Tuesday 9 April 2013

Re: [wanabidii] KUDUNDWA HAKIMU MKAZI LUSHOTO: KILICHOTOKEA

Tulie na maadili potofu yanayozagaa sasa na jinsi ya kuyarudisha nchi hii iwe ya maadili nyumbani, mtaani na maofisini ktk utendaji kazi mbalimbali ndugu yangu Edna. Tufanyeje Mndeme ili tubadilike positively? Tatizo kubwa.
 
Maadili yameshuka sio tu kwa Hakimu, Police, Watumishi wa serikali na makampuni, Mawakili ambao baadhi humtetea mkosa aliyekosa dhahiri kabisa pamoja na vidhibiti kuwepo. Makampuni binafsi-private companies ambayo yanatakiwa yawe efficient baadhi yana umangimeza na rushwa, uharibifu mazingira kuiba hadi umeme wa Luku na maji ya Dawasa kujifungia mita feki kupitia vijizi vyenzao vya mali ya umma.
 
Kuvunjika maadili-ni mpaka home. Unasoma matukio ya wizi wa kuvamia nyumba kuiba na kubaka mama mbele ya watoto; baba wa kambo kukabaka katoto ka kambo mbele ya mama yake na kumlazimisha mtoto kula uchafu daily na mama mzazi hachukui hatua anamwambia akubali ama sivyo watakosa pa kukaa na kula; baba kumbaka mtoto kumpa mimba kisha eti ndugu kumtoa; mwanafunzi/wanafunzi wanabaka walimu na wazazi kuwatoa kwa dhamana; mzazi kuchapa mwalimu shule eti mwanae kachapwa; vizee kubaka vichanga kuvivizia njiani vikienda shule, shamba au kutumwa dukani huko vijiji au kupita mijini vichochoroni vikitoka shule na foleni hizi za mabasi; Kijukuu kumbaka bibi na vibibi viishivyo peke yao kuuwawa usiku kukatwa viungo. Vijijini kwenda shamba maeneo mengine ni tatizo hakuna usalama unaogopwa kuuawa na kukatwa viungo vinavyotumika kiuchawi-kutajirika kwenye madini au biashara. Na bado magazeti (Private sector) yanaachiwa kutangaza dawa za hela za majini, hela za jini chuma ulete, dawa ya kuwa na akili darasani na kupasi mtihani; dawa ya kupata ajira na kupandishwa cheo vitu ambavyo ni kinyume na maadili ila yanaanchiwa yaendelee eti kuganga njaa kipato cha wahusika. Tunatazama kama tunavyotazama majengo yanajengwa pasipo ruhusiwa.
 
Vijana wa ulinzi shirikishi kugeuka kuwa waporaji wa mabavu, wakusanya kodi kiwizi na kumwaga biashara za wafanya biashara wadogowadogo waipotoa rushwa. ulinzi shirikishi unakuwa wizi shirikishi kwa vijana nwalioaminiwa kuvunja maadili na kuwaumiza waliowaamini. Vijijini baadhi ya wananchi wanakaribisha wahamiaji haramu, wengine kuwaoza watoto wao kwa wageni na kuwapa maekari ya ardhi. bado kuna mtu anamiliki customary land.
 
Hii ya kiongozi wa Usalama kumdunda mwanasheria si ajabu maana inatokana na mmomonyoko wa maadili. Kuna haja ya serikali kubadilika na serikali ni pamoja na sisi kukazania mabadiliko pale tulipo kujenga maadili. Ni pamoja na police na wanasheria kubadilika kujionya kikazi. Pamoja na mafunzo tupatayo ya kazi yetu, iwe lazima kuwa na semina za kikazi ya maadili na ushirikiano kazini. Zikifanyika kimkoa na kiwilaya, kata kamati za viongozi zinapokaa mfano regional management teams/committee, District (DMT) na Kata (WDC) na Village Council (VGT na kamati zake).
 
Bila ushirikiano, mawasiliano na uwiano kimaadili na kiutendaji daima hakutokosa utata bali ushindani na migongano. 
 
--- On Mon, 8/4/13, Edna Mndeme <ednamndeme@yahoo.com> wrote:

From: Edna Mndeme <ednamndeme@yahoo.com>
Subject: Re: [wanabidii] KUDUNDWA HAKIMU MKAZI LUSHOTO: KILICHOTOKEA
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Monday, 8 April, 2013, 15:59

 Eee hii nayo kali! tatizo la mamuraaaa wetu ni chochote hasa akishamtishia mtuhumiwa kuwa atafungwa ampe chochote na asimpe na akaenda mahakamani asifungwe. Waungu mtu hawa! Sasa huyu bosi wa muraaaa maskini ya Mungu mhh! nashindwa kuelewa interest yake kwenye kesi hii maana kweli kazi ya hakimu haimhusu.
Du Hakimu pole !

--- On Sun, 4/7/13, Lushengo Lutinwa <lutinwa@gmail.com> wrote:

From: Lushengo Lutinwa <lutinwa@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] KUDUNDWA HAKIMU MKAZI LUSHOTO: KILICHOTOKEA
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sunday, April 7, 2013, 9:15 AM

Anna,

Mara nyingi nashindwa kukuelewa. Issue sio  kupokea chochote, ni guts za kuamua kujichukulia sheria mkononi. Ukizingatia hawa polisi wa vodafasta   ( miezi 9 Moshi) ndio tunategemea kulinda sheria.

Lutinwa

Sent from Galaxy Note

On 7 Apr 2013 19:01, "anna nyanga" <luguanna@yahoo.com> wrote:
Mbona hujatueleza kuhusu chochote? je mheshimiwa Hakimu amechukua au la?
Hapo inawezekana ndipo utata ulipo!!

From: mutabaazi lugaziya <mjlugaziya@mail.com>
To: Mabadilikotanzania <mabadilikotanzania@googlegroups.com>; wanabidii@googlegroups.com
Sent: Sunday, April 7, 2013 3:50 PM
Subject: [wanabidii] KUDUNDWA HAKIMU MKAZI LUSHOTO: KILICHOTOKEA

Ndugu zangu,

Siku si nyingi, mama mmoja alimkuta kijana mmoja akiwa chumbani na mtoto wa dada yake. Binti huyo alikuwa na umri mdogo kwa hiyo, anachukuliwa kuwa hawezi kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi, (ex presumptioner juris)kwa namna yoyote.

Kitaani walifahamu kuwa mtoto yule alikuwa" mcharuko" ki namna fulani, hata hivyo, mama huyo alisisitiza kutoa taarifa polisi. Jalada la "kubaka" likafunguliwa, na mtuhumiwa kupelekwa mahakamani. Hata hivyo, inadaiwa mama huyo baada ya kuelezwa ukweli kuhusu binti yake, na kwamba majirani hawakudhani kuwa kijana amebaka(maana alikuwa ameingia muda mfupi), mama huyo alikwenda polisi na kuomba kufuta malalamiko yake. Mkuu wa Upelelezi alimweleza kuwa kesi hiyo ni kubwa na kwamba mama yule siye mlalamikaji, bali yeye ni shahidi tu wa Jamhuri. Ikadaiwa kuwa kama anataka kesi ifutwe, atoe chochote, jambo ambalo hakuliafiki.

Kesho yake kesi ikaja kutajwa, ambapo mama yule alisimama na kumweleza Hakimu Mkazi Yona Wilson, kwamba analazimishwa na polisi kuendeleza kesi ambayo yeye mwenyewe hataki kuendelea nayo. Baada ya Hakimu kuwasiliana na Mwendesha Mashtaka, wakakubaliana kwamba shtaka hilo liondolewe c/k 224 cha Penal Code. Kifungu hicho kinaipa mamlaka Mahakama kuondoa shtaka ambalo mlalamikaji anataarifu kwamba hana nia ya kuendelea na kesi. Hiyo ilikuwa tarehe 21/3/2013.

Taarifa za kuondolewa kwa kesi zilipomfikia OC CID, Jumanne Juke, hakuridhika. Kesho yake saa 2.00 asubuhi, akifuatana na askari anayeitwa Elisante, walikwenda hadi ofisini kwa Hakimu Mkaazi, na bila nidhamu yoyote kwa ofisi ile, wali 'storm in", na kuanza kumhoji Hakimu kwa nini amefuta kesi "kubwa" kiasi kile, kinyume na sheria inayozuia kufutwa kwa kesi "kubwa" kama hiyo. Hakimu akamweleza kuwa ameifuta kwa mujibu wa sheria na kama anaona kulikuwa na makosa, angekata rufaa.

Jibu hilo lilimuudhi OC CID ambaye alimpiga Hakimu na faili usoni na kuzua tafrani ofisini. Hakimu mwingine aitwaye Mng'uto aliyekuwa 'typing pool" ambayo mlango wake unaingiliana na ofisi ya Hakimu Mkazi huyo, alijitosa na kumdaka Hakimu aliyepandwa jazba. Wakati huo huo, askari Elisante akamvuta bosi wake na kumtoa nje. Hakimu Mhguto akafunga mlango kwa ufunguo ili jamaa wasirudi tena.

Kama kawaida, jeshi la polisi limekwisha kumtuma ofisa wake kuja kufanya "uchunguzi", ingawa wao ndio watuhumiwa.

Sisi(Mawakili)  kama maofisa wa Mahakama tumesikitishwa na tunalaani jambo hili kwa nguvu zote. Tumetoa taarifa kwa Rais wa CXhama cha Wanasheria Tanganyika. Tunategemea chama chetu kitatoa tamko hivi karibuni.

Mambo mengine unaweza kudhani ni simulizi za Abunuwas!

Natoa taarifa!

MJL

--
Jobs in Africa - http://www.wejobs.blogspot.com/
International Jobs - http://www.jobsunited.blogspot.com/
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
0 comments:

Post a Comment