Tuesday 16 April 2013

Re: [wanabidii] BAADHI YA MAMBO AMBAYO UNATAKIWA KUWA NAYO MAKINI KWENYE FACEBOOK

Shule nzuri lakini hatufundishiki bwana


2013/4/16 Yona Msuya <yonamsuya@gmail.com>

Facebook imekuwa kama Google ya mitandao ya kijamii. kama sasa hivi hauposti status yako basi unapandisha picha au unajibu quiz ya facebook games. Tunaandika vitu vya ndani kabisa vya maisha yetu ambavyo katika maisha halisi hatuwezi kumwambia yoyote. Tunadhani kwamba ili mradi tumeweka  privacy settings zetu sawa sawa basi tupo salama.

 tatizo ni kwamba hatujui nani hasa anatuchunguza habari zetu. Akaunti ya rafiki zatu inaweza ikawa hacked baada ya kuweka program ya ajabu ajabu kwenye simu au computer, au labda mjomba wake ndio anatumia account kwa sababu amesahau ku-log out. lakini vile vile ni internet cafe ambapo wabongo wengi tunapapendaKwa usalama wako na wa familia yako, kuna vitu haupaswi kuviandika Facebook. Kamwe. Hivi hapa ni vitu vitano ambavyo inabidi uvitoe au siviandike kwenye Facebook.

 1. Tarehe yako ya kuzaliwa yote kamili.

 Sote tunapenda kupata Happy birthday notifications kwenye walls zetu. Inatufanya ndani ya moyo tujisikie raha fulani kwamba kuna mtu  amekumbuka birthday yako na amekutumia wishes. Tatizo ni kwamba unapoweka mwaka wako wa kuzaliwa wote, unawapa wezi nafasi ya kupata moja ya taarifa za muhimu zinazohitajika ili kukuibia. Ni muhimu usiweke na kama ukiamua kuweka basi usiandike mwaka wenyewe. Kwanza marafiki zako halisi wanajua tayari.

2. Hali yako ya mahusiano

 Uko kwenye mahusiano au la, ni vyema usiutangazie umma. Stalkers watafurahia kujua kwamba kuna single mpya mtaani.Ukibadilisha status yako kuwa single ndio umewawashia taa ya kijani kwamba umerudi sokoni. Kama ulikuwa umeoa ndio utafanya wajue kuwa upo nyumbani peke yako. Cha busara kufanya ni kutokuandika kabisa.

 3. Mahali ulipo

 Kuna watu wengi wanapenda ile feature ya facebook ya location tagging ambapo unaweza kum-tag mtu/watu kwamba uko wapi. Tatizo ni kwamba umeshawaambia watu kwamba upo likizo mkoa na sio nyumbani kwako. Tena ukiongeza utakaa muda gani basi wezi/majambazi ndio watajua kabisa ni mmuda gani wakavamie kwako. Ushauri wangu ni kwamba usiandike kabisa. Unaweza kuweka picha zako za safari ukisharudi nyumbani.

 4. Kwamba upo nyumbani peke yako

 Wasichana wengi wa kibongo ndio wanapenda hii. "Nipo nyumbani peke yangu nimeboreka kweli!" "Nipo lonely nyumbani, nipeni ushauri fans wangu" na vitu kama hivyo ndio utavikuta kwa waTZ wa facebook wengi.

 Tunaweza tukadhani ni marafiki wetu tu ndio wanaona post zetu, lakini ukweli ni kwamba hatuwezi kujua nani anasoma tarifa zetu. Mtu anaweza kuiba akaunti ya rafiki yako mradi apate mwanya wa taarifa zako! Unaweza ukaweka privacy settings  lakini kama account ya rafiki yako  ikichezewa, kila kitu kipo wazi.

 5.Picha za wanao na tags za majina yao

 Wenye watoto mnapenda watoto wenu.Mtafanya chochote kuwalinda na kuwaweka salama. lakini wengi huweka picha za wanao ndani ya facebook na wengine huenda mbali mpaka kuweka picha za wanao kama profile picha!

 Wazazi 9 kati ya 10 wameshawahi kuweka picha za wanao na majina yao na wengine kuwa-tag na ndugu, marafiki, na jamaa zao. Taarifa kama hizi zinaweza kutumiwa na wahuni kukuumiza wewe. Wanaweza kutumia jina la mwanao na la ndugu kujenga uaminifu na kumshawishi mwanao kuamini kwamba wao sio watu wabaya au wageni kwenye maisha yake kwa sababu "ona mpaka najua ndugu zako wote na marafiki zako mpaka mama yako na baba yako nawajua!"

 Kama kuna haja ya kuweka picha zao basi usiandike majina yao kamili na tarehe zao za kuzaliwa. marafiki zako wa kweli hata hivyo si wanamjua mwanao tayari?

 Najua wazazi wengi wanajivunia watoto wao na wanatamani dunia nzima wajue kuwa wanawapenda wanao. Lakini "Kama kweli unampenda, utamlinda".

Chanzo:tanganyikanblog

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment