Sunday 7 April 2013

Re: [wanabidii] KUDUNDWA HAKIMU MKAZI LUSHOTO: KILICHOTOKEA

Anna,

Mara nyingi nashindwa kukuelewa. Issue sio  kupokea chochote, ni guts za kuamua kujichukulia sheria mkononi. Ukizingatia hawa polisi wa vodafasta   ( miezi 9 Moshi) ndio tunategemea kulinda sheria.

Lutinwa

Sent from Galaxy Note

On 7 Apr 2013 19:01, "anna nyanga" <luguanna@yahoo.com> wrote:
Mbona hujatueleza kuhusu chochote? je mheshimiwa Hakimu amechukua au la?
Hapo inawezekana ndipo utata ulipo!!

From: mutabaazi lugaziya <mjlugaziya@mail.com>
To: Mabadilikotanzania <mabadilikotanzania@googlegroups.com>; wanabidii@googlegroups.com
Sent: Sunday, April 7, 2013 3:50 PM
Subject: [wanabidii] KUDUNDWA HAKIMU MKAZI LUSHOTO: KILICHOTOKEA

Ndugu zangu,

Siku si nyingi, mama mmoja alimkuta kijana mmoja akiwa chumbani na mtoto wa dada yake. Binti huyo alikuwa na umri mdogo kwa hiyo, anachukuliwa kuwa hawezi kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi, (ex presumptioner juris)kwa namna yoyote.

Kitaani walifahamu kuwa mtoto yule alikuwa" mcharuko" ki namna fulani, hata hivyo, mama huyo alisisitiza kutoa taarifa polisi. Jalada la "kubaka" likafunguliwa, na mtuhumiwa kupelekwa mahakamani. Hata hivyo, inadaiwa mama huyo baada ya kuelezwa ukweli kuhusu binti yake, na kwamba majirani hawakudhani kuwa kijana amebaka(maana alikuwa ameingia muda mfupi), mama huyo alikwenda polisi na kuomba kufuta malalamiko yake. Mkuu wa Upelelezi alimweleza kuwa kesi hiyo ni kubwa na kwamba mama yule siye mlalamikaji, bali yeye ni shahidi tu wa Jamhuri. Ikadaiwa kuwa kama anataka kesi ifutwe, atoe chochote, jambo ambalo hakuliafiki.

Kesho yake kesi ikaja kutajwa, ambapo mama yule alisimama na kumweleza Hakimu Mkazi Yona Wilson, kwamba analazimishwa na polisi kuendeleza kesi ambayo yeye mwenyewe hataki kuendelea nayo. Baada ya Hakimu kuwasiliana na Mwendesha Mashtaka, wakakubaliana kwamba shtaka hilo liondolewe c/k 224 cha Penal Code. Kifungu hicho kinaipa mamlaka Mahakama kuondoa shtaka ambalo mlalamikaji anataarifu kwamba hana nia ya kuendelea na kesi. Hiyo ilikuwa tarehe 21/3/2013.

Taarifa za kuondolewa kwa kesi zilipomfikia OC CID, Jumanne Juke, hakuridhika. Kesho yake saa 2.00 asubuhi, akifuatana na askari anayeitwa Elisante, walikwenda hadi ofisini kwa Hakimu Mkaazi, na bila nidhamu yoyote kwa ofisi ile, wali 'storm in", na kuanza kumhoji Hakimu kwa nini amefuta kesi "kubwa" kiasi kile, kinyume na sheria inayozuia kufutwa kwa kesi "kubwa" kama hiyo. Hakimu akamweleza kuwa ameifuta kwa mujibu wa sheria na kama anaona kulikuwa na makosa, angekata rufaa.

Jibu hilo lilimuudhi OC CID ambaye alimpiga Hakimu na faili usoni na kuzua tafrani ofisini. Hakimu mwingine aitwaye Mng'uto aliyekuwa 'typing pool" ambayo mlango wake unaingiliana na ofisi ya Hakimu Mkazi huyo, alijitosa na kumdaka Hakimu aliyepandwa jazba. Wakati huo huo, askari Elisante akamvuta bosi wake na kumtoa nje. Hakimu Mhguto akafunga mlango kwa ufunguo ili jamaa wasirudi tena.

Kama kawaida, jeshi la polisi limekwisha kumtuma ofisa wake kuja kufanya "uchunguzi", ingawa wao ndio watuhumiwa.

Sisi(Mawakili)  kama maofisa wa Mahakama tumesikitishwa na tunalaani jambo hili kwa nguvu zote. Tumetoa taarifa kwa Rais wa CXhama cha Wanasheria Tanganyika. Tunategemea chama chetu kitatoa tamko hivi karibuni.

Mambo mengine unaweza kudhani ni simulizi za Abunuwas!

Natoa taarifa!

MJL

--
Jobs in Africa - http://www.wejobs.blogspot.com/
International Jobs - http://www.jobsunited.blogspot.com/
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
0 comments:

Post a Comment