Kama tupo Serious na kukana udhalilishaji wanawake-tungeomba tuombwe Radhi na Wabunge waliotaka Kumpiga Speaker Mh Anna makinda kwa kutaka kuvamia Meza yake. Ama hata kama maspeaker wengine huko nyuma walikosea na kutoa watu nje au kumtaka mtu akae au aendelee kuongea wakati umma wa wabunge wengine hawakutaka hakuna aliyezuka kutaka kumpiga. kumuandika vibaya na kumchora vikatuni ni udhalilishaji kwa vile tu ni 'Mwanamke'. hatujaona wanaharakati na wa masuala ya Jinsia ya kumtetea mwanamke kukemea hili au kwa vile halina mshiko? Kingine ni akina dada wasaiii nao kujilinda na kuheshimu utu wao. leo tunaona gazetini ana bwana huyu, kesho wameachana ana bwana mwingine, tena wameachana ana yule na yule-hii nayo ipoje mara karudiana na yule wa zamani. Kwa nini kujirahisi hivi na kukubali picha zao za malavidavi kuwekwa magazetini front page. jee huwa wanalipwa na hayo magazeti. Mbona hatuoni au nkusikia wanayashitaki kwa kutoa picha zao za kubusiana wanawake kwa wanawake, na mabwana zao etc. Hii nayo imekaaje kiasi kwamba tukaone haya mengine muhimu. Wansanii wacheza dansi anavaa kaptura na sasa eti soksi ndefu lakini nyepesi za kuonyesha mapaja wanacheza matusi ya nguoni wanaonekana majukwaani, magazetini katika TV wakimwaga radhi. Mtu wa namna hii asiyejiheshumu kichupi jukwaani na nyuma katika mchirizi nyeti kajichora ameng'oa matako kimakusudi na kumwaga radhi-anatetewa vipi na anakuambia anaganga njaa! kwa kujidhalilisha? Heshima itakuja tu kama nawe utajiheshimu. Utakuwa katika kuchangia miradi ya maendeleo jamii si kuchangia ufuksa uendelee, utavaa na kutenda kiheshima ili utetewe kiheshima. Twataka tuone mamilioni umwagayo hovyo yakichangia maendeleo na ukiacha kujidhalilisha ili jamii tukutetee usidhalilishwe. Hii nayo imekaaje hata suala hili liingie kwa wanabidii? jee, mabaraza yao ya wasanii na kamati ay utamaduni kitaifa inachukuliaje masuala ya wasanii kuvaa wavaavyo na kufanya wafanyavyo kinyume cha maadili ya jamii? hivi hawaelewi kuwa wanavyobadili na kuchangia wapenzi ni hatari kiafya? Je, wanawapa semina za mafunzi ya HIV. Stadi za maisha na ujasiriamali? Kwa nini ukubali kutumika vibaya? Jua, Leo una miguu ya kutembea na kucheza dansi, kesho huna ni mgonjwa au hutembei itakuwaje? Mara tunaona na Wazazi wao nao magazetini picha na kuandikwa masuala mbalimbali. Tunakwenda wapi? Licha ya kudhalilisha wanawake-tunamuona ktk diamonf TV na magazeti akikumbatia kwa kushtukizwa kupewa busu na wanawake. Sasa, ni Vema kwa hao waendao ktk dansi zake kumuonya huko na kususia kwenda hall liwe tupu labda atajirekebisha na wanawake wamsuse kimapenzi ili wasichezewe ajifunze kitu maana si umma wote wa wanawake wa TZ wanafurahiwa na hata hayo ayafanyayo Wema na wasanii wengine masuala ya kujirahisi. Ni sawa kama wengine wasivyopenda tusemavyo hivi ninavyosema mimi hapa. Ni Food for thought. --- On Sun, 21/4/13, Buberwa Jackob <buberwajackob@yahoo.com> wrote:
|
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment