RE: Tanzania nakulilia nani atakukomboa! Utaikomboa mwenyewe kwa kulinda raslimali zake, kutumia kwa kuangalia uwezo wa raslimali hizo sio kuzidi uwezo, kuwa mkweli, mchapa kazi, unayekubali kubadilika kulingana na wakati, uchumi na technolojia lakini bila ya kukiuka maadili ya mila na nchi; mpenda na mtenda haki, mwenye macho yanayoona pande zote kama kinyonga ili ujue jema na baya, kuuona na kuukubali ukweli, kuacha shutuma pande moja daima, kuwa mtu wa Mungu, kuona pande zote hizo kujua nani anafanya nini na nani wa kumuhusisha ambaye mtapanga malengo tekelezeki na ambayo yatafikia viashiria mlivyoweka. Jee-Upo tayari?
Madam Kiwasila nimeupenda ushairi huu ulio toa, kweli wahenga waliona mbali: Penye wengi haliharibiki neno. Nafikiri unawafaa wanamabadiliko wote.
Nakubaliana pia kua uwindaji-haramu unamadhara makubwa kuliko huu wa Leseni. Lakini ni bora vilevile kujiuliza kama taratibu za kupata leseni zinaweza kuwa rahisi kumwezesha masikini nae kupata kibali. Mahala pengine sheria zinakua ngumu kiasi kwamba masikini wanakua hawana tena namna zaidi ya kufanya illegal hunting. Hali inapokua hivyo matokeo yake matajiri, wageni na watu wanao kua well connected na idara husika ndio wanahodhi sector ya uwindaji na kufaidika zaidi. Pia kumbuka mara nyingi conservation burden inakua kwa masikini wanao foregone matumizi ya hizo rasilimali for the sake of conservation. Nafikiri hapo napo panatakiwa kuangaliwa. Au unasemaje madam?
Kuhusu hoja ya usikubali kila unaloambiwa na wananchi au mtu yoyote pande moja bila vidhibiti na kukaa nao kujadiliana na kupekua kiundani kukwepan kanyaboya. Pia nakubaliana nayo. Ila kwa kisa hiki cha mgogoro wa Ardhi Loliondo, angalia chini hapo NGOs 13 zimetoa tamko la pamoja. Kama wote wanatudanganya juu ya OBC basi tumekwisha. Najua pia kuna baadhi ya NGOs zinatumiwa vibaya na nchi za magharibi hivyo kuna haja ya kuzichunguza na kuona wanachofanya.
Kuhusu jamiii kufaidika: Naamini kua Maasai na wafugaji wengine wanafaidika na uhifadhi, maana nimesoma na watu waliokua wanafadhiliwa na NCAA. Pia najua kua hutoa chakula cha misaada hasa katika vijiji ambavyo vimezuiwa kufanya shughuli za kilimo.
Ninavyo waza juu ya hili:yamkini hicho tunachokiita faida ni tone ukilinganisha na kinacho vunwa kutokana na hizo rasilimali. Au kati ya hao wafugaji wenyewe wachache wakawa wanafaidi on expense of others. Hapo lazima migogoro itaendlea. Tukumbuke kua hata katika rasilimali kama za madini tunaambiwa nchi inafaidika.
Hapa swali moja la kujiuliza kama tunafaidika Why those areas are experiencing endlessness conflicts??
Hapo pia nakubaliana kua kuna haja ya kumtafuta NEUTRAL PERSON adadafue kilichochini ya carpet.
Madam Kiwasila sijaelewa juu ya hii swali lako: Tunaponunua Faru kutoka South Africa na kuwapeleka katika Zuu la Kuzalisha Faru na Mbwamwitu Mkomazi kwa Tony fitzjohn hao Faru wanakuwa nyani au ni Rhino mnyama Pori ? Sasa, kama tunanunua toka S.A wanapanda meli au ndege-kwa nini nasi tusiuze na ruhusa za kuuza mnyama nlive zipo katika hifadhi za wanyama pori duniani? Ndio maana nchi nyingine hazina wanyama zinanunua na kuweka Zoo nchini kwao. wengine wananunua wanyama kwa utafiti wa madawa ya wanyama na binadamu ingawanye wanaharakati wa haki za wanyama huleta utata
Je! ulikua unajibu hoja ya wanyama waliobebwa na ndege ya jeshi la Qatar nililo tolea mfano?? Kama serikkali iliwauza kwanini wasituambie waliwauza ili watu wasiichukie serikali yao bure jamani?
From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, April 4, 2013 7:22 PM
Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA NGOS KUHUSU MGOGORO WA ARDHI WA LOLIONDO
Kijana chunga lugha yako au tutakung'oa kucha na meno!! Lakini ukisoma magazeti utaona wanatangaza uvunaji wanyama eneo fulani ambapo wanaonyesha na bei yake. kama wewe mwindaji una lesseni na bundiki yenye leseni au kuandikishwa miliki yake-unakwenda kuua mbogo, swala, ngiri, nguruwe mwitu etc baada ya kulilpia bei ya mnyama. Kila mnyama ana hesabu yake-bei na idadi yake ya kupunguzwa kwa mwaka. wapo pia wawindaji haramu wanauza nyama daily. utaona gari kando ya mbuga ya hifadhi (N.Park, Game Reserve, Game Conservation Area) mbovu imeharibika na tairi zimetolewa jamaa wanajifanya wanatengeneza. Kumbe wanasubiri ishara, wafunge tairi, jamaa walete na kupakia mzigo kukiwa shwari waondoke. bado hao wawindaji wasio kibali (haram) ambao hutimia mikuki, mishale ya sumu na mashimo ya kuchimba msituni ndani wakaweka mtego fyatuka na mnje wakaweka nyasi kama vile hakuna shimo. kama umepotea njia-please usipite hovyo porini mpakani na vijiji vilivyozunguka hifadhi-itakula kwako. Ukitumbukia ndani ya mashimo hayo, mtego utafyatuka unakunasa na kukukua. Mashimo ni mbinu ya uwindaji haramu. daima sindikizwa na wanavijiji ktk tembea na tafiti zako za Transect walk watakuambia-huko usipite-kubaya. wanyama wawindwao na sisi kiwizi bila leseni ni wengi sana sana kwa idadi. Kama kuna watu ambao hawawezi kulala kupata usingizi bila ya kula nyama pori-Wavidunda, Wasagala ni wamojawapo. Wengine kama Waikoma wa serengeti nyamapori ni sehemu ya Kirago. Ni wanyama wangapi kwa mwaka ukilinganisha na wale wa leseni? Si kwamba natetea wavunao kwa leseni (ambao anaweza akaandikiwa na kulipia 10 akavuna 30) bado mimi naona uwindaji-haramu unamadhara mpaka ya mnyama kupata kilema akijinasua mtegoni na kuondoka na mguu mbovu. Usikubali kila unaloambiwa na wananchi au mtu yoyote pande moja bila vidhibiti na kukaa nao kujadiliana na kupekua kiundani kukwepan kanyaboya. Hapa nitataja Kisa cha Kijiji kimojawapo cha jirani au karibu na Mji wa Mugumu-Serengeti. Kisa:- Serikali ililaumiwa mpaka tukapata Kizunguzungu. Jamaa akaonyesha mkono wenye makovu ya ajabu akasema alipigwa na game scout kwa kuonewa (Wa National Park wakitembelea Game conservation area jirani na kijiji hicho), amechanywa na kisu na hayo ndio makovu ya matokeo ya uonevu. Tuliandika haraka peni zikatembea ilivyo. Kumbe mwongo. Tukapiga picha na kuchukua maelezo. Lakini katika kusoma dalili za macho na kope za watu nikaona kuna zaidi baadae nikawafuata walionipiga UKOPE na nikaomba kunisindikiza kutembelea mazingira ya uchimbaji wa mawe ya rangi eneo hilo. Wakasema kuniambia huyo ni juangiri kuu hapa kijijini. Alikuwa anawinda akaangukia mshale wake wa Sumu ikabidi akate nyaman kabla sumu haijamuingia na anti-poison alikuwa kaifunga mbali. Sisi kwetu ingekuwa taarifa ya UONEVU na kudhuru mwili kumbe ilikuwa-kanyaboya. Tukawauliza viongozi wa kijiji wakathibitisha na mengine mengi. Kijijini tukapiga mapicha kibao ya nyama pori zilizoanikwa ili kutetea haki ya kupata nyama-kumbe ulikuwa uwindaji haram. Alexandar nisikupotezee muda na wa wengine. Bado hizo takwimu za hela toka NCAA, Tanapa, Hotels na huyo Mohamed Ali-Ali-OBC mahesabu unaweza ukayapata. Shukrani ya mwindaji wa Loliondo ilikuwa kubwa Halmashauri ya Wilaya tu jinsi anavyotoa mafao, kujenga airport na mengine mengi niliyataja huko nyuma. Anyway-Hakuna Kizuri 100% duniani. Hata zile za NCAA kama mafao ya kufaidika kwa wananchi ndani ya NCAA kwenda kwa Pastoral Council-Vijiji-mamilioni. Ulizia kutumika kwake upate na Kizunguzuru uone na mahindi mabovu yaliyonunuliwa badala ya mazima. Vitu hivi vya ufisadi hata ngazi ya chini ya mtu kutetea jamaa zake kwa wapenda maendeleo vinatutia wazimu. Fahamu hizi ni kazi ambazo wasomi hutumwa na GVT kama neutral people from academic institutions wenye uzoefu na kazi za jamii kuisaidia assessment na upangaji miradi au Evaluation fulani. Zinakusanya mpaka copy ya cheque hotel ilizotoa kupeleka halmashauri na kuuliza hela zilivyotiumika na vijiji pia walioipata toka halmashauri au miradi iliyohisaniwa na mafao mengine-scholarships kusomesha watoto kaya hadi kaya etc. Zipo NGO zinazopenda maendeleo ya wananchi na zipo za 'Tumboni Street'. Wapige kelele waonekane ndio wapate uhisani na huko Loliondo ndio zimejaa NGO kila kona na humo NCAA kwa jamii. Wapo NGO wapendao haki na kuitetea kimamilifu na wanawajibika grassroots. Na wapo kama hao wa kuhamasisha nchi isitawalike mpaka damu imwagike. Na huwezi kuona maendeleo yakawa ya mfano hapo walipo pamoja na raslimali kuwepo na misaada iliyoletwa na wakifanyiwa auditing inakuwa utata kuonyesha zilivyotumika. Na pamoja na kutetea haki na Demokrasia, viongozi wengine ni viongozi wa kudumu hawaachii ngazi maana ni ulaji. Toka kiundwe yeye ni director mpaka dunia iishe.Jiulize!! Nitasaka auditing report mojawapo ya 1997 ya fund mojawapo toka UK niliipata kwa siri huko UK na waliazimia kutokuwapa hela NGO hizo kutokana nan ufisadi. Chipalazya nikumbushe niisake nikuvurumishie. Nikuulize Kijana mwanaharakati-Tunaponunua Faru kutoka South Africa na kuwapeleka katika Zuu la Kuzalisha Faru na Mbwamwitu Mkomazi kwa Tony fitzjohn hao Faru wanakuwa nyani au ni Rhino mnyama Pori? Tumemaliza mbwa mwitu kwa kuwaua kwa sumu. Mbwa mwitu ni mnyama muhimu katika kurekebisha wingi wa wanyama wabaya wala watu. Mbwa mwitu wanakuja kwa ndege-Jee tunakuwa tumeleta panya buku au wanyamapori toka mbuga za wenyetu tumenunua? Nilisoma gazetini kuna Faru aliitwa jina la Mhemshimiwa-Kikwete. Hata wale Faru wa Kenya waliokuwa na bodu guard watano Faru mmoja wameuawa na majangiri. Sasa, kama tunanunua toka S.A wanapanda meli au ndege-kwa nini nasi tusiuze na ruhusa za kuuza mnyama nlive zipo katika hifadhi za wanyama pori duniani? Ndio maana nchi nyingine hazina wanyama zinanunua na kuweka Zoo nchini kwao. wengine wananunua wanyama kwa utafiti wa madawa ya wanyama na binadamu ingawanye wanaharakati wa haki za wanyama huleta utata. Usije ukashangaa ukatembea hovyo Uk, au USA ukaliwa na Simba aliyetoroka kwenye Zoo au ukakumbatiwa na gorilla barabarani kama ilivyotokea hivi majuzi ulaya. wanyama hawa wananunuliwa nchimbalimbali kulinganisha na harvesting quotas za live animals. wanaojua sheria za wanyama pori mauzo ya live animals na ya uwindaji watatujuza. -Pamoja na matatizo mengine-kumbuka ile case ya wasomali kutamba Loliondo kukaa ktk maboma huko na ugomvi uliotokea baadae kufa police kamanda Soitsambu katika mapambano baada ya marriage of convenience kuisha na serikali kupata taarifa. Kuna kilimo kikubwa sana tulikikuta baadhi ya vijiji na wanalima kwa plough za ng'ombe na unaona wanyama pori pembeni na mifugo ktka mabanda solid ya mbao ya mloliondo huko engerosambu, baadhi ya maeneo ya soitsambu. Kuna maeneo utaonyeshwa mpaka makazi ya wageni ila watakuambia (usinitaje kama ndiye niliyokuonyesha). Wageni Tanzania wapo Mikoa yote tunawakaribisha wenyewe. Kuna hatua viongozi/madiwani wa makabila ya wafugaji wamechukua kuondoa ukaukaji wa vyanzo vya maji maeneo ya wanyama pori NCAA na Loliondo pia vijiji vya Tarangire -Simanjiro kwa wafugaji kwa kudhibiti ukiukwaji hata wa Mila na bado wana matatizo. Olbalbal-NCA ni mahala pamoja wapo Diwani alifanya kazi kubwa. Niliwekaga mapicha humu huko nyuma ya Loiborsirret-Tarangire na degradation ya mto na ardhi. Si Loliondo tu kuwa tatizo. Hata ukienda Terrat kwa wafugaji ambapo ndio makao makuu ya NGO ya wafugaji, pana na radio station, kituo kikubwa-Mto terrat chanzo chake cha maji na mto umekuwa degraded. Mifugo na wanyama pori inapata tabu. Conservation biology imeshatupa maone kuwa wanyama pori wengi wapo jirani na makazi na maelezo yake mengi. Hili la wanyama kuwa karibu na watu si hadithi ya leo, kuna sababu zake nyingi pamoja na kuwa na Mosaic ya vegetation za lishe kwa kuwa binadamu anafanya modification na environment kwa kulima, kuchoma moto etc. Na ndio maana mbvuga hufanya controlled bushfire ili kuwapa lishe wanyama. Wanasayansi wa wildlife na conservation biology wakakutan Bali-Indonesia 1982 na maeneo mengine baadae na kukubaliana masuala ya 'Conservation with Development' (as part of benefit sharing); kuwe na benefit sharing kwa walindao wanyama na wanaoathirika na wanyama na misitu au mradi wowote ule wa conservation. Na ndio kuna concept ta Particiaptory Forest management, CBNRM, Wildlife Management Areas (WMAs). Ukitaka kujua hasa wananchi wanafaidikaje na NCAA, Serengeti national park, Loliondo na OBC please toa tender, tafuta neutral organizations, zikapekue mafao yaliyotolewa na evidence zake halafu ndio uanze kulaumu. Kweli Benefit sharing muhimu, kushirikisha wananchi ndio wimbo na sala ya maendeleo. basi yarekebishwe pale yalipokosewa tusije tukaingia vitani na tunazuia utalii usituingizie mapato. Umefika wakati sasa NGO kuunda Tanzania NGo volunteer Services yenye wataalamu mbali mbali ktk sekta mbali mbali ili kutoa ajira kwa wasomi vijana waende vijijini kusaidia upangai na utekelezaji maendelea ili tupunguze lelemama. usishangae-mharibifu na muhujumu naye hulalama. Hata atupaye takataka ndani ya mtaro zikakwama na kutoacha tabia ya uchafu, maji yakishindwa kupita yakafurika ndani ya nyumba akapoteza mali na uhai wa familia yake-hulalama kuwa serikali haimjali-sembuse kwenye ardhi kama mali asili ulinzi na matumizi yake hakutokosa lawama, kulaumiana na ulalamishi. Tanzania nakulilia nani atakukomboa! Utaikomboa mwenyewe kwa kulinda raslimali zake, kutumia kwa kuangalia uwezo wa raslimali hizo sio kuzidi uwezo, kuwa mkweli, mchapa kazi, unayekubali kubadilika kulingana na wakati, uchumi na technolojia lakini bila ya kukiuka maadili ya mila na nchi; mpenda na mtenda haki, mwenye macho yanayoona pande zote kama kinyonga ili ujue jema na baya, kuuona na kuukubali ukweli, kuacha shutuma pande moja daima, kuwa mtu wa Mungu, kuona pande zote hizo kujua nani anafanya nini na nani wa kumuhusisha ambaye mtapanga malengo tekelezeki na ambayo yatafikia viashiria mlivyoweka. Jee-Upo tayari? Mungu ibariki Tanzania. --- On Thu, 4/4/13, alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com> wrote:
|
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment