Friday 5 April 2013

Re: [wanabidii] Kasoro Za Uchaguzi Wa Wawakilishi wa Mabaraza ya Kata-Nzasa Mwenge

Ndugu Sasali ,  ndugu Peter  na wengine ambao hawajajitokeza kusema lolote hadi muda huu,
Ukweli hali ndo hiyo, na haifurahishi hata kidogo.
Naamini Jukwaa la Katiba Tanzania , linaloongozwa na ndugu Deus Kibamba na kuratibiwa na Dada Diana Kidala, wapo bega kwa bega nasi ili kuona tunakabiliana vipi na matukio haya au changamoto hizi. Hali ilivyo, tuna taka au hatutaki, mwisho ni kupatikana kwa katiba mbaya kuliko ya sasa, kwani pameshaingia itikadi za vyama na uchu wa kupata nafasi kama hizi za kuingia katika mabaraza ya katiba ya Wilaya,  hata kama mtu anajijua kuwa anauwezo mdogo sana katika masuala ya katiba mbadala na ilyobora zaidi.

Mwisho, naamini wote tutaungana na Jukwaa la katiba , kupitia fomu yao ya Tathmini, ili tuijaze na kuona nini kifanyike.

Asanteni sana,

Mpendwa  Chihimba
ED - Women Fighting AIDS in Tanzania( WOFATA )

--- On Thu, 4/4/13, Peter Lwegasira <petermakatu@yahoo.com> wrote:

From: Peter Lwegasira <petermakatu@yahoo.com>
Subject: Re: [wanabidii] Kasoro Za Uchaguzi Wa Wawakilishi wa Mabaraza ya Kata-Nzasa Mwenge
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, April 4, 2013, 7:03 AM

Sasali,

Asante kwa hilo. Mimi niligombea kwetu Mtaa wa Kingugi Kata ya Kiburugwa Wilaya ya Temeke.

Cha ajabu ni kuwa mtendaji wa mtaa (mwajiliwa wa serikali) aliponiona nafika kwenye eneo la tukio aliniuliza hivi: "Mbona huku

ja na wapiga kura wako?" Nikabaki mdomo wazi. Mengine yaliyojitokeza labda niandike kitabu!!!!!!!????

From: "samuel_sasali@yahoo.com" <samuel_sasali@yahoo.com>
To: marafiki Huruuu <marafikihuruu@yahoogroups.com>; "TAFESAssociates@yahoogroups.com" <tafesassociates@yahoogroups.com>; "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Thursday, April 4, 2013 12:32 PM
Subject: [wanabidii] Kasoro Za Uchaguzi Wa Wawakilishi wa Mabaraza ya Kata-Nzasa Mwenge

Ninawasalimu,

Ikiwa zoezi la kuhesabu kura likiendelea hapa Mwenge Nzasa kwa ajili ya Wajumbe Wa Mabaraza Ya Kata kwa Ajili Ya Kutengeneza Rasimu Ya Katiba Likiendelea kumetokea kasoro kadhaa ambazo kwa namna moja ama nyingine naona ni kama vile gharama ya Kukaa Uswazi sehemu ambayo utaratibu wa kufuatwa ni kitendawili.

Niliwasili eneo la uchaguzi mnamo saa 4 na dakika 10 na utaratibu wa kujiandikisha kwa wakazi lilikuwa likiendelea. Baada ya dakika chache ukatangazwa utaratibu wa Kupiga kura kwa makundi matatu, watu wazima, wanawake na vijana hapo ndipo kasoro zilipoanza.

1. Wagombea Kuto Kupata Nafasi Ya Kujieleza. Kundi la kwanza lilikuwa na wagombea zaidi ya 20 ambao hawakupewa nafasi hata ya kujieleza. Nina amini katika Kujieleza sababu wawakilishi hawa wanakazi ya ujenzi wa hoja huko wanakokwenda. Kitendo hiki kinasababisha uchaguzi usiwe wa huru sababu majina yamewekwa ubaoni kisha unaambiwa chagua jina moja hapo tunawafahamu vipi hawa wagombea?

2. Kukosekana Idadi Kamili ya Wapiga Kura. Huu uchaguzi hauna idadi maalum ya wapiga kura. Hakuna mfumo wa kuhakiki kuwa ni kweli hawa wapiga kura ni Wakazi wa Mwenge Nzasa ama lah. Kumekuwepo na Mamuluki wakutosha, idadi ya wapiga kura haifanani na wale waliojiandikisha kupiga kura, yamkini kuna wapiga kura wamepiga kura zaidi ya Mara moja katika zoezi la kupiga kura.

3. Kampeni Chafu Wakati wa Kupiga kura. Kutokana na wakazi wengi kutokuwa na Elimu ya Kutosha juu ya Kinachoendelea wengi wao wamejikuta wakishawishiwa na baadhi ya wapiga kura kumpigia kura fulani kutokana na kufahamiana na sio uwezo wa mtu kufanya kazi. Nimekutana na watu wengi hapa ambao najua uwezo wanao wa kuleta mabadiliko lakini swali la Kujiuliza nani anawafahamu awapigie kura wale wanaojulikana kwa kutumia watu waliokuja nao wengine wamefanikiwa kuwarubuni wapiga kura ili kuweza kumpigia Kura fulani pasipo jali uwezo wa Mtu.

4. Utaratibu Mbovu wa Kuhesabu Kura. Zoezi la kura wakati linaendelea wametokea tu watu ambao wamesema "wamejitolea" na si "mawakara" wa wagombea. Tunathibitishaje kuwa hawa wanaohesabu kura wanaziweka sehemu husika?nani anajua majina ya wagombea ki ufasaha?ninachelea kusema kuna "magic barrot" hapa itatokea na kitendo cha wagombea wengine kuondoka kituoni kinatoa loop hole ya kura kuchakachuliwa kutokana mfumo mbovu wa kuhesabu.

MWISHO.
Kwa kuwa kuna kujuana kwingi kuliko uwezo wa wagombea ninafikiria kuulalamikia uchaguzi huu rasmi katika ngazi ya Wilaya kwa sababu ambazo nimezitaja hapo juu, is kwa sababu tu mimi ni mgombea bali ili kuweza kupata viongozi wasiochakachuliwa na mfumo uliopo.

Sasali
Mgombea Nafasi Ya Kuwakilisha Vijana
Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment