Wednesday 24 April 2013

Re: [wanabidii] Rais Kikwete akutana na Viongozi wa Madhehebu ya Kikristo Ikulu

Huwezi kusema Heri anayekimbilia Ikulu kuliko anayeendekeza udini kwenye siasa wakati utamgundua kuwa ana udini akisha fika Ikulu. Umenipata?
Nimependekeza kwenye katiba ijayo moja kati ya Tume ya uchaguzi ni kuzipitia ilani za uchaguzi na kuyaondoa madudu kama ya 2005 yaliyoruhusu udini kwenye ilani ya uchaguzi. Natamani kipengele hicho kipite na nimegombea ujumbe wa Baraza la Katiba wilayani kwangu nikapata. Nataka kuyafuatilia mambo madogo kama hayo.
Kweli taifa ni letu lakini huwa tunajisahau na kufikiri ni la viongozi. Tunazinduka kidogo kidogo. Tunawapongeza viongozi wa Serikali na dini kuanza kuyaona hayo

--- On Wed, 4/24/13, Nico Eatlawe <eatlawe@yahoo.com> wrote:

From: Nico Eatlawe <eatlawe@yahoo.com>
Subject: Re: [wanabidii] Rais Kikwete akutana na Viongozi wa Madhehebu ya Kikristo Ikulu
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, April 24, 2013, 3:37 AM

Kweli hata mimi napongeza hatua ya serikali na viongozi wa dini ya Kikristo kukaa pamoja na kufanya mazungumzo. Nakumbuka Nyerere alivyosema mtu anayetaka kukimbilia ikulu aogopwe kama ukoma. Nafikiri ni heri mara mia ya mtu anayekimbilia ikulu kuliko anayeendekeza udini katika siasa! Tumeshaonja adha ya kuingiza dini kwenye ilani za siasa ijapokuwa kwa kwa uchache! Mwaka 2015 lazima tuwe macho na aina ya watu wanaotumia dini kupata wadhifa wa siasa! Tulikuwa tumelala ila sasa tumeamka nchi nzima baada ya kuona maafa yaliyotokea! Kweli kama Biblia inavyosema 'Kila mtu kile apandacho atavuna' basi tulipanda udini kwenye siasa na tumevuna! Sasa tuna gharama ya kutoa ili kujenga ufa ambao itachukua miaka kuuziba!
 
Kufanya kosa ni kosa ila kurudia ni kosa ni kosa kubwa kasema mwimbaji mmoja. Tumefanya makosa na kuwatoa wengine kafara sasa tusifanye kosa tena!

From: ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Wednesday, 24 April 2013, 10:59
Subject: Re: [wanabidii] Rais Kikwete akutana na Viongozi wa Madhehebu ya Kikristo Ikulu
Hii ni hatua ya kupongeza viongozi wetu (wa dini na serikali). Tulikuwa tunaelekea kubaya.
Tunaamini na viongozi wa dini watafanya kama Rais. Kuhakikisha waumini wao wako wote. Nina maana hawawaburuzi (Maana hawaburuziki). mtume Mohamed si wa mashehe wala Yesu si wa maaskofu. Wao wamedhaminiwa tu. Ni wetu wote. Viongozi wetu wakihakikisha hilo watakuwa wakweli na wawazi.
Baada ya hapo tunatarajia
1) Tanzania ambamo serikali haina dini kama katiba inavyoonyesha.
2) Mihadhara ya matusi inakoma
3) Mauaji ya viongozi yanakoma
4) Ilani za siasa zinajitenga na dini
5) Nakadhalika.
Baada ya hapo mambo mengine yatajifuta yenyewe. Habari za kuchinja zitajifuta nakadhalika.
Kama viongozi wetu wataona tatizo ni haya majani na maua basi watakuwa wanafumba macho kutoona vidonda vinavyovuja. Ila vitakuwa vinavuja tu.
Nawapongeza kwa mara nyingine viongozi wetu kwa mwelekeo huu. Wakijiambia na kuambiana ukweli tunatarajia Tanzania iliyoanza kusahaulika kuona inarudi.
 
Natanguliza shukrani zangu
Elisa Muhingo --- On Wed, 4/24/13, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:

From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
Subject: [wanabidii] Rais Kikwete akutana na Viongozi wa Madhehebu ya Kikristo Ikulu
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, April 24, 2013, 1:02 AM

Viongozi wa dini wamewataka waumini kote nchini kulinda amani na umoja uliopo ili nchi isije ikaingia kwenye mgawanyiko wa kidini na kuleta machafuko hapa Tanzania.Wito huo umetolewa na viongozi wa dini leo Ikulu ya Dar-Es-Salaam mara baada ya kikao cha pamoja baina ya viongozi wa dini na Rais Jakaya Kikwete.Viongozi hao wa dini wamefika leo wakiongozwa na Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).Viongozi wengine wametokea Baraza la Kikristo Tanzania (CCT) Seventh Day Advertist (SDA) na Baraza la Pentekoste Tanzania (PCT).Mkutano huo umeanza kwa Askofu Ngalalekumtwa kusoma tamko lao la pamoja kwa Rais Kikwete ambalo ndilo limetoa muongozo wa mazungumzo hayo ya leo ambayo yamehusu Amani na Usalama wa Taifa na migogoro ya kidini ndani ya jamii.Mkutano wa viongozi wa dini ya Kikristo Tanzania ni mojawapo ya jitihada za Rais Kikwete kutafuta muafaka na kutafuta utatuzi wa hali ya sintofahamu ambayo inanyemelea nchi yetu katika kipindi hiki."Nataka tuzungumze ni namna gani tunaweza kutoka kwenye hali hii na tunakwendaje mbele zaidi na kuhakikisha nchi yetu bado inakua ya amani na umoja kama ilivyozoeleka" Rais amesema na kutoa nafasi kwa viongozi wa dini kutoa maoni yao.Viongozi hao wa dini wamemueleza Rais Kikwete kuwa wanaunga mkono jitihada zake za kutafuta amani na kwa pamoja wamekubaliana uandaliwe mkutano wa pamoja baina ya viongozi wa dini zote ambapo masuala ya amani na umoja wa nchi utajadiliwa kwa kirefu.Katika kikao cha leo pande zote zimekubaliana kuwa kuna changamoto zilizoko sasa zinahitaji kutatuliwa haraka iwezekanavyo ili kuepusha nchi kutumbukia katika mgogoro mkubwa zaidi, na pia kukubaliana kuwa pande zote, kwa maana ya serikali na taasisi za dini, zinawajibu mkubwa wa kuhakikisha amani inadumu.Kabla ya kikao cha leo , Rais amewahi kukutana na viongozi wa dini ya kiislamu na kikristo mmoja mmoja ambapo alikua akitafuta maoni na ushauri wa pande zote kabla ya pande zote hazijakaa pamoja na kuwa na msimamo wa pamoja.Kikao cha leo kimehitimisha jitihada hizo na kinachofuata ni mkutano mmoja ambapo Rais Kikwete atakutana na viongozi wa dini zote kwa pamoja hivi karibuni.………..."MWISHO"……..Imetolewa na: Premi Kibanga,Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,Ikulu-DSM23 Aprili, 2013

Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2RMk79jym
-- Send Emails to wanabidii@googlegroups.com   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. --- You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group. To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com. For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.    

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment