Wednesday 24 April 2013

Re: [wanabidii] Nilimwona Mbongo anakuja na...

Kaka sina mbavu mie!!!

2013/4/24 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
Mbongo, Mganda, na Mkenya walikamatwa na makosa huko Uchina. Wakaambiwa adhabu ni ama kifo cha moja kwa moja au adhabu nyingine ambayo atakayeifaulu atakuwa huru, na atakayeshindwa atauawa. 

Basi wao wakaomba wapewe hiyo adhabu nyingine wajaribu bahati yao.

Wakapelekwa msituni wakaambiwa  kila mmoja aende kwa njia yake halafu arudi na matunda kumi ya kufanana. 

Wakaingia msituni kila mtu kashika njia yake. 

Mganda akarudi wa kwanza na machungwa kumi. Akaambiwa adhabu ni kulimeza moja moja likiwa zima bila kufumba macho, bila kulia, wala kucheka, wala kujitikisa, mpaka yote kumi yaishe. Akameza la kwanza. Safi. Kumeza la pili, akashindwa kuvumilia akafumba macho. Akapigwa risasi, akafa. 

Mkenya akaja. Ana vitunda vidogo vidogo kama pipi, vilaini. Akasomewa masharti. Akaanza kumeza bila kufumba macho wala kulia, wala nini... alipofika cha tisa akashindwa kuvumilia, akaangua kicheko! Akapigwa risasi, akafa. 

Wakiwa kuzimu, Mganda akamwuliza Mkenya, "Vipi, mbona ulishindwa kuvumilia wakati kilibaki kitunda kimoja tu?"

Mkenya akamjibu: "Mkuu, nilishindwa kuzuia kicheko maana nilimwona Mbongo anakuja na matikiti maji!"

Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2RMjsJgsZ

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment