Tuesday 19 March 2013

[wanabidii] RE:Wakikuyu wanatwaa ardhi Arusha?


Chambi na Wasimbeye,
Chambi aksante kuliona hilo. Mimi binafsi nitofautiane na wa-Simbeye juu ya mawazo yake. Japo sheria hairuhusu mgeni kununua ardhi hatupaswi kuwaacha wachukue ardhi alafu baadae ndipo tuende kuwapinga mahakami. Tukiacha ifikie hapo tutapata shida sana mbeleni, hasa ukizingatia udhaifu wa vyombo vyetu vya kutoa haki kama polisi na mahakama kutokana na RUSHWA. Kumbukeni kuo hao Wakenya Kwa sasa wanatumia pia KETE AU UJANJA wa kuoa dada zetu ili wapate haki za-Watanzania hasa Ardhi. Kimsingi hawana haja ya kuwaoa ila wanataka kuhararisha kiu yao ya ardhi. Ikiwezekana tunapaswa kukaza sheria kua wanapowaoan dada zetu ardhi iandikishwe kwa jina la mwanamke.

Chamsingi ndugu zangu tunapaswa kuwafundisha watu wetu juu ya umhimu wa ardhi hasa katika kipindi hiki ambapo ardhi inatafutwa na mataifa mengi. Wakenya wameshindwa kutatua masuala ya ardhi internally-maana wameacha watu wachache kujimilikishia maeneo makubwa; ndio maana matukio ya mapigano juu ya ardhi Kenya ni mengi sana . Kwa mtizamo wangu nchi nyingi tulizojiunga nazo kwenye hii EAC na hasa Kenya lengo lao kubwa nikutumia EAC kutatua matatizo yao ya ndani hasa suala la ardhi. Yatupasa tuwe macho sana. Watanzania tunatakiwa kufumbua macho na kuona nje ya BOX kinachoendelea. Mara nyingi viongozi wanasaign mikataba ambayo itatuacha solemba mbeleni kama taifa.
Alexander


From: Finnigan wa Simbeye <f_simbeye@yahoo.com>
To: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Sent: Tuesday, March 19, 2013 2:10 PM
Subject: Re: [Mabadiliko] Wakikuyu wanatwaa ardhi Arusha?

Chambi,

Wameliwa hao, ardhi siyo swala la Jumuiya na sheria yetu inakataza mgeni kumiliki ardhi, watanunua lakini mwishowe watu watawarudi baada ya kwenda mahakami. Wanaweza kupata ardhi kama wawekezaji kupitia TIC. Waache waje nami nawashauri Watanzania mlioko na ardhi Arusha wauzieni then mwende mahakamni hawana chao!!

wa Simbeye



--- On Tue, 3/19/13, Chambi Chachage <chambi78@yahoo.com> wrote:

From: Chambi Chachage <chambi78@yahoo.com>
Subject: [Mabadiliko] Wakikuyu wanatwaa ardhi Arusha?
To: "Wanazuoni" <Wanazuoni@yahoogroups.com>
Date: Tuesday, March 19, 2013, 2:02 PM

Mfuatiliaji wa kwa karibu wa masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anasema kuwa katika miaka ya 70 baada ya Arusha kufanywa makao makuu ya jumuiya hiyo, Wakikuyu wengi walinunua/walitwaa ardhi hapo. Hivyo, Arusha ikaanza kuwa kama sehemu ya Kenya na fedha ya Kenya ikawa ndio inadaiwa/inatumika katika mahoteli, maduka n.k. Kwa mujibu wa maelezo yake, hali hii ilikoma baada ya Tanzania kufunga mpaka wake na Kenya katika mtafaruku wa kuivunja jumuiya hiyo.

Mdau huyo anasisitiza kuwa tukio hilo lilisababisha Wakikuyu warudi/wakimbilie kwao Kenya. Sasa anaona wanarudi kwa kasi sana na anahisi Watanzania hawana wasiwasi kabisa. Anashauri watafiti wa masuala ya ardhi watathmini kwa kina ni kiasi gani cha ardhi huko Arusha kimeshatwaliwa na Wakikiyu. Hofu yake ni kuwa ushindi wa Uhuru Kenyatta unaweza kusababisha hali hii izidi hasa katika muktadha wa kuiimarisha Arusha kama makao makuu ya Jumuiya mpya ya Afrika Mashariki. 

"Kwa kuwa Arusha sasa imekuwa kitongoji cha Nairobi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ni vyema kutathmini ardhi inayotwaliwa na Wakikuyu" - Mdau Mfuatiliaji
--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
 
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 
--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
 
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 




0 comments:

Post a Comment