Kiwasila,
Nakuhakikishia kila mbunge akiambiwa atengeneze plan yake ya maendeleo na aitekeleze wengi hawataoneka. Pamoja na pendekezo hilo zuri kabisa nami napendekeza mishahara ipunguzwe. Walipwe kama watu wengine; na hapo tutapata wabunge wa kweli wenye nia ya kutetea wananchi na sio tumboni street (kama unavyo eleza daima hapa jukwani).
Pia itasaidia watu kubakia kwenye taaluma zao na wao waishauri nchi kwenye field husika. Hatutaona ma Dr. na Ma professor wakikimbilia ubunge. Inashangaza sana sasa hivi mtu akipandishwa cheo mfano akapewa ukuu wa wilaya, mkoa au uwaziri watu wanampongeza, maana kwao kapata ulaji na sio kumenyeka kwa ajili ya jamii husika.
Pia kuna haja kukawa na kigezo maalumu cha elimu kwa mbunge. Tukumbuke kua kuisimamia serikali na kutunga sheria sio kazi nyepesi inahitaji uelewa wa mambo mengi amabayo tunaamini mtu aliesoma anakua nao ukilinganisha na mtu ambae hakubahatika kupata hiyo nafasi. Hii itasaidi kupunguza wabunge wanao ingia bungeni kisa wanajua kupiga domo kaya.
Hapa majuzi tumemsikia Madam Makinda alipokua akichangia kwenye Katiba mpya kua tuwe na mabunge mawil; la SENETI na la kawaida. Sababu aliyotoa ni kua wabubge wengi hawana uelewa mkubwa juu ya mambo mengi. Hivyo kushindwa kuchambua mambo vizuri kwa faida ya nchi. Mimi napendekeza ni bora kua na bunge moja ila lenye nguvu, watu wachache lakini makini. Kuliko kua na lundo la wabunge wasiojua hata ni kwa nini wapo bungeni. Ndio maana tunaishia kuona taarabu na wengine wakiwa wana sinzia.
Alexander
From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Friday, April 19, 2013 5:03 PM
Subject: Re: [wanabidii] RE: [Mabadiliko] Haya matusi sasa too much, Kesho tutasikia ngumi zimepigwa
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Ipo siku wananchi watavamia bunge kuwachapa. Kuwatoa kwa kutumia polisi itakuwa kazi ndogo. Inavyoonekana, kuna wakati viti vingi vitupu hawapo. Waweke sheria kwamba atakayekuja kusaidi asubuhi hayupo kutwa nzima bila sababu za kukubalika na kupata ruhsa asilipwe posho. Inaweza kuwa-wengine wanafika kupata posho kisha wanakwenda na hamsini zao. Si wanajua posho itaingia jioni atapata pesa? Mimi huomba daima-kila mpunge awe na plan yake ya shughuli za maendelo ktk jimbo lake. Si wanapewa hela za jimbo? akiwa na plan yake ya maendeleo ya jimbo lake, lazima ahusishe miradi iliyopangwa kwa kupitia strategy ya serikali ya O&OD akiunganisha na vertical programs za serikali kiwizara na hizo zake alizoibua na wananchi wake ambazo hazipati hela ya serikali za O&OD aidha anatumia raslimali zilizopo ktk eneo au anatafuta mwenyewe sources zake na hizo za jimbo kwa miradi iliyokubalika. Awe na action plan na plan of operation. Hivyo, kila mmoja atakaguliwa na Kamati maalum ya bunge ambayo itathibitisha utendaji wake. Waziri husika akitoa bajeti yake na taarifa zake ataitaja miradi anzilishi ya mbunge. Kipindi kiwepo maalum cha bunge ambapo kila mbunge atatoa taarifa ya maendeleo ktk jimbo lake, alichofanya kwa ushirika na idara mbalimbali na alichoibua mwenyewe na watu wake na kufanikisha. Hii itaondoa kumuona mbunge anatafuta ufahari kupitia vyombo vya habari. atajibu hoja na wananchi wanaweza wakaandika magazetini kutoa maoni kama ana danganya. Maana mradi unaweza kuwa donor funded akadai ni wake kauanzisha na kuugharimia. Hata hao akina Sabodo wakimpa hela watampa kukamilisha miradi ya maendeleo sio hela za kulipia safari za uhamasishaji maandamano au kujenga chama bali kujenga maendeleo vijijini kichama, kujenga daraja, madarasa, barabara. Hao watoa hela watoe hela za maendeleo sio kisiasa maandamao. Kingine ni haya malumbano ya ardhi Loliondo Serengeti ambapo sasa kila chama kinashabikia kila mmoja aonekane mtetezi. Hivi ni wananchi wangapi walitolewa maeneo yao sasa wanashida ya ardhi. Wenzetu wafugaji wanazagaa nchi nzima na huko watu wanalishiwa mashamba na kuchapwa na hawana mtetezi? Wao wanalima mpaka ndani ya hifadhi ya wanyama pori kwa vile kwa sasa wamebadilika hawachungi mifugo tu. Hifadhi ngapi ziko kwa wakulima ambao wapo nje sio ndani na mafao hawapati? Kinanuka leo malumbano kaenda wa CCM huko kesho kaenda wa Chadema au wa kabila lake-kitanuka cha moto risasi na mikuki soon. Kinachotakiwa ni kutumia picha za video pia kuonyesha mipaka na uchakachuaji ardhi/uharibifu kwenye maeneo hifadhi wanyama, maji. Maneno tu ktk TV au radio wasiotembea vijijini hawapati picha ya ugaribifu mazingira kupitia kukata miti kuchoma mkaa; kuvamia maeneo ya hifadhi na kulima; ulimbikizaji mifugo na uharibifu mazingira ya mifugo na wanyama pori. Piga picha uonyeshe gold mining ilivyo na utata kwa wachimbaji wadodo wadogo na makampuni. Picha picha onyesha wananchi vijijini walivyojenga mabondeni maeneo ya mto na zima au kujenga fukwe za bahari na Tsunami sasa ni tatizo. Budi sasa kuonyesha maeneo hatarishi kutumia Media kufundisha na kuelekeza watu kwani climate change na mafuriko kwa sasa yanatokea-nchi nzima watu wanaathirika-fedha ipo wapi ya kutoa huduma kwa wote. Hata mbunge akitoa hela kusaidia-daima itajirudia. Asaidie kazi ya kuwashauri wasikae mabondeni asipige kelele tu Bungeni watu wake hawahami maeneo hatarishi. TV onyesha pia hatari ya viwanda kuwa makazi ya watu kwa kuweka video hizo kipindi maalum ktk TV mfano cha malumbano ya hoja. Unyesha mpango ulivyokuwa na uvamizi na ujenzi wa sasa. Jadili hatari iwapo kiwanda kitaungua moto na gas mbaya kutoka kama Bopol na sasa Texas. Si wataungua na hatuna zima moto efficient mpaka tusaidiwe na private companies. Na wala hatuna helikopta ya zima moto. Shughuli za Mbunge ziwe kutetea uhifadhi ardhi, usalama wa raia mipango miji na vijiji vizingatiwe SIO kutaka ufahari kutetea bila kuzingatia umuhimu wa usalama wa watu, viumbe na ecosystem yao. Binadamu tumebadilika ktk nidhamu, mbunge awe wa kutukummbusha wajibu hata wa kujitegemea kwa raslimali tulizonazo kwa kujituma lakini matumizi endelevu. Leo mbunge anayebwatabwata nikienda kijiji kwake (sio jimbo ni kubwa) nitakuwa watu wangapi wanachoo, mazingira safi na wanalima mashamba yao au kufuga sustainably? Huweza ndio zile kelele za debe tupu haliachi kutika. Utakuta hawana vyoo, kinyesi cha mifugo au watu hovyo mpaka vyanzo vya maji au mlangoni yeye anapita na gari. Miti ipo, nyasi au makuti ya kusaidia kujenga choo cha bei nafuu lakini hakuna hamasa na hawajengi. Tupo kuchafua na kuharibu mazingira tunayotegemea kwa survival. Labda wapewe TOR za kazi zao na training katika majukumu yao na mbinu za mawasiliano. Kwani wapo wasomi na wengine ambao si wasomi ila wana nia nzuri ya kusaidia ila hawajui mbinu za bottom-up na integrated approaches (Bottom-up+Top Bottom) na mbinu za mawasiliano na nadharia nyuma yake ya mawasiliano na jinsi ya kubadili tabia na mienendo bila Kubwata. Inasikitisha. Tujadili ya maendeleo kama haya sio kutaka JINA. Hata uwapeleke JKT warudi na vipara wanarudi wanaanza malumbano kama jana na kutoana nje. Jee, mafunzo ya uraia na utanzania hayakufaa au hayakufanyika huko? --- On Fri, 19/4/13, alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com> wrote:
|
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment