umiliki wa ardhi bali inatoa mamlaka kwa mkurugenzi wa wanyama pori kusimamia wanyama pori waliopo katika eneo hilo pamoja na kutoa mamlaka ya kugawa vitalu vya uwindaji kwa makampuni ya uwindaji bila kuingilia haki za ardhi kwa wakazi wa maeneo husika. Aina hii ya mgawanyo, usimamizi na matumizi ya ardhi na rasilimali zake imekuwa ndicho kiini kikubwa cha mgongano wa maslahi na migogoro ya mara kwa mara katika eneo hili na maeneo mengine yenye sifa ya aina yake.
Mwaka 1992 serikali ilimruhusu mwana mfalme Brigadia Mohamad Al-Ali kupitia kampuni ya Otterlo Business Corporation (OBC)  kuwinda ndani ya vijiji vya tarafa vya Loliondo na Sale. Ruhusa hiyo haikufuta haki na uhalali wa wananchi wa kuendelea kuwepo na kutumia ardhi yao kulingana na sheria ya Ardhi ya vijiji ya mwaka 1999 na sheria ya serikali za mitaa, tawala za wilaya.
Tangu wakati huo kumekuwepo na upotoshaji mkubwa kuhusu uhalali wa umiliki wa eneo la Loliondo ambao umefanywa na serikali kwa lengo la kuilinda kampuni ya uwindaji ya OBC. Upotoshaji huo umekuwa ukifanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii na uongozi wa Mkoa wa Arusha na wilaya ya Ngorongoro na kupelekea wananchi kutolewa kwa nguvu katika maeneo hayo kwa madai mbalimbali ikiwa ni pamoja na madai kuwa wananchi wa Loliondo ni wakenya, waharibifu wa mazingira na kuongezeka kwa watu na mifugo. Upotoshaji huu umekuwa na lengo la kuwaahadaa umma wa Watanzania  na ulimwengu kwamba eneo lote la Loliondo ni eneo la hifadhi pekee na siyo ardhi ya vijiji na kwamba wananchi ni wavamizi wa eneo hilo jambo ambalo siyo sahihi wala halina uhalali wowote wa kisheria.
Kutokana na nia ya serikali kuwaondoa wananchi katika maeneo yao ya vijiji vyao kumekuwepo na harakati mbalimbali za wizara kutumia mbinu mbalimbali za kumega na kupokonya kilomita za mraba 1500 ya ardhi ya vijiji na kuikabidhi kampuni ya OBC kwa kisingizio cha kwamba wanawagawia wananchi sehemu ya pori tengefu la Loliondo. Jambo hili siyo sahihi kwani ardhi hiyo ni ardhi ya vijiji husika.
Tarehe 21 Marchi 2013 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Balozi Khamisi Khagasheki, alitoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari. Taarifa hiyo ina kichwa cha habari  "Wizara ya Maliasili kurekebisha mipaka na ukubwa wa eneo la Pori tengefu la Loliondo kutoka Kilometa za mraba 4,000 hadi 1500". Katika taarifa hiyo Waziri ametangazia umma kwamba serikali imeamua kupunguza ukubwa wa eneo hilo ili kutatua migogoro iliyopo katika eneo hilo, kunusuru ikolojia ya hifadhi ya Serengeti, Ngorongoro na Pori tengefu la Loliondo.
Vilevile katika tamko lake Waziri alielezea sababu zingine kwamba ni kulinda masalia ya wanyama pori, mapito na vyazo vya maji kwa ajili ya ustawi wa hifadhi kwa manufaa ya wananchi wenyewe na taifa kwa ujumla. Pia waziri alizungumzia kwamba wananchi wataweza kuanzisha hifadhi za wanyama pori (WMA)  katika ardhi itakayobaki kuwa ardhi ya vijiji.
Kutokana na tamko hili la Mh. Waziri , SISI mashirika ya kiraia yanayojihusisha na utetezi wa Haki za Ardhi na Haki za Binandamu na ambao tumekuwa tukifuatilia suala hili kwa karibu sana tunapenda kujulisha umma wa watanzania kama ifuatavyo;
  1. Kwamba siyo kweli serikali inawaachia wananchi ardhi yenye ukubwa wa kilomita za mraba 2500 kwani ardhi hiyo ni ardhi ya vijiji iliyopo ndani ya mipaka ya vijiji na kinachofanyika ni kuwapokonya wananchi ardhi iliopo ndani ya mipaka ya vijiji vyao yenye ukubwa wa kilomita za maraba 1500 na kumpatia mwekezaji wa OBC.
  2. Hakuna eneo lolote alilopewa OBC kama waziri alivyo potosha katika ukurasa wa pili wa taarifa  yake  kwa umma kwamba "serikali ipo tayari kuangalia upya eneo kubwa alilopewa OBC na ikibidi litapunguzwa…"            Ukweli ni kwamba OBC iko katika eneo la pori tengefu la Loliondo ndani ya vijiji husika  kwa kibali cha kuwinda tu na sio umiliki wa ardhi na hawakuwahi kupewa ardhi anayodai  Mh Waziri kwamba wamepewa. Vilevile waziri anatuaminisha kwamba mgeni amemilikishwa ardhi ya Loliondo jambo ambalo ni kinyume cha sheria  ya ardhi na sheria ya uwekezaji inyokataza wageni kumiliki ardhi isipokuwa kwa kuwekeza tu.
  3. Kwamba uamuzi wa serikali wa kugawa eneo la vijiji na kulifanya kuwa pori tengefu unachochea mgogoro uliopo. Kusema kuwa serikali inawagawia wananchi eneo watakaloikalia ni upotoshaji kwani  wananchi  ndio wenye haki ya kugawa eneo lolote ndani ya mipaka ya vijiji vyao  kwa matumizi watakayoamua wao.  Serikali kudai kuwagawia wananchi eneo ambalo tayari ni la kwao inatosha kuchochea mgogoro katika eneo hilo na ni dalili ya serikali kutaka kutumia mabavu kama ilivyotokea mwaka 2009.
 
  1. Kwamba siyo kweli kuwa serikali ina lengo la kuinusuru ikologia ya hifadhi ya Serengeti ila ina lengo la kumpatia mwekezaji (OBC) eneo la kuwindia bila kuzingatia sheria na matakwa ya wananchi wa vijiji husika. Hili pia halina ukweli wowote kwani serikali wasingeruhusu uwindaji ufanyike kama wangekuwa na uchungu wa kuwalinda wanyama pamoja na ikolojia hiyo. Hili linadhihirishwa na wanyama wenyewe kukimbilia karibu na maboma ya wafugaji ili kuwakimbia wawindaji  wa OBC kwani wanyama pori wanajisikia wako salama zaidi wanapokuwa karibu na mifugo kuliko kuwa karibu na wawindaji.
  2. Siyo kweli kwamba serikali inataka kulinda vyanzo vya maji  kama anavyodai Mh Waziri. Hili linadhihirishwa na ujenzi wa kambi ya kudumu ya OBC  kwenye chanzo cha mto wa Olasae linalotegemewa na wanyamapori pamoja na wanakijiji wa kijiji cha Soit Sambu , Arash,Ololosokwa na Kirtalo. Ujenzi huu umefanywa na kampuni ya OBC ndani ya mita 10 kutoka chanzo cha maji  kinyume cha sheria.
  3. Taarifa ya Mh. Waziri haikuzingatia suala la utawala bora wala sheria ya wanyama pori ya mwaka 2009 kifungu cha 16(5) ikinachomtaka kwamba hakuna ardhi ya kijiji itakayoingizwa ndani ya pori tengefu. Kipengele hiki kinasomeka kama ifuatavyo;  16(5) "For the Purposes of subsection (4), the Minister shall ensure that no land faIling under the village land is included in the game controlled areas."  Kipengele cha 16(6) "Subject to subsection (4), the Minister shall, in consultation with the relevant authorities, make regulations prescribing the manners in which sustainable management of game controlled areas shall be achieved."
Kutokana na maelezo yetu hapo juu sisi  mashirika ya hiari tunaitaka serikali kutekeleza yafuatayo;
  1. Serikali iache mara moja mpango wake wa kugawa ardhi ya wananchi kwa manufaa ya mwekezaji kwa kisingizio cha manufaa ya umma badala yake itambuwe ardhi yote ya Loliondo kama ardhi ya vijiji na kuwaachia vijiji kujipangia matumizi yao ya ardhi kwa njia shirikishi na mujibu wa sheria za ardhi.
  2. Kuacha mara moja kupotosha umma kwamba ardhi hiyo siyo ya vijiji na izingatie sheria kwa kuvipa vijiji haki yao ya kujiamulia mambo yao wenyewe kwa kutumia sheria zilizopo za ardhi na za serikali za mitaa.
  3. Serikali iweke bayana  kwa umma nia  yake ya kuchukua ardhi hii kwamba ni kwa ajili ya mwekezaji wa OBC badala ya kisingizio cha uhifadhi wa mazingira na sio vinginevyo.
  4. Serikali iache mara moja vitisho kwa wananchi wa Loliondo na wawakilishi wao, wanaharakati, mashirika na waandishi wa habari wanaofuatilia mgogoro huu. Serikali kuendelea kutishia makundi haya inakiuka haki ya kikatiba ya kupata habari na kuzuia jamii kuelimishwa juu ya haki zao za kikatiba na kisheria kwa manufaa yao wenyewe na taifa kwa ujumla. Kufanya hivyo ni kuwanyima haki yao ya kupata taarifa na kutoa maoni kama inavyolindwa na katiba ya Tanzania na mikataba ya Kimataifa ambayo serikali imeridhia.
  5. Serikali iache mara moja kudharau na kuingilia utendaji wa  mhimili wa mahakama kwa kuacha kuingilia suala la Loliondo kwa kuzingatia kuwa tayari kuna kesi ya kikatiba (MISC CIVIL CAUSE NO 15/2010) iliyofunguliwa katika mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha ambapo Waziri wa Maliasili  na Utalii na mwekezaji wa OBC ni miongoni mwa  wa walalamikiwa.
 
  1. Serikali iache mara moja visingizio kwamba mgogoro wa Loliondo unasababishwa na wanaharakati na mashirika ya nje kwani yenyewe inatambua uwepo wa mgogoro huo unasababishwa na maamuzi ya serikali ya kugawa ardhi ya wananchi bila kuwashirikisha kwa kuangalia upande mmoja wa manufaa kwa wawekezaji tu bila kuangalia athari kwa wananchi.
  2. Serikali iache matumizi mabaya ya  vyombo vya usalama hasa jeshi la polisi ambalo hutumiwa kuwaondoa wananchi katika makazi yao kwa nguvu huku wakisababisha athari kubwa kwa wasiojiweza, wanawake na watoto.
 
TAMKO HILI LIMETOLEWA LEO TAREHE 4 APRILI 2013 NA MASHIRIKA AMBAYO NI;
  1. PINGOs Forum
  2. Tanzania Land Alliance- TALA
  3. Haki Ardhi
  4. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu- LHRC
  5. Tanzania Human Rights Defenders
  6. Tanzania Gender Network Program (TGNP)
  7. Tanzania Natural Resource Forum –TNRF
  8. Cords
  9. Ujamaa Community Resource Team- CRT
  10. Pastoralists Women Council –PWC
  11. Ngorongoro NGOs Network –NGONET
  12. Tanzania Pastoralists Community Forum-TPCF
  13. OSEREMI
 
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment