Tuesday 16 April 2013

Re: [wanabidii] KUTOA TAARIFA ZA MAWASILIANO YA ELEKTRONIKI NI KOSA LA JINAI

Maoni yangu ni machache katika hili .

1 – Tunataka sheria ya mawasiliano ya elekroniki iangaliwe upya ili iweze kuendana na wakati wa sasa iliyopo sasa hivi ina mianya mingi ya watu haswa wahalifu kutumia mapungufu hayo kutenda makosa .

2 – mawasiliano mengi ya sauti au sms yanaweza kupatikana hata kwa njia ya mtandao tu kuna tovuti za kulipia zinazotoa huduma hizo za sauti na mtu anaweza kudownload akaenda kusikiliza na kama ni sms akasoma .

3 – kampuni za simu zina tabia za kuhifadhi mawasiliano ya watu , nashauri mteja awe ana uwezo wa kujua ni mawasiliano gani yake yaliyohifadhiwa na kama yamehifadhiwa kwa idhini yake au ya nani .

4 – pindi taarifa za mteja zinapohitajika na mtu mwingine lazima mteja au mmiliki wa namba husika ya simu ahusishwe maana siku hizi tumeona watu wanatumiwa sms na promosheni bila kujiunga wao wenyewe

5 – watumiaji wenyewe wa huduma hizi za mawasiliano wajenge utaratibu wa kujua na kusoma haki zao kama wateja wa huduma hizi na endapo wakidhulumiwa pia wajue njia za kufikisha suala katika vyombo vya sheria .

2013/4/16 Josephat Isango <joseisango@yahoo.com>
Vyombo vya Usalama vinavyolinda mawasiliano ya watu yabaki salama bila uhai wa watu wenyewe ni hatari zaidi. Watu wanatumia vyombo vya mawasiliano kupanga mikakati michafu ya kuteka, kujeruhi na kuumiza, hiyo tunataka ibaki kuwa siri. Siri za kuua, siri za kuteka, siri za kujeruhi hizi ndio zibaki Siri. Idara ya habari maelezo imesema kweli, kuwa serikali inaficha taarifa za wauaji, inaficha taarifa za watekaji. Ingekuwa haifichi watu wasingekwua wanafanyiwa vitendo vya kinyama nchini halafu tunajidai hatuwajui waliofanya vile, wakati mamlaka ya TCRA ni ya Serikali, Vyombo vyote vya Usalama ni vya Serikali. Habari maelezo imesema imeivua nguo serikali kukubali ambacho kila mara kimekuwa kilikalalamikiwa. Kutokana na Ukweli huu ambao unaletwa na Idara ya Habari maelezo, Simu ya Dr. Ulimboka haitachunguzwa na kama ikichunguzwa hatutaambiwa aliwasiliana na nani hata kama yeye alimtaja. Pili, simu ya Kibanda haitachunguzwa tutapigwa danadana ili wapatikane wakubambikizwa kesi ili wale waliofanya vitendo vya kiharamia waendee kunufaina na "UHURU WA KUJITENGENEZEA". Mwenye kutunza Siri ndiye mwenye wajibu wa kulalamika siri zake zikiibwa, lakini kama anayetunza siri kaona hakuna umuhimu wa kuzitunza basi hizo sio siri tena. Hata hivyo kufanya siri katika kuua watu, Habari maelezo warudi mezani kuandika tamko jingine, hili halijakidhi viwango.

--- On Tue, 4/16/13, Yona Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:

From: Yona Maro <oldmoshi@gmail.com>
Subject: [wanabidii] KUTOA TAARIFA ZA MAWASILIANO YA ELEKTRONIKI NI KOSA LA JINAI
To: "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>, "Wanazuoni" <wanazuoni@yahoogroups.com>
Date: Tuesday, April 16, 2013, 5:20 AM

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

YAH: KUTOA TAARIFA ZA SIRI KATIKA MAWASILIANO

YA ELEKTRONIKI NI KOSA LA JINAI

Jana na leo, Serikali imeona kuzuka kwa tabia ya uvunjaji wa kanuni ya utunzaji wa siri za taarifa za mawasiliano binafsi ya watumiaji wa huduma za simu za mkononi. Taarifa hizo zimefikia hatua ya kuchapishwa katika vyombo vya habari kwa kutaja bila idhini yao, namba za simu, wahusika wa namba hizo, maongezi na muda wa mawasiliano Kati yao. Jambo hili ni Kosa la Jinai. Mfano; tamko la Chadema lililotolewa na Ndugu Mabare Marando Mjini Dar es Salaam tarehe 14/04/2013.

Serekali inapenda kuchukua fursa hii kuwakumbusha wenye makampuni ya Simu, Vyombo vya Habari na wananchi kwa ujumla kuwa, kutoa taarifa za mawasiliano binafsi ya simu baina ya watumiaji wa huduma hiyo, ni uvunjaji wa Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta Na. 3 ya mwaka 2010 na Kanuni za Mawasiliano (Kulinda Wateja) za mwaka 2005.

Kifungu cha 98 ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kinasema;

"Mtu yeyote ambaye ni mfanyakazi wa kampuni yenye leseni ya kutoa huduma za mawasiliano, au mwakilishi wake, ana wajibu wa kutunza siri za mawasiliano binafsi na taarifa zozote za siri za wateja kwa mujibu wa sheria hii". Aidha, "Mtu yeyote haruhusiwi kutoa taarifa binafsi za mteja yeyote alizopokea au kusikia kwa mujibu wa sheria hii isipokuwa tu mtu huyo ameruhusiwa kwa mujibu wa sheria"

Kanuni ya 12 ya Kanuni za Mawasiliano za mwaka 2005 za Tanzania (Kulinda Wateja) inasema:-

"Mtoa huduma za Mawasiliano haruhusiwa kuingilia kati, kusikiliza au kutoa taarifa zozote za mazungumzo ya mteja yeyote yaliyopitia kwenye mtandao wa mtoa huduma, isipokuwa kwa ruhusa kulingana na mahitaji maalumu kwa mujibu wa sheria zilizopo"

Hivyo basi wananchi wanapewa tahadhari kuhusu kutafuta au kutaka kupata taarifa za mawasiliano ya siri kutoka kwa watoa huduma na kuzitumia taarifa hizo binafsi za mawasiliano pasipo kufuata utaratibu ulioruhusiwa kisheria.

Aidha Serikali inapenda kuwatoa wananchi hofu kuwa Mawasiliano yao (maudhui) hayapaswi kuingiliwa kwa kusikilizwa mazungumzo yao au kusomwa meseji zao katika mitandao ya simu. Serikali Kwa kutumia vyombo vyake vya usalama inawahakikishia wananchi kuwa haki zao za faragha katika mawasiliano zinalindwa Kwa Mujibu Wa Sheria Na. 3 ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya mwaka 2010 pamoja Na Kanuni zake.

Kwa taarifa ambazo zimechapishwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari hivi karibuni, Mamlaka ya Mawasiliano pamoja na taasisi nyingine husika kwa mujibu wa Sheria ya EPOCA pamoja na Kanuni zake, wanaelekezwa kufanya uchunguzi wa uvunjwaji huo wa sheria na Mamlaka husika zichukue hatua za kisheria kwa yeyote atakayebainika kuvunja sheria hiyo. 

Serikali inayakumbusha Makampuni ya simu, Vyombo vya Habari na wananchi kwa ujumla kuhakikisha siri za mazungumzo binafsi ya wateja zinahifadhiwa na hazitolewi kwa yeyote isipokuwa kwa mujibu wa sheria.

Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo
16 April 2013

--
www.wejobs.blogspot.com Jobs in Africa
www.jobsunited.blogspot.com International Job Opportunities
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment