Saturday 16 March 2013

[wanabidii] TANGAZO: KATIKA KUITAFUTA JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR YENYE MAMLAKA KAMILI

Haya haya wazanzibari! Kumekucha! La mgambo likilia kuna jambo! Chama cha wananchi CUF kinawatangazia wanachama, wapenzi na wazanzibari wote wa mikoa miwili ya Pemba, wazalendo na wapenda nchi yao kwa jumla kuhudhuria kwa wingi katika mkutano  mkubwa wa hadhara wa  aina yake utakaofanyika leo Jumamosi tarehe 16/03/2013 katika viwanja vya Tibirinzi, Chake Chake, Mkoa wa Kusini Pemba. Mgeni rasmi katika Mkutano huo ni Simba wa nyika, tishio la vibaraka wauza nchi yetu, kipenzi cha wazanzibari, mwenye  uzalendo wa hali ya juu na mapenzi makubwa kwa Zanzibar na wazanzibari, Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.

Agenda kuu katika mkutano ni kwa nini wazanzibari wanataka mamlaka kamili ya nchi yao? ni jinsi gani wazanzibari wanavyopaswa kujipanga kuelekea kuitia mikononi mwao Zanzibar yao yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa? Kwa nini  muungano wa MKATABA na Tanganyika badala muungano wa kinafiki uliopo sasa hauepukiki?.

Halkadhalika hali ya kisiasa na madudu yanayojiri nchini wakati huu wa mpito kuelekea Zanzibar mpya yatazungumzwa na kufafanuliwa. Mkutano utaanza saa 8 barabara za mchana hadi saa 12:00 jioni.

Hatumwi motto! Shime wazanzibari wote kuhudhuria kwa wingi bila ya kukosa!

TUNATAKA NCHI YETU SASA TUMECHOKA TAFRANI!

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment