Hoja yangu ni kuwa: ukitaka kutetewa acha kujidhalilisha mwenyewe. Hii italeta maana zaidi. Unacheza mauno umebong'oa na kushika meza unakatakata-watakuja hata watoto wadogo kukutomasa hapo kisha udadai haki. Ulaya wabongo walifanya makosa sana miaka ya nyuma. Anaingia bar anamgusa msichana anayetoa huduma kama afanyavyo TZ. Anajikuta anapelekwa policy. Kumbe kule kuuza bia bar ni employment hata ya wake za watu, wanafunzi wasomi masters, PhD wanajitafutia hela na sio malaya. Dreva hata wa Bus, taxi anakuwa msomi anaganga njaa na mwingine anafagia barabara au kuzoa taka kugawa magazeti. Sasa leo una bwana huyu, kesho yule na picha za magazeti za ajabu ajabu. unajipunguzia thamani hata kama unastahili kutetewa. Ujiuze au utembee uchi kwa makusudi barabarani halafu utegemewe kutetewa? Ina gharama yake. Hata wale ambao hutengeneza na kununua mikorogo kisha wanajichubua sana uso anatoka madonda analazwa. uso umebabuka anatisha. Figo zinadhurika pia, wanatutia gharama na kujaza vitanda hospitali bure. Matibabu yao yawe ghali kuliko yule aliyemwagiswa tindikali kwa makusudi. Ufike wakati sasa wasanii na hawa Miss Tz, Miss beer ya Kilimanjaro wawe models wa kusaidia maendeleo badala ya kupamba magazeti kwa uhodari wa vituko vya kujidhalilisha. Jee, hayo magazeti huwa yanawalipa yanavyowatua hivyo wanavyowatoa. Je, Wema amefungua mashitaka mahakamani kumshitaki Diamond na kudai fidia. Amshitaki kwanza ili tuunge mkono. isije kuwa kama yule mama majuzi hapa mume kabaka mtoto wao wa miaka sita GVT imemfunga maisha mama wa mtoto ambaye ndio mke anasema kuwa-mumewe asamehewe. Wema afungue mashitaka na ushahidi anao nasi tutaunga mkono. Isijekuwa Sitaki-Ninataka sisi tushabikie. Shitaki kisha achana naye kupigiana simu na kutongozana naye upya kila wakati naye anakudhalilisha daima. Pia-ogopa HIV, siku hizi hata mate yanaambukiza sio damu pekee. Wanajilindaje na haya kucha kuachana na kurudiana na kuchangia? Anyway, sielewi mengi nimechangia tuu baada ya kusoma-nami ninaomba Kusamehewa!! --- On Mon, 22/4/13, Joseph Beda Rupia <rupia.joseph@gmail.com> wrote:
|
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment