Sunday 21 April 2013

Re: [wanabidii] Mwanamuziki Diamond ni mdhalilishaji wa Mwanamke "Bi.Wema Sepetu"

Ni kwamba kama watu wasima hujiuliza-hivi inakuwaje mtu mzima msanii unabadilisha mabwana au mabibi kama nguo. Alijitoa msichana magazetini etc klujieleza alivyochezewa na kuahidiwa watamtoa kisanii na hakuna lolote. Kuchezewa na wenye hela humo au ndani ya usanii ndio mchezo. Unamuona msichana au mama ana mume au watoto, wazazi na majirani ndugu na jamaa anavyocheza jukwaani matusi ya nguoni kabisa kavaa kichupi. Taifa linaangamia, mbona hatukemei ikawekwa sheria kwa wamiliki wa band kuzuia kulazimisha wacheza dansi kuvaa utupu. Kucheza ni kiuno tu na hata kwa kubong'oa matako na kucheza ambavyo kiafrika ni vya chumbani leo ndio furaha ya jukwaani. Utu na utaifa wetu tunauua. Tunaiga wavaa chupi na wacheza uchi wa ulaya. Tuyakemee na kuyarekebisha haya badala ya kuyachekea. Na ndivyo tunavyokemea kwa sasa yanavyoendelea Bungeni ya maneno na vitendo kinyume na maadili. Tumekee haya ya wasanii. Mbona kwa sasa mavazi ya barmaids yamebadilika wanavaa suruali badala ya sketi nusu uchi. Apendae kuheshimiwa-Pia ajiheshimu.

Bwana Mgeta-tunamengine ya kushughulikia ambayo ni muhimu kama hilo attached na hayo yanayoendelea bungeni.

--- On Mon, 22/4/13, Mashaka Mgeta <mgeta2000@yahoo.com> wrote:

From: Mashaka Mgeta <mgeta2000@yahoo.com>
Subject: Re: [wanabidii] Mwanamuziki Diamond ni mdhalilishaji wa Mwanamke "Bi.Wema Sepetu"
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Monday, 22 April, 2013, 1:29

Hilda, nimependa hoja yako hasa aya hii:

Kingine ni akina dada wasaiii nao kujilinda na kuheshimu utu wao. leo tunaona gazetini ana bwana huyu, kesho wameachana ana bwana mwingine, tena wameachana ana yule na yule-hii nayo ipoje mara karudiana na yule wa zamani. Kwa nini kujirahisi hivi na kukubali picha zao za malavidavi kuwekwa magazetini front page. jee huwa wanalipwa na hayo magazeti. Mbona hatuoni au kusikia wanayashitaki kwa kutoa picha zao za kubusiana wanawake kwa wanawake, na mabwana zao etc. Hii nayo imekaaje kiasi kwamba tukaone  haya mengine muhimu.

--- On Sun, 4/21/13, Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk> wrote:

From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
Subject: Re: [wanabidii] Mwanamuziki Diamond ni mdhalilishaji wa Mwanamke "Bi.Wema Sepetu"
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sunday, April 21, 2013, 6:23 PM

Kama tupo Serious na kukana udhalilishaji wanawake-tungeomba tuombwe Radhi na Wabunge waliotaka Kumpiga Speaker Mh Anna makinda kwa kutaka kuvamia Meza yake. Ama hata kama maspeaker wengine huko nyuma walikosea na kutoa watu nje au kumtaka mtu akae au aendelee kuongea wakati umma wa wabunge wengine hawakutaka hakuna aliyezuka kutaka kumpiga. kumuandika vibaya na kumchora vikatuni ni udhalilishaji kwa vile tu ni 'Mwanamke'. hatujaona wanaharakati na wa masuala ya Jinsia ya kumtetea mwanamke kukemea hili au kwa vile halina mshiko?

Kingine ni akina dada wasaiii nao kujilinda na kuheshimu utu wao. leo tunaona gazetini ana bwana huyu, kesho wameachana ana bwana mwingine, tena wameachana ana yule na yule-hii nayo ipoje mara karudiana na yule wa zamani. Kwa nini kujirahisi hivi na kukubali picha zao za malavidavi kuwekwa magazetini front page. jee huwa wanalipwa na hayo magazeti. Mbona hatuoni au nkusikia wanayashitaki kwa kutoa picha zao za kubusiana wanawake kwa wanawake, na mabwana zao etc. Hii nayo imekaaje kiasi kwamba tukaone  haya mengine muhimu.

Wansanii wacheza dansi anavaa kaptura na sasa eti soksi ndefu  lakini nyepesi za kuonyesha mapaja wanacheza matusi ya nguoni wanaonekana majukwaani, magazetini katika TV wakimwaga radhi. Mtu wa namna hii asiyejiheshumu kichupi jukwaani na nyuma katika mchirizi nyeti kajichora amebong'oa matako kimakusudi na kumwaga radhi-anatetewa vipi na anakuambia anaganga njaa! kwa kujidhalilisha? Heshima itakuja tu kama nawe utajiheshimu. Utakuwa katika kuchangia miradi ya maendeleo jamii si kuchangia ufuksa uendelee, utavaa na kutenda kiheshima ili utetewe kiheshima. Twataka tuone mamilioni umwagayo hovyo yakichangia maendeleo na ukiacha kujidhalilisha ili jamii tukutetee usidhalilishwe. Hii nayo imekaaje hata suala hili liingie kwa wanabidii? jee, mabaraza yao ya wasanii na kamati ya utamaduni kitaifa inachukuliaje masuala ya wasanii kuvaa wavaavyo na kufanya wafanyavyo kinyume cha maadili ya jamii? hivi hawaelewi kuwa wanavyobadili na kuchangia wapenzi ni hatari kiafya? Je, wanawapa semina za mafunzi ya HIV. Stadi za maisha na ujasiriamali? Kwa nini ukubali kutumika vibaya? Jua, Leo una miguu ya kutembea na kucheza dansi, kesho huna ni mgonjwa au hutembei itakuwaje?  Mara tunaona na Wazazi wao nao magazetini picha na kuandikwa masuala mbalimbali. Tunakwenda wapi?

Licha ya kudhalilisha wanawake-tunamuona ktk diamond TV na magazeti akikumbatia kwa kushtukizwa kupewa busu na wanawake. Sasa, ni Vema kwa hao waendao ktk dansi zake kumuonya huko na kususia kwenda hall liwe tupu labda atajirekebisha na wanawake wamsuse kimapenzi ili wasichezewe ajifunze kitu maana si umma wote wa wanawake wa TZ wanafurahiwa na hata hayo ayafanyayo Wema na wasanii wengine masuala ya kujirahisi. Ni sawa kama wengine wasivyopenda tusemavyo hivi ninavyosema mimi hapa. Ni Food for thought.

--- On Sun, 21/4/13, Buberwa Jackob <buberwajackob@yahoo.com> wrote:

From: Buberwa Jackob <buberwajackob@yahoo.com>
Subject: [wanabidii] Mwanamuziki Diamond ni mdhalilishaji wa Mwanamke "Bi.Wema Sepetu"
To: "buberwajackob2012@yahoo.com" <buberwajackob2012@yahoo.com>
Date: Sunday, 21 April, 2013, 14:35

             WANAWAKE WAUNGANA KUSUSIA BIDHAA NA MAONYESHO YA MWANAMUZIKI DIAMOND
                         Kwa Kumdhalilisha Bi.Wema Sepetu kwa kumrekodi katika simu na kusambaza mazungumzo nyeti !

Kitendo cha Mwanamuziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul Juma maarufu kama Diamond,cha kurekodi mazungumzo yake na star wa Bongo Move Bi.Wema Sepetu,
na kuyatuma mazungumzo yao ya mapenzi katika mitandao ni kitendo cha "Udhalilishaji wa Mwanamke" . kwa kuwa wanamuziki na wasanii wote wanatakiwa wawe ni mfamo na kioo cha jamii katika kielekeza jamii kuishi 
kwa kufuata na kuheshimu mahadili ,lakini mwanamuziki Diamond ameonekana kuwa ni  kiongozi wa "Udhalilishaji wa Mwanamke" kufuatia kitendo chake cha
kurekodi na kusambaza mazungumzo yao ya simu  ya kimapaenzi kati yake na
Bi.Wema Sepetu na mpenzi wake wa sasa Bi.Penny,kitendo hiki ni cha "kuwadhalilisha wanawake wa kitanzania" Tunaowaomba akinamama
na kinadada na wanawake wote kwa ujumla kususia kununua video,vcd,cd
pia kugomea kuhudhuria onyesho lolote lile litakalofanya na mwamuziki
Nasibu Abdul Juma aka Diamond hadi pale atakapo waomba radhi wanawake wote
wa kitanzania popote pale walipo.
Wanawake wote wanatakiwa kugomea maonyesho ya mwanamuziki huyo na
na kutonunua bidhaa za mwanamuziki huyo Diamond ili kukomesha kabisa tabia hizi chafu za "Udhalilishaji wa Mwanamke"

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment