Ni vurugu za kipuuzi. Huenda vijana wa kijiweni walianzisha vurugu ili wapate mafao ya kupora vitu. Nani atanizuia nisichinje nyumbani kwangu na nikala mwenyewe kiasi aje kunipiga au kunichomea mali zangu? katika familia zetu kuna watu wa madhehebu mbali mbali. kama mnafanya kikao cha ukoo wa watu hao dini mbalimbali-Muislamu anapewa kuchinja ili mle wote. Kama ninakula na familia yangu moja ya dini moja tunachinja wenyewe hata wakristu wanachinja na mwanamke (Mkristu) anachinja anakula na wanae au familia yake (wakristu). wapo wamama wanachinja kuku lakini sio mifugo mikubwa kama mbuzi, kondoo, ng'ombe. Wanawanjinja wao au watoto wao wa kiume na mchuzi hunoga. Zipo mila zinazozuia wamama na wadada kuchinja ila kijana hata awe mdogo std 1 atachinja kuku. Wanyama wakubwa wanahitaji uhodari amasivyo atakupiga pembe na kukuua hivyo watoto hao wadogo-hawaruhusiwi. Kama kifamilia walipochanganyika madhehebu ilianza hivyo na ikafika kitaifa kukubaliana hivyo kwamba Bucha za Umma mwislamu achinje leo tatizo ni nini? Kama wakristo wa madhehebu fulani wana bucha zao na wanataka kujichinjia-waacheni wakabe na kuchinja wanyama wao-si wanakula wenyewe hiyo Haram? Nao hao wa madhehebu mengine-Waislamu wana bucha zao-wachinje, wajiuzie, wale. labda liwe suala la kukosa wateja kama eneo waislamu ni 2% na waliobaki watachinja na kujiuzia na wenye bucha hasa na maduka makubwa ni Waislamu kipato kitashuka. Hawa na hasa huko Mbeya-wapeleke nyama nchi jirani wakause mbona ni utandawazi? Hapa hakuna hoja ila ni Kufirisika Kidini. unatafuta sababu ya kukupa sifa-mchongo duni ambao utakuangamiza mwenyewe. Au, kuna ulitakalo umekosa jinsi ya kuonekana unapitia mchongo huu wa KUCHINJA WANYAMA. ULAANIWE na radi ije kukupiga ufe usituletee balaa. Basi kuna waliozaa wakristu na waislamu hao watoto watachinjwa sasa wasiwepo duniani? Maana mmeunganisha damu mbli haram!! Wengine makanisa wanaanzisha yanazuka kama uyoga ambapo sasa kuanzisha makanisa imekua biashara huria. Mwenye misingi ya Kikristo hasa au kiislamu hasa-hawezi kuleta haya yanayotokea sasa kwa sababu-waafrika Tanzania tumechanganyikana kidini na kikabila. Tumechanganyikana Race na hata bunge lentu lina watu wa rangi mbali mbali waliozalia hapa bongo. Hata alikotoka babu Mhingi, Mwarabu, Mdachi, Gerumani, Mwingereza, Giriki baadhi yao hawajafika ni hiyo rangi na jina tu la ukoo na wanachaguliwa na wananchi wao kwa UPENDO. Leo kuchinja tu ikaewe sababu ya kuchomeana majumba na kuuana-Imeingia Siasa, Ufisaji, Kutaka Jina au kitu kingine humu. Moto unawasubiri Kiama. Hivi ukiua binadamu ndio Utauona Uwingu au Kuingia Mbiguni? kila alichoumba Mwenyezi Mungu kwa mkono wake ni chema-utakikataje Roho hasa akiwa Mwana Adamu? unaua, halafu ukipelekwa mahakamani hata ya kitaifa unakana unasema-hujaua. Jee, wewe unamjua Mungu kweli? halafu unaonekana unasali, unasujudu mbele za uwanja ulikochoma moto au kuua watu au mahakamani. ama huyu Mungu kujificha imekuwa Kheri maana angejitokeza sijui kama foleni ya kwenda kwake kumuhoji maswali magumu tulionayo ingekuwa na urefu gani daily. --- On Wed, 3/4/13, Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com> wrote:
|
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment