Wednesday 24 April 2013

Re: [wanabidii] BOMOA BOMA KIGAMBONI


Poleni Kigamboni. Lakini undani ujulikane ni mazao ya aina gani-mchicha, nyanya, au minazi, miembe etc maana kila zao lina bei yake. Jee, huko nyuma hilo eneo ni lao asilia au, walivamia, wakakaa miaka hapo palikuwa pa jeshi JWTZ, Magereza, Police au Chuo cha huko, mashamba ya katani au ya Social Welfare na makazi ya wazee au vilema na mashamba yao kisha vikaishia mashamba yakaachwa hayalimwi wao wakahamia au ni ya Taasisi ya Bandari na makazi ya wafanyakazi wao au ya taasisi ya dini enzi za ukoloni?

Jee baada ya kutakiwa kuondoka hapo wamepimiwa viwanja na walilipwa fidia ya nyumba na wakapewa grace period ya kuhama? Miaka mingapi imepita? Maana wengine hulipwa bei itakiwayo ya nyumba na mashamba, wakatumia hela na kubaki hapo bila kujenga, miaka ikapita wakaanza madai mapya kuwa hela ilikuwa ndogo, hatuondoki na kuanza litigation isiyokwisha serikali ikachoka kusubiri. Haya nayo yanawezekana maana hata maeneo mengine haya ya pili hutokea. Mtu anapata milioni 20 anaona nyingi baada ya muda zinaishia na utata unaanza. Au eneo ni la GVT/umma anapewa tu hela kuondoa usumbufu (milioni 50 wale wa Gerezani nyumba za registrar wakazania za babu) wakagoma kuondoka na kufungua kesi zikaja kuvunjwa na waliogoma wakakosa hata hiyo milioni 50 ya bure na nyumba za ghorofa hizo si zao. Tumeona ktk TV issue hii. GVT iliweka vijiji nje ya miji kama Dar na viliandikishwa. Watu wakawa na mashamba kilimo cha kufa na kupona. Sasa inasema-huu mji hakuja vijiji na mashamba-watu wanaathirika vibaya ambapo mashamba hayo yangewasaidia kujikimu. Nchi haina social security fund ya kumlipa mtu mshahara kima cha chini kama hana ajira. Unachukua eneo lake na kupima viwanja. Hao wapewao viwanja na GVT hawamlipi na serikali hailipi haina hela na waliopimiwa na kupewa hutumia nafasi waliopata kuviuza na kupata mamilioni wao.

Sijui bomoabomoa itakapoingia Ubungo Mataa hadi Kimara Temboni pande zote mbili itakuwaje!! Maana pamoja na EIA iliyofanyika na valuation 1994, na malipo na X kuwekwa waliobomoa na kuondoka ni wachache, bado wanaendelea kujenga katika Road Reserve na msongamano unakua. Watakapoanza kubomoa Jangwani na bonde lote la Msimbazi na ya Mito ya Mbagala patakalika maana bado ujenzi bondeni na makazi yanaendelea na mvua ikija na maji yake inawatesa kweli wao na wengineo maana maji yanakosa mapito yake asili na kutafuta mapito mengine na kupasukia huko. Jinsi barabara mpya inavyojengwa Manzese, Kagera na mvua hii kunyesha maji yanayotoka barabarani kushuka bondeni ambako ndio kuna nyumba na zimebanana ktk mapito ya maji ni hatari. Kwani hata ule mjengo wa NHC na barabara zake zilikwisha kufungwa na vibanda vya biashara. Ili kuwe na feeder roads na mitaro ya kupita maji, itabidi kubomoa baadhia ya nyumba na kutumia Ramani ay 1970 kuzirudisha zile barabara na mitaro ya maji. Hapo hapatakalika-kuchoma magreda moto na kuua polisi. Bado kule ambako kulikuwa na NHC houses mijini quarters za serikali vibanda vya vigae na bati vilivyokaa vibaya ambako wakazi waliokuwa wakiishi kama watumishi wamejenga nyumba za kisasa lakini hawajauziwa hizo za NHC. Na huko ambako serikali inajua ina shamba la katani au Minazi, Kahawa, Malaka ya Pamba na imepata mwekezaji lakini anapofika huko anakuta maboma ya mifugo na nyumba/boma za makazi za wachungi wahamajihamaji; wanakuta nyumba za kisasa, miembe na minazi jamaa wamehamia wakijua mashamba hayo hayatolimwa tena na GVT. Huku nako ubomoaji itakuwaje. Patakalika kweli nchini?
Ina maana, serikali na mashirika yake ya mwaka 47 iangalie uwezekano wa kuwa na vurugu kubwa na mauaji kama hawatojirekebisha sasa na utendaji wao ktk kuangalia mali za umma, kutekeleza sheria mara badala ya kuacha tatizo zinaendelea halafu kuzusha ya kuzusha. Mfano wanaona watu wanajenga vibanda vya biashara ktk public place ya kuzunguka shule wanatazama tu waje kubomoa baadae. Shule inajenga ukuta kuzunguka eneo lake, kuweka vyumba vya biashara kuongeza kipato cha shule na kutoa fursa kwa wafanyabiashara kupanga bila ya kuangalia aina ya biashara kimaadili.Wanaona biashara zinapangwa ktk njia za watembea kwa miguu na watembea kwa miguu hatuna pa kupita na pikipiki zinapita humo kati ya biashara na upoenyo mdogo uliobaki wa miguu-tabu na karaha. Lakini inaendelea.

Mifugo mjini inachungwa kando ya barabara-Serikali hawaibebi kuipeleka kuitaifisha maana ni uvunjaji sheria. Inasababisha accidents na kutishia watu maisha maana ng'ombe wengine wakali.Kama ni Zero grazing iwe ndani ya nyumba na bila karaha kwa wakazi wengine. Lakini ni mifugo barabarani ktk city, harufu ya mifugo na kinyesi kwa majirani na kinyesi na maji yake kuzagaa. Serikali za mitaa zipo. Mtanzania anaona anakosea lakini anaendelea kufanya visivyo. Mwenye migombe mikubwa hiyo ni wealthy person na anaweka mchungi.Haihamishii nje ya mji kwa nini? Bongoland huru bila kuzingatia sheria ndio donda sugu letu.Dhuluma na uonevu ni kilema.


--- On Tue, 23/4/13, Didas Clemence <didasclemence@yahoo.com> wrote:

From: Didas Clemence <didasclemence@yahoo.com>
Subject: [wanabidii] BOMOA BOMA KIGAMBONI
To: "wanabidii google" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Tuesday, 23 April, 2013, 14:00

Hii inasikitisha sana,nimeenda na kujionea mwenyewe, naweka picha vizuri ili mjionee wenyewe, to me this is not fair,,,,kwa vyovyote vile hii haikubaliki

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment