Friday 12 April 2013

Re: [wanabidii] SUALA LA KUCHINJA-MWINYI AKATA MZIZI WA FITINA- ASTAHILI PONGEZI

Nashindwa kuelewa kwanini wachangiaji wengine wamejaa hisia za udini mwanzo mwisho!? Inakera mno wala si uongo comrade Matinyi.
Moses Gasana

Sent from my iPhone

On Apr 13, 2013, at 12:06 AM, Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com> wrote:

Unajua vizuri sana kwa nini huielewi!
 

Date: Fri, 12 Apr 2013 10:07:37 -0700
From: abachamani@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] SUALA LA KUCHINJA-MWINYI AKATA MZIZI WA FITINA- ASTAHILI PONGEZI
To: wanabidii@googlegroups.com

Matinyi,
Sina chenga yoyote ndugu yangu.Nadhani umesema zaidi ya hilo ila hiyo mifano unayoitoa ndiyo siielewi.





Walewale.



From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Friday, April 12, 2013 7:56 PM
Subject: RE: [wanabidii] SUALA LA KUCHINJA-MWINYI AKATA MZIZI WA FITINA- ASTAHILI PONGEZI

Amour,
 
Usipige chenga, ujumbe wangu ni rahisi tu: Acha kuona na kufikiria kila jambo kwa macho na mawazo ya udini udini udini udini udini udini udini udini udini.
 
Watanzania ni WATANZANIA - hayo ya dini ni ziada tu na hayana sababu ya kuingilia UTANZANIA wetu.
 
Matinyi.
 

Date: Fri, 12 Apr 2013 09:42:47 -0700
From: abachamani@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] SUALA LA KUCHINJA-MWINYI AKATA MZIZI WA FITINA- ASTAHILI PONGEZI
To: wanabidii@googlegroups.com

Matinyi,
Nimesoma maandishi yako mara tatu lakini sijakuelewa.Nitajaribu tena na kesho kusoma na kuuliza watu wengine.Ukweli sijakuelewa, kama una namna nyingine ya kunielekeza naomba.





Walewale.


From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Friday, April 12, 2013 5:07 PM
Subject: RE: [wanabidii] SUALA LA KUCHINJA-MWINYI AKATA MZIZI WA FITINA- ASTAHILI PONGEZI

Amour,
 
Nadhani wewe una tafsiri mbaya ya maana ya dini.
 
Pia, kwa ushauri wangu tu, usitumie udini kwenye kila jambo; mathalani, hoja inayoashiria kwamba Mkapa huwa halaumiwi na Wakristo haina maana tukiangalia ukweli wa mambo. Nadhani, kama ni lazima tufuate busara zako, na kisha tuangalie ni nani waliombana Mkapa, tutakuka wote ni Wakristo ingawa wewe utasema mengine kabisa. Pia, si kweli kwamba Waislamu hawambani JK labda kama unasema kwamba Lipumba si mwislamu. Na kama shida yako ni kuangalia dini tu, basi utaleta matatizo makubwa mno. Kimahesabu, iwapo kuna makundi makubwa mawili tu, ina maana uyumkini wa mtu wa kundi fulani kufanya kitu utazidi 1/4 na kuelekea kwenye 1/2; kwa hiyo kila ukitaka kuwabagua watu utapata sababu lakini kimsingi ni hali halisi ya mambo tu.
 
Lakini pia, si kweli kwamba yanayosemwa yapo? Mathalani, ni kweli kwamba Mwinyi alikuwa na tatizo la kuilinda katiba na ikavunjwa licha ya kuwa anasifiwa kwa mengine na watu wote tu, ingawa wewe utawaona waislamu tu. Je, Mkapa naye hakupata matatizo ya kashfa kibao? Alipata pia na alisemwa na watu wote.
 
Jifunze kuwaangalia Watanzania kama Watanzania na si kwa dini dini dini dini dini dini dini.
 
Inakera mno!
 
Matinyi.
 

Date: Thu, 11 Apr 2013 20:30:14 -0700
From: abachamani@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] SUALA LA KUCHINJA-MWINYI AKATA MZIZI WA FITINA- ASTAHILI PONGEZI
To: wanabidii@googlegroups.com

Selemani
Suala hapa ni Kikwete na serikali yake.Ndiyo maana juzi nilishangaa Mkapa akiwa Bukoba anasema wakati wa utawala wake misingi ya utaifa ilikuwa vizuri sana kana kwamba hajui Mauaji ya Mwembe Chai na Mwembe Togwa Zanzibar yalitokea lini.
Hajasema ujambazi,EPA ,Kuuza mashirika ya Umma,Kugawana nyumba za serikali,mikataba ya madini,mauaji kila mahala nk.Leo huyo naye ni msafi sana.
Huwa na sema Tanzania lolote kufanyika itakuwa ni ngumu na sababu ni hizi tofauti za dini zetu.Mtu akiwa dini yako hakosei hata kidogo lakini wa dini nyingine makosa yote yake.
Pengine tutafika lakini sijui wapi.
2015 akitangulizwa mwenzao wote watahama hata hiyo CHADEMA na kurudi nyumbani.Ndiyo maana huwa nasema ni chama cha msimu.
Wakati wa Mwinyi iliimbwa sana katiba kuvunjwa nasasa wakati wa Jakaya ni bahati nasibu ya ajabu hii.





Walewale.



From: Selemani Swalehe <semkiwas@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, April 11, 2013 10:53 AM
Subject: Re: [wanabidii] SUALA LA KUCHINJA-MWINYI AKATA MZIZI WA FITINA- ASTAHILI PONGEZI

Amour nilikuwa naongea na watu wa imani ile  asubuhi hii na wao wamekubali kuwa katika imani yao hakuna restriction katika kuchinja. Mtu yoyote miongoni mwao anaweza kuchinja mwanaume,mwanamke,mtoto na kadhalika. Bali ile imani nyingine kuna restrictions. Mwanamke hachinji wala mtoto wa kiume ambae haja balehe
 hachinji. Sasa wanashindwaje kuwavumilia wale ambao imani yao ina restriction juu ya jambo hili ili wote wale nyama kwa pamoja na mahusiano mazuri yaendelee? Wanataka kuvunja mahusiano mazuri hawa ni wakorofi. 
 
Suleiman Swalehe.
 
 
 
 
 
 
 
2013/4/11 amour chamani <abachamani@yahoo.com>
Selemani,
Usiogope malumbano.
Wanajua sana hao ila wana lao.





Walewale.



From: Selemani Swalehe <semkiwas@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, April 11, 2013 8:06 AM
Subject: Re: [wanabidii] SUALA LA KUCHINJA-MWINYI AKATA MZIZI WA FITINA- ASTAHILI PONGEZI

Mwinyi kaongea kama alivyoongea lakini hebu tutafakari kidogo na tuangalie mbele zaidi.  Mtu yoyote Akichinja  bila kufuata utaratibu wa kiimani hata angekuwa mwislamu, ina maana wale wanaofuata imani barabara kama inavyoelekeza kuhusu kuchinja hawatakuwa na imani na nyama yoyote inayozouzwa kwenye bucha lolote hadi wajue aliechinja nyama hiyo ni nani. Haitaishia hapo bali pia hatakula nyama ya hotelini au bar na kwingineko hadi  ajue aliechinja ni nani . Haitaishia hapo vile vile hatathubutu kula kwenye nyumba ya mtu wa imani tofauti na yake hadi ajue aliechinja nyama ho ni nani, na huo ndio mwanzo wa ubaguzi wa imani, ndio udini unafuata  na ukabila unafuata na ndio kuvujika kwa ushirikiano wa kiimani na kijmii na kuingia kwenye wakati mgumu ambao haujapata kushuhudiwa toka Tanzania iumbwe na Maulana. Hivi ni nani alielianzisha hili? Mbona tuliishi vizuri kwa ushirikiano kiasi kwamba tukikaa pamoja  mtu hawezi kujua huyu  imani gani na yule imani gani hadi mtu aulize. Sasa hakutakuwa na kuuliza tena  itaonekana wazi kuwa wao imani ile na sisi imani hii. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema,ubaguzi wa aina yoyote ile ni dhambi na dhambi yenyewe ni sawa na kula nyama ya mtu. Ukishakula utaendelea tu. Natoa angalizo sitaki malumbano.
 
Suleiman Swalehe
 
 
 
 
2013/4/10 Jovias Mwesiga <ngonzy@gmail.com>
Maslah yat taifa mbele si upuuzi. Mzee ruksa kaongea tena ngoja tuone

On 4/10/13, Josephat Isango <joseisango@yahoo.com> wrote:
> MWINYI AMEKATA MZIZI WA FITINA SUALA LA KUCHINJA, AMESEMA HAYO WAPI,
> AMEWAAMBIA AKINA NANI?  HATAKI LONGO LONGO AMENYOOSHA MANENO SOMA HAPA.
> Na Mwandishi wetu
> RAIS mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ally Hassan Mwinyi amesema kila mtu ana
> haki ya kuchinja kutokana na imani yake ilimradi tu asivunje sheria za nchi
> .
> Alisema anashangaa watu kugombania kitu kidogo kama cha kuchinja ilihali
> Tanzania ni nchi yenye  utamaduni wa kuwa na amani siku zote na kwamba kila
> mtu ana imani yake ya dini anayoiamini.
> Hayo aliyasema jana katika hoteli ya Kilimanjaro wakati wa kongamano  juu ya
> utamaduni wa kiislamu Afrika Mashariki        ambapo Tanzania imechaguliwa
> kuwa mwenyeji wa kongamano hilo .
>  "Imani ni nafsi ya mtu na haitakiwi mtu kumlazimisha kula nyama
> iliyochinjwa na mwenzio na kama unaona aliyochinja mwenzio ni kibudu basi
> usile chinja yako kula hata ukitaka kula  chura, mjusi konokono kula
> utakacho ruksa ilimradi tu usiingie katika jinai,"alisema Alhaji Mwinyi.
> Pia alisema majaribu kama hayo yaliwahi kumtokea katika miaka 80 wakati wa
> utawala wake lakini alijitahidi kuweka sawa kwa kumwambia kila mtu ale kile
> anachofikiri ni chakula bila kumlazimisha mwenzake ale anachokitaka yeye.
> Alisema watanzania wamezaliwa ardhi moja na kwamba kinachotakiwa ni kuwa na
> misingi ya kuvumiliana na kwamba sifa ya uislamu ni pamoja na kuwa na
> uvumilivu si kufanya vurugu kama inayotafsiriwa na makundi ya wanaotaka
> kuvunja amani ya nchi kwa kutumia jina la dini ya kiislamu.
> Pia alimshukuru Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ulimwengu wa Kiislamu Duniani
> (RABITA) Dk.Abdullah Mohsin Al-Turki  kwa kuichagua Tanzania katika kuhubiri
> amani pia.
> Wakati huo huo ,Waziri wa maji Profesa Jumanne Maghembe ambaye
> alimuwakilisha Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal amesema utamaduni wa kiislamu
> wa Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla ni kuvumiliana katika dini huku
> akitolea mfano wakati wa kumaliza kuswali ndio maana mtu anageuza shingo
> huku na kule.
> Pia aliwataka waislamu kujiendeleza katika elimu huku akieleza kuwa hata
> mtume alihamasisha hayo lakini waislamu wameshindwa kuyafuata.
> Akitolea mfano alisema waislamu wanachuo kimoja kikuu huku dhehebu moja la
> Lutherani wanavyuo vikuu 11 hivyo ni vyema wakaungana na kujenga vyuo kwa
> ajili ya kusaidia kuongeza wasomi kutoka katika taaluma mbalimbali.
> "Suala la elimu ya Dunia pia ni muhimu lakini mfano mzuri wa elimu kushuka
> ni katika mikoa ya pwani ambapo ndio ilipoanzia mwaka 1995 wanafunzi
> walioanza darasa la kwanza walikuwa 35,000 lakini walikuja kumaliza darasa
> la saba 9000 hapa inaonesha kua waislamu tunarudi nyuma badala kwenda
> mbele,"alisema Profesa Maghembe.
> Hata hivyo alisema kua suala la kuporomoka kwa elimu wakati mwingine wa
> kulaumiwa ni wazazi kwa kushindwa kuwasimamia watoto wao katika maadili ya
> taaluma na wazazi kushindwa kuwasimaia katika misingi ya dini zote.
> Dk.Abdullah Mohsin Al-Turki alisema katika nchi ya Saudia wanaishi watu
> tofauti tofauti lakini wakiwa katika upendo huku akisisitiza kikubwa ni

0 comments:

Post a Comment