Tuesday 9 April 2013

Re: [wanabidii] Re: [Mabadiliko] Uchambuzi Wa Habari: Viboko Shuleni Au La, Ni Mjadala Wa Aibu!

Wiziri mwenyewe elimu yake inatiliwa mashaka na ilijidhihirisha kule Afrika Kusini alipotutia aibu ya mwaka!! Nashangaa bosi wake hajatambua kuwa hawezi kazi aliyompa, sasa anaanza kutoa maamuzi magumu ya kuendelea kutuharibia watoto/wajukuu badala ya kushughulikia matatizo makubwa yaliyoporomosha elimu nchi hii.

Sisi wengine tuliweza sana kielimu na kiheshima, bila kuchapwa viboko hata mara moja!! LKK

 


From: Augustine Rukoma <arukoma66@gmail.com>
To: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Cc: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Wednesday, April 10, 2013 7:03 AM
Subject: [wanabidii] Re: [Mabadiliko] Uchambuzi Wa Habari: Viboko Shuleni Au La, Ni Mjadala Wa Aibu!

"Ndio maana shule yangu ilikuwa inaongoza mkoa wa mbeya" st. Francis
inayoongoka kitaifa kila mwaka haiko mbeya? Kuna mtoto anachapwa
bakora pale? Nakubaliana na aliyesema yeye ndiye wa kulambwa bakola

On 4/9/13, Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:
> Ndugu zangu ,
>
> Moja ya habari kubwa leo ni hii;
>
> "Serikali imesema itarudisha adhabu ya viboko kwa wanafunzi shuleni ili
> kujenga nidhamu na kujituma.Akizungumza Dar es Salaam jana wakati akizindua
> tovuti ya www.shledirect.co.tz inayowezesha wanafunzi kujisomea kwa njia ya
> mtandao, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo ilisema
> kuondolewa kwa adhabu ya viboko shuleni kumewafanya wanafunzi wengi kukosa
> nidhamu na wakati mwingine kujifanyia mambo kienyeji.
>
> "Wasipotandikwa mambo hayaendi, nilipokuwa mwalimu mkuu nilikuwa
> nawatandika kweli ndiyo maana shule yangu ilikuwa ikiongoza Mkoa wa Mbeya
> hivihivi hawaendi..." alisema huku akishangiliwa na wageni waalikwa." (
> Mwananchi, Aprili 9, 2013)
>
> Nionavyo;
>
> Tunarudi nyuma miaka 50 badala ya kwenda mbele. Kuna wengi kama mimi
> tusioamini, kuwa, kumchapa mwanafunzi bakora ni kumsaidia kujenga nidhamu
> na kujituma.
>
> Kinyume chake, kama ni nidhamu, utamjengea nidhamu ya woga na kufanya yale
> ambayo anadhani unataka ayafanye na si kuwa ayafanye kwa faida yake na
> jamii hapo baadae.
>
> Viboko vinamfanya mwanafunzi asijiamini na hata akose uwezo wa kudadisi.
> Bado nakumbuka, kuwa nikiwa Darasa la Tano ilinitokea nikachapwa bakora
> darasani kwa kosa la ' kumdadisi sana mwalimu'. Mimi nilitaka kupata
> ufahamu zaidi lakini mwalimu aliniona nimekosa nidhamu.
>
> Habari hiyo ya kwenye Mwananchi inazungumzia mpango wa kurudisha sheria ya
> adhabu ya viboko wakati kimsingi watoto wetu wanachapwa viboko mashuleni
> kila kukicha.
>
> Wanafunzi kukosa nidhamu na kutokufanya vizuri kwenye masomo inachangiwa na
> mambo mengi. Tuanze kuyaangalia hayo kwanza kabla hatujawahamasisha walimu
> wakate bakora za miti ya mipera kuwachapa watoto wetu.
>
> Na kwa Waziri mwenye dhamana kuonyesha kushabikia watoto kuchapwa bakora si
> kitu kingine bali ni jambo la kusikitisha sana. Na mjadala wa kama watoto
> tuwachape bakora au la, katika wakati tulio nao, ni mjadala wa aibu- A
> shameful debate!
>
> Maggid Mjengwa,
>
> Iringa.
>
> 0788 111 765
> http://mjengwablog.co.tz/<http://www.facebook.com/l.php?u=http%3A%2F%2Fmjengwablog.co.tz%2F&h=YAQH9aSj_&s=1>
>
> --
> Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
> Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda;
> mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
> Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
>
> TEMBELEA Facebook yetu:
>  http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
>
> For more options, visit this group at:
> http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
>
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Mabadiliko Forums" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>
>

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.




0 comments:

Post a Comment