Tuesday 9 April 2013

Re: [wanabidii] TAMKO LA JUKWAA LA WAKRISTO MKOA WA MBEYA KUHUSU VURUGU ZA KIDINI NCHINI

Marcus,
Wewe ni Mtanzania kweli na unajua kinachoendelea hapa nchini?
Unajenga hoja lemavu mno.





Walewale.



From: marcus kabwella <marcuskabwella@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, April 9, 2013 2:44 PM
Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA JUKWAA LA WAKRISTO MKOA WA MBEYA KUHUSU VURUGU ZA KIDINI NCHINI

Swala la kuwaachia waislam wachinje, lilikuwa ni kwa hiyari kwa wakristo kwani wakati huotuliishi nakuchukuliana kama ndugu na wao kwa kuwa dini yao hawastahili kula kilichochinjwana mwingine tukaona isiwe taabu kwani Bismillah haipunguzii maumivu achinjwae! Siku za karibuni kwa kutumiaudhaifu wa umaskini wa akili wa baadhi ya waamini, kukatokea kundi la watu wakitaka kuwaamsha waislam kwa madai eti wameonewa siku nyingi na kutawaliwa na wakristo!
 
Jambo ambalo walikuwa wakisema wakristu wanapendelewa kwenye elimu, na ajira na kuwaona maeneo ya makanisa kuna maendeleo zaidi ya misikitini, jambo ambalo ninalipinga kwa nguvu zote.  Nikianza na elimu wakristu hasa wakatoliki ndiyo walipasa kulalamika maana shule zao nyingi ndo zilitaifishwa na serikali kwa lengo kila mmoja asome maana waislamu walikataza watoto wao kusoma huko kwa hofu ya kulishwa najisi na nyamafu. Lakini baada ya hapo wakristu hawakuchoka waliendelea kuhimiza watoto kwenda shule na kujenga shule nyingine na kuziwekea waalimu wazuri na wakutosha na vifaa vya kila aina na kuendelea kufanya vizuri. Kama haitoshi shule hizo bado zinachukua wanafunzi wa dini zoote mfano shule zinazoongoza nchini Marian girls ya Bagamoyo na ile ya Mtakatifu Francis ya Mbeya wanapokea kila aina ya mwanafunzi bila kujali dini wala dhehebu, Kama haitoshi Mariani wakati ilipoanzishwa Padre Bayo alipita mitaani kule Bagamoyo kuwaomba watoto waje kusoma kwa gharama ndogo lakini wenyeji wengi walikataa na akalazimika kutoka nje ya wilaya baadae kuona inaongoza eti wakaandamana kutaka kuichoma moto kwa madai eti kwa nini shule inayofanya vizuri iwepo wilayani mwao na wanafunzi watoke nje?
 
Serikali hii ndiyo iliyotaifisha hospitali na mpaka leo kuna wilaya wanategemea hospitali za makanisa kwa kuongezea tuhela kidogo na kuziita teule.
Mimi ninaamini kuna waislamu wengi ni waelewa na hata wao hawapendi matukio haya.
 
Leo hii Makanisa yana vyuo vikuu vyao wamevijenga na kuanzisha kwa gharama zao, Isipokuwa Mt. Yohana cha Dodoma (Anglican) na Sebastiani Kolowa (Lushoto) Ambapo serikali kwa hiari iliamua kuwarudishia Makanisa hayo shule ilizokuwa imezitaifisha Yaani Mazengo na Magamba. Lakini ndugu zangu waislam mna chuo cha kiislam ambacho kilikuwa chuo cha TANESCO mali ya umma Rais mstaafu Benjamini william Mkapa ambae ni mkristo alitoa majengo hay yaliyokuwa yamekamilika kila kitu na kuwapa mfanye chuo kikuu cha KIISLAM leo hii mnapolalamika mnaonewa mnatenda haki kweli mbele ya mwenyezi Mungu? Kwa mfano leo hii serikali ikiamua kurudisha shulena hospital zote iliyozitaifisha ndugu zangu mtarudishiwa shule na hospital ipi? (nitajie walau mbili tu maana Tnzania ni kubwa kwinginekosijafika)
 
Nawaomba wakristu kama suala la kuchinja litatufanya tugawanyike na damu imwagike tuseme hapana! tuwaache wachinje na nyama tule maana hata ukichinja mwenyewe kitoweo hicho mwishowake ni chooni. wala hakina mahusiano ya kufika mbinguni. Kama tutachinja huku tukiuwana, kudhulumiana na kuoneana wivu hatutafika mbinguni ng'o hata kama tutalala makanisani.
 
Watanzania wenzangu wenye mapenzi mema wakristo kwa waislam na wasio na dini napinga kwa nguvu zote kauli ya serikali eti tuvumiliane sio sahihi tuna wajibu wa kupendana na sio kuvumiliana. Kuvumiliana maana yake Mauwaji na vitendo vya kidhalimu viendelee na wale wanaofanyiwa hivyo wakae kimya, wapendwa imetulia hiyo?
 
Wanaotaka kutuchonganisha kwa makabila,udini,uitikadi hata usimba na uyanga kwa kubaguana na hata kumwaga damu hao ni watu wakuwaogopa hasa watu wa dini wafahamu kwamba kuutoa uhai wa mtu ni kwenda kinyume zaidi na malengo ya Mungumaana ndiye muumbaji.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

From: paul lawala <pasamila292000@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Tuesday, February 19, 2013 3:58 PM
Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA JUKWAA LA WAKRISTO MKOA WA MBEYA KUHUSU VURUGU ZA KIDINI NCHINI

Aise
 
Kumbe tamko la tangu mwezi wa 12 mwaka jana?

2013/2/19 Jane Mwakalukwa <mwakalukwa@gmail.com>
TANZANIA CHRISTIAN FORUM (TCF) MKOA WA MBEYA

TAMKO RASMI KUTOKA KTK JUKWAA LA WAKRISTO MKOA WA MBEYA

MHESHIMIWA NDG. ABAS KANDORO,

KAMA MKUU WA MKOA NA MWAKILISHI WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE MKOA WA MBEYA, TUNAPENDA KUSOMA MBELE YAKO TAMKO RASMI LA JUKWAA LA WAKRISTO MKOA WA MBEYA (TCF).
NDUGU MKUU WA MKOA,

            "HAKI HUINUA TAIFA BALI DHAMBI NI AIBU YA WATU WOWOTE" (Mit. 14:34).

Katika mkutano wa jukwaa la Wakristo Tanzania mkoa wa mbeya ulionyika tarehe 12/02/2013 Jijini Mbeya, wajumbe tulitafakari kwa undani juu ya hali inayoendelea kujitokeza katika nchi yetu na hasa katika mahusiano baina ya dini mbili kuu UKRISTO NA UISLAMU.

Jukwaa hilo lilijumuisha taasisi zake kuu (yaani mabaraza ya Madhehebu ya Kikristo) Tanzania Episcopal Council (TEC), Christian Council of Tanzania (CCT) na Pentecostal Council of Tanzania (PCT). Mbali na mambo yake ya kawaida jukwaa hilo lilitafakari utekelezaji wa Serikali juu ya tamko Rasmi la jukwaa la Wakristo kitaifa lililotolewa tarehe 06/12/2012 na kusomwa katika makanisa yote ya Kikristo nchini kwenye sikukuu ya Krismas tarehe 25/12/2012. Katika tafakari letu jukwaa la Wakristo wa Mkoa wa Mbeya tumeona kuwa kunabaadhi ya mienendo inayojitokeza katika nchi yetu ambayo kama isipodhibitiwa na kukomeshwa na Serikali italeta athali kubwa na hata kuondoa amani na uthabiti (Stability) wan chi.

Katika kutafakari kwa jukwaa juu ya athari zinazoweza kujitokeza, kumekuwepo na mambo yanayotendeka waziwazi yenye athri kubwa kwa amani na usitawi wan chi na wanchi wake kwa ujumla. Kwa mfano, uchochezi, kashfa, matusi na 
uchokozi wa wazi unaofanywa na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu kupitia vyombo vya habari vya kidini (rediona magazeti), mihadhara, kanda za video, CD na DVD pamoja na kauli zinazotolewa na viongozi wa dini hiyo kwenye baadhi ya nyumba zao za ibada(ushahidi upo kama vile uhamasishaji wa Sheikh Ilunga) pasipo serikali kuchukua hatua stahiki na badala yake kubaki kimya au kupambana na wanaofichua harakati hatarishi kwa utulivuwa nchi.

Miongoni mwa harakati hatarishi zinazosambazwa kwa njia ya CD na DVD za Sheikh Ilunga, kuhusu kuua Wachungaji, Mapadri na Maaskofu zimeanza kuwa matokeo mabaya; kwani Padri kule Zanzibar alipigwa risasi na watu walioitwa na serikali wahuni na sasa kifo

Kimetokea na mchungaji Mathayo Kachila kule Buselesele Mkoani Geita na kikundi kinacho dhaminiwa ni wanaharakati hao wa kiislamu wenye jazba na gadhabu kali inayotokana na mvutano uliopo kati ya wakristo na waislamu kuhusu nani mwenye haki kisheria KUCHINJA WANYAMA. Hatua zinazochukuliwa na Serikali hazilizishi wala kukidhi matakwa ya wananchi wapenda amani. Tuna mifano kadhaa ya matukio kama haya yaliyojitokeza kwa wanchi wenzetu moja ni ile ya wenzetu aliyepigwa risasi kule Rungwe Ndg. John Mwankenja (Mwenyekiti wa CCM Rungwe) aliyepigwa risasi kwa mambo yanayodhaniwa kuwa ni ya kisiasa) Serikali ichukuwe hatua madhubuti kwa kutuma wachunguzi kutoka Dar es salaam kwa swala hilo na wote tuliridhika kwa hatua hizo madhubuti. Hatua kama hizo mbona hazichukuliwi katika masuala haya ya kidini na badala yake Serikali inakaa kimya au ina chukua hatua ambazo kimsingi hazitatui tatizo ili wananchi waridhike na Seeikali yao? Je tuseme Serikali inaangalia haiba (Personality) za watu au aina ya vikundi? Swala la uchinjaji lilipo jitokeza kule Mwanza waziri wan chi ndg. Steven Wasira alienda na kutoa majibu mepesi katika swala zito je, tuseme aliyoyatamka huko yalikuwa ni KAULI YA SERIKALI au kauli yake mwenyewe? Na kama yake mwenyewe mbona Serikali haijakanusha waziwazi? Na kama ni kauli ya serikali hiyo haki ya kuchinja kwa waislamu inatokana na sheria zipi za nchi? Je huo ndio utawala wa sheria tuliyoahidiwa na serikali ya awamu ya nne kuwa itatenda kazi kwa kuzingatia utawala wa sheria.

Kupigwa risasi kwa Pdri na kuuwawa kwa mchungaji kunathibitisha hazma halamu na batili ya "Ua, chinja" mapadri, wachungaji na maaskofu iwe kwa siri au kwa wazi iliyohasisiwa na Sheikh Ilunga ambayo sio tu inahatarisha amani ya nchi lakini pia inavunja haki za kuishi za binadamu zilizoainishwa katika katiba ya serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Aidha harakati hizi ziana muelekeo wa kudhoofisha ukristo Tanzania kama sio kuumaliza kabisa. Pamoja na mambo mengine kinachosikitisha ni namna ambavyo serikali inavyoyashughulikia mambo mazito yanayotikisa amani na utulivu wan chi. Utasikia mala ikisema "Mtu haruhusiwi kujichukulia sheria mkononi" na ndipo kikundi Fulani kitaibuaka na kuvunja mabucha na kuchoma nyama iliyomo humo hapo tena utasikia serikali hiyohiyo ikitowa kauli kwamba "Mvumiliane" je tunakwenda wapi?

Kwa misingi hiyo kwanini tusite kusema kwamba serikali ya chama cha mapinduzi (CCM) inaibeba dini ya kiislamu? Kwakuwa jukumu la serikali ya chama cha mapinduzi ni kuhakikisha kuwa wananchi wote wa Tanzania bila kujali dini zao, makabila yao na hata rangi zao wanaishi katika misingi ya uhuru, haki, udugu na amani kama raisin a watendaji wake walivyotoa kiapo mara baada ya kupewa dhamana ya kuiongoza nchi na wananchi wake kwa ujumla pasipo na ubaguzi wowote.

HITIMISHO: Ili wakristo wote nchini warudishe imani yao kwa serikali ya chama cha mapinduzi mambo ya fuatayo ni lazima yachukuliwe hatua za haraka iwezekanavyo: 

Tunataka Serikali izingatie utawala washeria kulingana na ahadi yake katika kushughulikia maswala ya kijamii na sio vinginevyo. Kwa kuzingatia sheria maswala ya imani na dini yapo wazi kabisa kama zilivyoanishwa kwenye katiba ibara ya 19 (1), (2) (3) (4)  na kufanya vinginevyo ni uvunjifu wa sheria.
Swala la kuua lisichukuliwe kama mazoea ya kawaida na inapotokea popote ni lazima Serikali ichukuwe hatua inayostahiki kwa kuzingatia utawala wa sheria kwakuwa wote wako sawa mbele ya sheria ibara ya 12, 13 (1) –(5).Usawa huo ni lazima uonekane katika swala la mauaji ya Mchungaji Mathayo Kachila na kama hatua zilivyochukuliwa katika mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri na mwenyekiti ya CCM Wilaya ya Rungwe Ndg. John A. Mwankenja. Hiyo ni haki ya msingi kkwa kila mtantania bila kuangali haiba (Personality) yake kama katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania inavyoainisha haki xza kuishi, kulindwa na kushughuklikiwa kisheria katika ibara ya 14 na 15 pamoja na vifungu vyake viwili vidogo.
Tunataka Serikali itueleze ni ushahidi gain zaidi inayoutaka kuliko ule unaopatikana kwenye CD na DVD zilizotolewa na Sheikh Ilunga kama inazingatia utawala utawala wa sheria.
Tunataka Serikali iwajibike kutolea ufafanuzi kauli ya waziri wan chi Ndg. Steven Wasira inayohusu haki ya kuchicha kwa waislamu kama inatokana na sheria gain ya nchi?
Kama Serikali inatekeleza utawala wa sheria, tunataka wakristo tuwe na machinjio na bucha zetu kulingana na imani yetu.
Kama Serikali haitachukuwa hatua za makusudi katika kutekeleza madai yetu sisi kama viongovi wa dini ya kikristo tutachukua hatua ya kuwaambia waumini wetu kwamba Serikali ya chama cha mapinduzi inaibeba dini ya kiislamu na wao watajua la kufanya.

Pamoja na kutaka utekelezaji wa haraka kutoka kwa Serikali bado tunawaomba wakristo tuwe katika hali ya maombi na utulivu kwa wakati huu ambapo tumo katika vita vya kiroho ili Mungu akatuimarishie amani ambayo ni nguzo kuu ya Taifa letu. Tamko hili rasmi la jukwaa la wakristo Mbeya lisomwe katika makanisa yetu yote siku ya juma pili tarehe 24/02/2013.

Tunakuambatanishia na nakala ya Tamko Rasmi la TCF Taifa la tarehe 6/12/2012.

NDUGU MKUU WA MKOA NAWASILISHA.

Nakala kwa:
Mwenyekiti wa CCM Mkoa.
Tanzania Christian Furum Taifa
Mwenyekiti wa the Tanganyika Law Society.
Vyombo vya habari TV, Redio na magazeti


--
Jobs in Africa - http://www.wejobs.blogspot.com/
International Jobs - http://www.jobsunited.blogspot.com/
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
mailto:wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mailto:wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 


0 comments:

Post a Comment