Wednesday 24 April 2013

Re: [wanabidii] Ezekiel Maige : Kwa nini nimekataa bajeti ya Kilimo

Yeye binafsi kwa nafasi yake kama mbunge na waziri, kuna jambo lolote alilifanya kuhakikisha, japo kwa kiwango kidogo, kunakuwa na mashamba ya umwagiliaji katika eneo lake?

Serikali kuu kwa kupitia wizara ya kilimo ina wajibu wa kukuza na kuimarisha kilimo lakini jukumu hilo lipo pia kwa serikali za mitaa, kiongozi mmoja mmoja na mwananchi mmoja mmoja.

Huko nyanda za juu anakosema kuna miradi ya umwagiliaji, siyo miradi yote ilianzishwa na wizara, mingine ni ya jamii ambayo imeongezewa nguvu na wahisani mbalimbali lakini pia yapo mashamba yanayomwagiliwa ambayo ni ya makampuni na watu binafsi.

Kuna mwamko mdogo sana wa kilimo cha umwagiliaji kanda ya ziwa, na hata viongozi wa maeneo hayo, nao hawaoni kama kuna umuhimu, na ndiyo maana hata viongozi binafsi hawaweki jitihada katika kuanzisha na kuendeleza kilimo cha umwagiliaji.

Bart

From: mngonge <mngonge@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Wednesday, April 24, 2013 10:05 AM
Subject: Re: [wanabidii] Ezekiel Maige : Kwa nini nimekataa bajeti ya Kilimo

Awe anahudhuria au haudhurii RCC au vikao vya wilaya haizuii kuona kwamba hakuna mafanikio yoyote yanayoonekana katika kilimo chetu. Ipo haja ya kulitazama vizuri swala hili kwa makini na kufanya mapinduzi katika kilimo. Watanzania walio wengi tunasema ni wakulima na hivyo tukiendelea kuleta mchezo katika kilimo Tanzania itabaki na maendeleo kwenye majukwaa ya siasa tu. Tutabaki na misemo yetu ya dhihaka kwa umma kama vile "Maisha bora kwa kila mtanzania
"

2013/4/23 Nyabenda Juma <jngama@yahoo.co.uk>
Mkataa bajeti anayo hoja, lakini ananinisikitisha anaposema kuwa maeneo yenye mvua  ndiyo yaliyopewa irrigation schemes, kwake hakuna. Inashangaza coz uwepo au kuanzishwa kwa irrigation schemes sasa kunafanywa na kanda kwa kushirirkiana na mikoa/wilaya. sijui kama yeye anahudhuria RCC au viakao vya wilaya.... ninamashaka na uwajibikaji wake kwa wananchi

--- On Tue, 23/4/13, Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com> wrote:

From: Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>
Subject: [wanabidii] Ezekiel Maige : Kwa nini nimekataa bajeti ya Kilimo
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Tuesday, 23 April, 2013, 16:03

Wapendwa marafiki, yawezekana wenginenhamjafuatilia mjadala Bungeni leo na hivyo mnaweza kusikia kupitia vyombo vya habari na hivyo kupata edited version of my comments. Nawafahamisha kuwa nimekataa bajeti kwa kuwa Bajeti haijatatua wala kuonyesha mwelekeo wa kutatua matatizo ya wananchi wangu ambayo ni NJAA ENDELEVU kutokana na ukame wa mara kwa mara na UMASKINI unaozidi kuongezeka kutokana na BEI DUNI YA MAZAO YA KILIMO NA MIFUGO NA TIJA NDOGO KATIKA KILIMO. Nilitegemea Bajeti iwe na Skimu zaUMWAGILIAJI kama jibu la mvua haba na pia PRICE STABILIZATION FUND kwa bei ya Pamba. Aidha nilitegemea kungekuwa na mkakati wa kuanzisha viwanda vya nguo ili kuwa na soko la ndani kwa pamba yetu! Sjinyanga, ambayo kila siku kuna njaa hakuna skimu ya umwagiliaji na maeneo yenye mvua kama Kigoma, Rukwa, Katavi, Kilimanjaro, Mbeya nk yenye mvua ndiyo yamewekewa skimu za umwafiliaji. Hili haliwezekani. NIMEKATAA.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment